Ushauri: Kwanini Hazina wasianziashe zone - financial account kulingana na kanda mbalimbali

scatter

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
1,667
925
Lazima tukubali uchumi wa nchi yetu ili ukue kwa kasi katika kila kanda hasa kwenye miradi ya maendeleo kuna ulazima wa serikali kama wanaweza wagawe kanda za kiuchumi na kuwe na account maalum pale hazina inayosimamia miradi hii

Mfano pawe na South economic zone accout, central economic zone,middle economic zone, west economic zone,east economic zone na north.

Hizi account zitasaidia kurahisisha ufanisi wa maamuzi ya matumizi ya pesa za umma na hata kuzuia ubadhirifu kwani makusanyo ya pesa yatakua yanajulikana kwa kanda zote hivyo ufuatiliaji wa pesa hizi unakua rahisi sana.

Pia itazifanya halmashauri mbalimbali kujua wanakwama wap kwenye makusanyo kwa kila kanda.

Pia ipo haja ya kubuni mfumo wa DIGITAL ambao utakua una - link kati ya takukuru na hazina nchi nzima kuweza kuzifuatilia hizi pesa maana kwa hali ya sasa tunaona uzembe na ubadhirifu ukishafanyika then ndio wanaitwa takukuru wachunguze kodi zetu zilizopetea ìnauma sana maana inachuka muda watu wanafilisiwa au wanafungwa lakini pesa zimeshapotea.

Pia hii link ya kidigital IWE SPECIAL KATI YA HAZINA ,TAKUKURU,NA OFISI YA CAG ambao kama itafanya kazi nafasi za ajira zitakuwa nyingi kwa kada mbali mbali na itakua ni muarobaini wa kukomesha matumizi mabaya ya fedha ya umma.

Hazina ya sasa ina usiri mkubwa sana ndio maana rushwa hazitaisha tutawaonea sana wakurugenzi tutalazimisha sana watu wafanye mambo ambayo si taaluma zao then kitakacho kuja kutukea ni ubadhirifu ,wizi mkubwa kwenye pesa za maendeleo kwa hii miaka mitano ya mwisho.

Kama litafanikiwa hili ma Dc ,RC DAS na RAS na wenyeviti wa vyama wataweza kufanya kazi bila pressure kwani watakuwa wamezungukwa na watalaam.

Ukweli lazima usemwe.
 
Nchi hii kwa sasa ina ombwe la mawazo/ubunifu.

Tunatumia muda mwing kujadili matatizo na watu wanaotusababishia matatizo huku tukitumia muda mchache kubuni vitu vitavyazuia matatizo au kutuoa suluhu ya matatizo tuliyonayo kama nchi.

Njoo na hoja ya namna ya kutatua tatizo fulani na mwingine aje na hoja juu ya tatizo fulani halafu uone ni ipi itajadiliwa zaidi.
 
Hata kwa mfumo huu wa sasa hizo taarifa unazotaka kuzijua mbona Hazina wanazo kwa maeneo mbalimbali,namaanisha kila mkoa mchango wake kiuchumi kwa Taifa unajulikana na taarifa hizo zipo,labda kama unataka kuboresha mahali ktk bandiko lako
 
Yaani kuna Watanzania type yako wanaofikiria tatizo la uchumi ni ukusanyaji wa pesa badala ya ukweli kwamba kuna tatizo la uzalishaji kwenye uchumi wetu.

Kodi inatokana na uzalishaji lakini Tanzania hakuna uzalishaji wa kutosha hivyo tuweke mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye kilimo mfano na kuongeza ajira kwa vijana.

Uwekeaji bado ni mdogo sana sana na tuwekeze kwenye elimu ya teknologia ya kisasa na tupate wataalamu kwenye technologia .

Wafanyakazi wa serikali au bandari wakila pesa za kodi hilo ni tatizo la uendeshaji sio tatizo la kodi
 
Hata kwa mfumo huu wa sasa hizo taarifa unazotaka kuzijua mbona Hazina wanazo kwa maeneo mbalimbali,namaanisha kila mkoa mchango wake kiuchumi kwa Taifa unajulikana na taarifa hizo zipo,labda kama unataka kuboresha mahali ktk bandiko lako
Kama wanazijua kwanini pesa zinatumika vibaya?

Kwa nini wizi upo?

Kwanini wakurugenzi waonekane wanafanya matumizi mabaya ya pesa?
 
Wazo lako si sahihi linapingana na aina ya Utawala uliopo. We unazungumzia mambo ya transparency open government, inawezekana kwenye tawala za kidemokrasia na sio za kijamaa, kikomunisti na kidikteta huku KILA kitu ni Siri.
 
