Ushauri: Kwanini Hazina wasianziashe zone - financial account kulingana na kanda mbalimbali

Unatuletea mambo ya Ethiopia na majanga ya tigrey
Wamejitahidi kutugawa kwa makabila wameshindwa, kwa dini wameshindwa sasa wanakuja na mipango isiyoeleweka

Mungu ibariki Tanzania
 
lazima tukubali uchumi wa nchi yetu ili ukue kwa kasi katika kila kanda hasa kwenye miradi ya maendeleo kuna ulazima wa serikali kama wanaweza wagawe kanda za kiuchumi na kuwe na account maalum pale hazina inayosimamia miradi hii...
Pia usisahau kushauri vitengo maalumu vya makusanyo viongeze juhudi katika makusanyo,ili hats wanyonge wajinyonge vizuri.
 
Tatizo kubwa la nchi yetu haina mfumo wa uongozi ulio madhubuti na imara
Tokea enzi ya mwalimu kila kiongozi au uongozi unaoingia madarakani unakua na kazi ya kurekebisha makosa ya uongozi ulioutangulia.

Ali Hassan mwinyi alianza na kurekebisha makosa ya uongozi was mwalimu nyerere.

Benjamin mkapa alianza na kurekebisha makosa yaliotokana na uongozi wa All Hasan mwinyi.

Jakaya kikwete nae alianza kwa kurekebisha makosa ya Benjamin mkapa.

John maguful alipoanza yeye alianza kurekebisha makosa si ya jakaya kikwete tu bali yokea ya enzi za mwalimu.
Kule kusema wale waliomtangulia hawakufanya kitu Bali yeye ndie anaefanya huko ni kukosoa na kufanya marekebisho ya mfomo wote uliowekwa na kila kiongozi.

Kuna mifumo mingine iliowekwa na viongozi waliomtangulia ambao Kama walewalipokea huo uongozi wangeendelea nayo Leo hii tusingwkua tunazungumza namna hii.

Walao jakaya alitembea katika mfumo aliouasisi mkapa kidogo hayakuonekana makosa Kama yanayonekana katika awamu hii.

Kusema ukweli Kama kunamtu atapata shida isiyo ya mfano ni huyo kiongozi ajae baada ya magufuli. Sijui ataanza moja, ama atarekebisha Nini na Nini aache ukizungatia ni miaka mitano.

Laiti kungalikuwepo na mfumo ambao unamueeka kiongozi anaeingia madarakani katika kifungo Cha kutokuvunja kile kile kilichowekwa na uongozi uliopita tungepiga hatua.

Hii ya kurekebisha makosa itatuchelewesha sana tena sana.

Mifumo ya kodi na ukusanyaji Kodi ulishawekwa madubuti laki kila anaekuja anakuja na lake.

Tukirudi mwaka wa 2000 uongozi wa mkapa uliandaa dira ya taifa Kati ya 2000 na 2025 ambao ndani yaje kulikua na mfumo wa ukusanyaji was mapato.

Lakini kabla ya huo mwaka wa 2025 hakuna tena Cha dira ya taifa Wala ya mtu mmoja mmoja kila my analia kivyake! Na hakika haya hayakuwa malengo ya dira au vision ya taifa kwa miaka 25 iliokua ifuatie.
 
Kama wanazijua kwanini pesa zinatumika vibaya..??
Kwa nini wizi upo?
Kwanini wakurugenzi waonekane wanafanya matumizi mabaya ya pesa?
Unafikiri matumizi mabaya ndio yanasababishwa na kutokuwepo kwa hizo kanda??

Kufanya matumizi mabaya ni kitu personal hakuzuiwi na kuwepo kwa hizo kanda,kwenye kanda hizo hizo kama mtu ni mpigaji atapiga tu kama kawaida.
 
Tatizo tunakusanya wkt kuzalisha ni kudoho sana.Mkulima hana uhakika wa soko,matokeo bidhaa zetu tunatumia wenyewe tena bila uhakika wa soko.
 
Back
Top Bottom