Ushauri kwa wizara ya maliasili - kuuza wanyama pori nje ya nji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri kwa wizara ya maliasili - kuuza wanyama pori nje ya nji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtazamaji, Dec 18, 2010.

 1. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi
  Kuna tatizo kubwa serikali yetu kuingia mikataba inayolinda maslai ya watanzania

  Baada ya kunagalia documentary moja ya kipindi cha wanyama pori walioko zoo moja huko ulaya mimejiuliza maswali mengi..... Lakini baada ya kujiuliza maswali nimekuja na mapendekezo ambayp yakiwekwa mikataba ya kuuza wanyama wetu nje inaweza kuwa na manufaa zaidi tuliyonayo sasa.

  Pendekezo la Kwanza

  Tikiwapa/Tkiwauzia wanayama wetu tuwawkeee kipengele cha hati/haki miliki ibaki kwetu. Hata wanyama wataozaliwa na yule mnyama bado iwe haki miliki yetu.Tuweke kipengele ambapo huyo myama atakapokuwa yatawekwa maandishi kuwa katoka tanzania na apewe jina la kitanzania . Tuweke kipengele pia tukimuhitaji mnyama wetu tutamdai na kumrudisha na kuwarudishia peza zao.

  Ikiwezekana mnyama akifa arudishwe tanzania kwa gharama zao afanyiwe mazsihi rasmi
  . No for this am joking


  Pendekezo la Pili
  Kwa kila mnayama aliyeuzwa kupelekwa kwenye zoo tutoze dola moja au mbili kwa siku kwa siku zote atakazokuwa kwenye zoo za huko ulaya. Hela zitakazo patikana ziingizwe kwenye mfuko wa kuhifadhi wanyama walio katika hatari ya kupotea.


  Nimeshanga kuona wazungu wanahamisha mbuga za wanyama kwao.

  Nimeshanga kuona zoo zinapata watalii na mapato kuliko hta serengeti na wale watalii shida yao ni kuona simba chui, etc.

  Vipengele hivi naona ni mikataba endelevu kwa manufaa ya watanzania.

  Nawasilisha kwa mjadala
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Wachina wanakodisha wanyama wao panda kwa dola milioni moja kwa kipindi cha miaka kadhaa kwa zoo za Marekani. Ni sisi tu tuliozubaa tunawaruhusu wale Waarabu wa Loliondo wazoe wanyama wapendavyo eti ni wawekezaji.
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu wewe naona umekuja na wazo bora badala ya kuwauza tuwakodishe hawa wanyama wetu. Hii imekaa vizuri.

  Inashangaza Nimeona sehemu ya zoo imeitwa East african area.. wamei "customise" kwa mazingira na hali ya hewa ya africa mashriki. Ile zoo inaiba watalii wengi sana wa frica mashariki na hakuna sehemu wantangaza nchi walizotoka
   
 4. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,859
  Likes Received: 4,539
  Trophy Points: 280
  Usafirishaji na uuzaji wa LIVE ANIMALS is prohibited! Kwaiyo huo mpango utakua redundant. Dawa ni kuenforce iyo sheria,then kutangaza zaidi vivutio vyetu na kuonyesha tofauti ya kutembelea ZOO na a real game reserve or national park.
   
 5. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Prohibited kivipi Mkuu? Hii hi habri nzuri lakini kam ni kweli. imekuwa prohibiited lini? Mi nimeona documentary wanasema mnyama kasifirishwa mwaka huu na yuko kwenye zoo huko ulaya.

  Sasa tofauti ya zoo na geme reserve si njia moja wapo ni kuwaforce kwa njia ya mikataba hao wenye zoo kuweka matangazo na mabango nchi lipotokamnyama fulani

  Mimi nimeongelea kipingele wanachoweza kuweka kwenye mikataba ya kuuza/kukodisha wanyama ili wanyama hao watumike zaidi kutangaza wanapotoka kuliko ilivyo sasa.
   
 6. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,859
  Likes Received: 4,539
  Trophy Points: 280
  Joh! Unaifahamu CITES? Wale jamaa walioizuia TZ kuuza zile pembe za ndovu! TZ ni mmoja wa wanachama wa CITES. Sasa hawa CITES wameweka sheria zinazozuia uuzaji na usafirishaji wa wanyamapori walio HAI. Ukiona wanauzwa na kusafirishwa kwenda nje,ujue ni ILLEGAL like what's happening in Loliondo Game Controlled Area,whereby Arabs are said and seen to be engaged in transporting live animals to UAE! Ndo ivyo arif Bongo yetu kwishnei!
   
 7. shejele

  shejele Senior Member

  #7
  Dec 18, 2010
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Unachosema Nyandaigobeko ni kweli kabisa, tena si kuuza na kusafirisha wanyamapori tu hata kusafiri sehemu za baadhi ya wanyama kwa research purpose lazima uwe na kibali toka CITES. Hao wanyama aliowaona jamaa yetu ndio itakua waliosafirishwa kwa njia za panya.
  Tukitaka kuongeza kipato kupitia wanyama wetu, ni kuongeza bidii kwenye kujitangaza zaidi vinginevyo tutakuwa tunaona wenzetu wanafaidika na maliasili zetu.
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Ndiyo maana utalii wa wanyama umepungua sana, wengi wanaongia nchi ni kwa utalii wa kupanda mlima Kilimanjaro, na mapumziko kwenye fukwe za Zanzibar
   
 9. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  ndio kama wanasoma jf waone vipengele japo vya kuboresha hiyo mikataba .
  Tutakalia tunajisifia kuwa tuna mbuga kubwa ya wanyama dunianiani lakini idadi ya watalii na mapato wanaotembelea mbuga inanzidiwa na ZOO ya UK au US.
   
Loading...