Kama wanazijua kwanini pesa zinatumika vibaya..??
Kwa nini wizi upo?
Kwanini wakurugenzi waonekane wanafanya matumizi mabaya ya pesa?
Zile nyimbo za kudhibiti rushwa, wizi na ufisadi huwa ni za majukwaani Hali halisi uwaumbua
 
Yaani kuna Watanzania type yako wanaofikiria tatizo la uchumi ni ukusanyaji wa pesa badala ya ukweli kwamba kuna tatizo la uzalishaji kwenye uchumi wetu. Kodi inatokana na uzalishaji lakini Tanzania hakuna uzalishaji wa kutosha hivyo tuweke mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye kilimo mfano na kuongeza ajira kwa vijana...
Unakusanyaje pesa wakati huna vyanzo vya pesa.

Sipo huko mkuu namaanisha hizi kanda za ki uchumi zikiwepo zitachochea upatikanaji wa ajira. Mfano mdogo kama itatengwa kanda za kusini wanalima sana korosho chai maparachichi hivyo katika makusanyo yao kuna asilimia lazima iwepo kwenye kanuni za hazina kuu za kuwaboreshea masoko yao madawa na hata ikiwezekana kuanzishiwa viwanda vya malighafi hivyo hivyo kwa kanda ya Magharibi Kaskazini na hata mashariki kuliko kwa sasa pesa zi kusini zinajenga Dar, pesa za dar zinajenga Magharibi lazima uchumi wa watu uwe mgumu
 
Wazo lako si sahihi linapingana na aina ya Utawala uliopo. We unazungumzia mambo ya transparency open government, inawezekana kwenye tawala za kidemokrasia na sio za kijamaa, kikomunisti na kidikteta huku KILA kitu ni Siri.
Kwani serikali yetu si ya uwazi na ukwel i au umesahau
 
Tatizo la awamu hii wao wanadhani tatizo ni ukusanyaji thus wanawakamua wananchi KILA kona na still Bado awapati makusanyo.

Shida sio ukusanyaji shida ni uzalishaji, Kama uzalishaji, uchochei kuzalisha utakusanya toka wapi.

Nguvu Kazi haitumiki, vijana awatumiki vya kutosha Ili watumie raslimali zilizopo Ili tuongeze export.

Kama uchochei export umekazania tu kubuni ukusanyaji ni ngumu kuwa na ziada.
 
Tatizo la awamu hii wao wanadhani tatizo ni ukusanyaji thus wanawakamua wananchi KILA kona na still Bado awapati makusanyo. Shida sio ukusanyaji shida ni uzalishaji, Kama uzalishaji, uchochei kuzalisha utakusanya toka wapi. Nguvu Kazi haitumiki, vijana awatumiki vya kutosha Ili watumie raslimali zilizopo Ili tuongeze export. Kama uchochei export umekazania tu kubuni ukusanyaji ni ngumu kuwa na ziada.
Magu haijui theory ya DIMINISHING RETURNS
 
Kwani serikali yetu si ya uwazi na ukwel i au umesahau
Characteristics zinagoma.
.Uhuru wa habari
. Demokrasia
.Uwazi wa mikataba.
.Bungelive
.Uhuru wa utoaji maoni
.Ushirikishwaji wa walipa kodi kwenye mipango ya matumizi ya Kodi zao ikiwemo vipaumbele vya wananchi.Tofautisha vipaumbele vya wananchi na vipaumbele vya watawala.
 
Udini/Ukanda unawafanya msifanye mambo ya maendeleo, kubaki kulalalamika na kukodolea macho mkono wa binadamu kama fisi kufikiri utaanguka.
 
Magu haijui theory ya DIMINISHING RETURNS
Ajui kwamba trekta ni muhimu kuliko ndege,trekta ukuza zaidi uchumi kuliko ndege,trekta uajiri wengi mara 300 ya walioajiriwa kwenye ndege,trekta uleta fedha nyingi Sana za kigeni tena kwa mda mfupi kuliko ndege.

Huwezi endelea kwa kukopa na kutegemea kukusanya tu pasipo kuzalisha. Na huwezi zalisha Kama purchasing power ya watu imekufa. Mfano utakusanya nn toka kwa mtu aliyekuwa anamudu kula milo 3 kwa siku leo anakula mlo mmoja tena mara 4 kwa wiki means sababu ya kusomeshwa namba uwezo wake wa kununua umekufa ambayo kiuchumi ni hatari Sana.

Uchumi ni sayansi na unahitajika reasoning capacity na sio claiming capacity.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom