Ushauri kwa Yono Auction Mart na wanadi wengine jinsi ya kuendesha minada.

abudist

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
850
780
Yono Auction Mart mnafahamu hii siyo mara ya kwanza kwamba minada inaharibiwa makusudi na baadhi ya watu. Lakini inaonyeshwa Yono hawana njia ya kuzuia uharibifu huu zaidi ya kutegemea sheria ya kusubiri kwanza mnada uharibiwe ndiyo mtu mnunuzi bandia achukuliwe hatua. Kwani nini mnasubiri mtu afanye kwanza kosa kwanza badala ya kukinga??? Kumsomea mtu masharti ya mnada haitoshi kuzuia uharibifu.

Kumbukeni mnanadi mali za mamilioni kama siyo mabilioni lakini mchakato wenu wa zabuni za mnada ni wa kizembe kama vile mnauza vitu visivyozidi mali isiyozidi shs 10,000! Tena mnanadi mali hizi zingine kubwa kwa niaba ya serikali. Hivi inakuwaje mtu anatokea tu ghafla na kuanza kupanda dau la mnada wakati hamna hata habari zake fupi za uwezo wake.
Mnapoteza muda wa bure
USHAURI: Fanyeni pre-screening interview kwa wateja wenye nia ya kununua mali mnazonadi.
  1. Tangazeni vitu mnavyotaka kuuza na thamani yake yaani bei ya (Reserve Price) ambayo mali hiyo haitauzwa chini ya hapo. Yaani ndiyo thamani ya mali yenyewe ilivyothaminiwa.
  2. Tangazeni watu wanaotaka kushiriki mnada kujiandikisha kwenu na pia kuwasilisha baadhi ya vielelezo muhimu kama vile, vitambulisho, kazi wanazofanya, uwezo wao wa kifedha, mfano bank statements, barua ya mwajiri, kama mfanya biashara - jina la kampuni, TIN, Income tax, Corporate Tax reports etc...
  3. Tumieni vielelezo hivyo kujiridhisha kwa njia za kisheria kwa kushirikiana na benki, mwajiri, na TRA kama ni kampuni ndiyo mnunuzi kujua kama mnunuzi mtarajiwa ana uwezo kulipa mali anayotarajia kununua. Hii ni pamoja na kulipia hiyo asilimia 25 mnayotaka ilipwe mara tu mnada unapomalizika.
  4. Hivyo baada ya uchunguzi huu watu mliofanya mahojiano nao wasiokidhi vigezo mnawaondoa katika hatua hii. Hawa wanaitwa 'time wasters'. Na watu waliokidhi vigezo mnawaalika kushiriki katika minada yenu. Na wanasaini
Msipobadilika mtajikuta kila siku mnawapepea na kuwaimbia wasanii kama Professor Louis Shika. Matokeo yake mtakosa hizo percentange zenu za commission ya mauzo, na mwishowe tender mtanyang'anywa wapewe watu wenye akili. Kuweni wabunifu msifanye biashara kizamani.
 
Naomba kuuliza kitu kimoja.

Jumba ya Upanga ambalo dakta Luis alishinda bidding likikuwa limeashauzwa kabla ya hapo.

Cheki hawa waarabu walivyoshinda mnada kwa milioni 700.



Sasa ikawaje tena jumba likarudi sokoni na kuchukuliwa na dokta Louis?

Ni kwamba wakati wa malipo hii minada yao huwa inaenda ina baunsi? Na kwa nini hawa waarabu hawakuchukuliwa hatua kwa kushindwa kulipa milioni 700?
 
Namba 2 na namba 3 hapo juu hilo jambo haliwezekani.

Taarifa za kampuni ni siri na hutakiwi kuzi-expose hovyo hovyo isipokua kwa sababu maalum

Yono wana minada mingi, sasa kama kila siku wakiwa wanapokea bank statements za watu wanaoonyesha maslahi, una uhakika gani wa usalama wa taarifa zako kutokwenda mahala pengine maana yono sio taasisi ya serikali.

Huwezi kuruhusu mtu kienyeji apate access financial position au liquidity position yako kienyeji enyeji tu.

Hayo mambo hayawezekani bado.

Bado utaratibu wa yono ndio njia rahisi na salama kwa watu kwa sasa.

Hayo mambo mengine huwezi kuyaignore completely, ujinga unatokea tu.
 
Back
Top Bottom