abudist
JF-Expert Member
- Oct 25, 2009
- 850
- 780
Yono Auction Mart mnafahamu hii siyo mara ya kwanza kwamba minada inaharibiwa makusudi na baadhi ya watu. Lakini inaonyeshwa Yono hawana njia ya kuzuia uharibifu huu zaidi ya kutegemea sheria ya kusubiri kwanza mnada uharibiwe ndiyo mtu mnunuzi bandia achukuliwe hatua. Kwani nini mnasubiri mtu afanye kwanza kosa kwanza badala ya kukinga??? Kumsomea mtu masharti ya mnada haitoshi kuzuia uharibifu.
Kumbukeni mnanadi mali za mamilioni kama siyo mabilioni lakini mchakato wenu wa zabuni za mnada ni wa kizembe kama vile mnauza vitu visivyozidi mali isiyozidi shs 10,000! Tena mnanadi mali hizi zingine kubwa kwa niaba ya serikali. Hivi inakuwaje mtu anatokea tu ghafla na kuanza kupanda dau la mnada wakati hamna hata habari zake fupi za uwezo wake.
Mnapoteza muda wa bure
USHAURI: Fanyeni pre-screening interview kwa wateja wenye nia ya kununua mali mnazonadi.

- Tangazeni vitu mnavyotaka kuuza na thamani yake yaani bei ya (Reserve Price) ambayo mali hiyo haitauzwa chini ya hapo. Yaani ndiyo thamani ya mali yenyewe ilivyothaminiwa.
- Tangazeni watu wanaotaka kushiriki mnada kujiandikisha kwenu na pia kuwasilisha baadhi ya vielelezo muhimu kama vile, vitambulisho, kazi wanazofanya, uwezo wao wa kifedha, mfano bank statements, barua ya mwajiri, kama mfanya biashara - jina la kampuni, TIN, Income tax, Corporate Tax reports etc...
- Tumieni vielelezo hivyo kujiridhisha kwa njia za kisheria kwa kushirikiana na benki, mwajiri, na TRA kama ni kampuni ndiyo mnunuzi kujua kama mnunuzi mtarajiwa ana uwezo kulipa mali anayotarajia kununua. Hii ni pamoja na kulipia hiyo asilimia 25 mnayotaka ilipwe mara tu mnada unapomalizika.
- Hivyo baada ya uchunguzi huu watu mliofanya mahojiano nao wasiokidhi vigezo mnawaondoa katika hatua hii. Hawa wanaitwa 'time wasters'. Na watu waliokidhi vigezo mnawaalika kushiriki katika minada yenu. Na wanasaini