Ushauri kwa Wizara ya Fedha ili kufikia lengo la kuwa na mapato mengi ya ndani

Jul 11, 2020
64
139
Nimeona Video ambayo Waziri wa fedha anawaambia watu wa idara zote zinazohusika na ukusanyaji wa mapato ya kodi na yasiyo ya kodi ya serikali kukusanya mapato mengi ili malengo ya serikali ya awamu ya tano yatimizwe na fedha za ndani

Mbali na haya yote mimi nasema fedha nyingi zinaweza kupatikana mahakamani. Dkt. Mipango kama utapita kusoma hama naomba ujue hili,

Kuwafunga watu jela kwa kosa la ambalo ni la kawaida itakuwa ni suala la ajabu badala yake mtu apewe option ya faini ili fedha ziongezeke. Makosa kama kutumia laini kwa jina la mtu mwingine, makosa ya mtandao nk hayana madhara mtu akibaki uraiani hivyo hakuna haja ya kukomoana.

Hata vituo vya matangazo kama redio, tv na magazeti havina haja ya kufungiwa, kwa kuwa inaathiri uchumi wa walioajiriwa katika sejktta hizo, badala yake makosa hayo yawe ni kulipa faini tu.

Makosa ya kustahili mtu kukaa jela yawe ni kujeruhi, Uhaini na yenye ufanano na hayo. Haya mengine inabidi yaiingizie nchi kipato ili tuache utegemezi.

Nawasilisha, naenda zangu kusolve another mathematical Equation
 
Ungejua wengi walio-jela ni walioshindwa kulipa faini ungejikita tu 'kusolve mathematical equations'
 
Ni tofauti ipi kimaisha u mehisi tokea tuambiwe tuko Uchumi wa kati ukilinganisha na Uchumi wa Chini tuliokuwa nao?
 
Kwa nini unatoa ushauri na kuifundisha serikali kutumendea ili tuuze mashamba yetu ya urithi kwa bei ya kutupwa ili tuwanusuru ndugu zetu walishitakiwa.
 
Back
Top Bottom