Ushauri: Law School iwe na mtihani wa kuchuja waombaji

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,088
2,000
Wadau nawasalimu nyote.

Mimi ni mdau wa Sheria. Nimekuwa nafuatilia sana Shule hii ya Masuala ya Sheria "LAW SCHOOL". Kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wanaomaliza mafunzo yao ya sheria katika Vyuo mbalimbali hapa Nchini.

Kwa uzoefu wangu ufundishaji wa Vyuo vingi ni wa kiwango cha chini sana.Na baada ya kuhitimu mafunzo yao Wanavyuo huomba kujiunga na Law School.

Kutokana na matokeo ya Law School kuonyesha kuwa Wanavyuo wengi hushindwa kufaulu mafunzo hayo.

Nashauri Law School iwe na utaratibu wa kuandaa Mtihani kwa waombaji wake ili wasio na uwezo wachujwe mapema kuliko kuendelea na utaratibu wa sasa wa kuwapokea wote walioomba na mwisho kuwa na matokeo ya kutia aibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,037
2,000
Hiyo ni sawa na kusema wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza wapewe mtihani ili hali walishafaulu tayari!

Ungeshauri shule ziongezwe ikibidi kila kanda, ningekuelewa zaidi. Kulundika wanafunzi wa nchi nzima eneo moja nalo ni tatizo linalopunguza tija kwenye ufundishaji.
 

BenKaile

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
448
500
I thought you have passed from the school with whatever experience you came out with from there, kumbe ni mdau wa nje. Aisee kazi kweli kweli. Sitapenda kukudharau ila naona ujaelewa mantiki ya Law school inavyo operate na hata elimu ya mahakama Lushoto, mathalani maarifa yako yameishia kiwango hicho, keep it up!
 

GODZILLA

JF-Expert Member
Dec 26, 2014
4,664
2,000
Wewe ni mjinga tu na inawezekana una ujinga mwingi kuliko hao wanaofeli huko law school.
 

Dar_Millionaire

JF-Expert Member
Aug 6, 2008
227
225
Wadau nawasalimu nyote.Mimi ni mdau wa Sheria.Nimekuwa nafuatilia sana Shule hii ya Masuala ya Sheria "LAW SCHOOL"Kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wanaomaliza mafunzo yao ya sheria katika Vyuo mbalimbali hapa Nchini.Kwa uzoefu wangu ufundishaji wa Vyuo vingi ni wa kiwango cha chini sana.Na baada ya kuhitimu mafunzo yao Wanavyuo huomba kujiunga na Law School.Kutokana na matokeo ya Law School kuonyesha kuwa Wanavyuo wengi hushindwa kufaulu mafunzo hayo.Nashauri Law School iwe na utaratibu wa kuandaa Mtihani kwa waombaji wake ili wasio na uwezo wachujwe mapema kuliko kuendelea na utaratibu wa sasa wa kuwapokea wote walioomba na mwisho kuwa na matokeo ya kutia aibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukichuja watu utapataje hela? Waache wapokee tu, kwani umesikia kufaulu ni lazima? Kulipa ada ndo lazima.
 

Dar_Millionaire

JF-Expert Member
Aug 6, 2008
227
225
Hiyo ni sawa na kusema wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza wapewe mtihani ili hali walishafaulu tayari!

Ungeshauri shule ziongezwe ikibidi kila kanda, ningekuelewa zaidi. Kulundika wanafunzi wa nchi nzima eneo moja nalo ni tatizo linalopunguza tija kwenye ufundishaji.
Acha uchawi. Wawekezaji tunapiga hela ndefu Sinza hapa kutoka kwa hawa mawakili watarajiwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom