getrusa
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 2,150
- 1,812
Salaam,wana Jamvi!
Ninatoa wito kwa Wizara ya Elimu kutambulisha sare rasmi kwa walimu wa shule za msingi na Sekondari hapa Nchini.
Kutokana na utafiti usio rasmi niliofanya kwa shule nyingi hapa kwetu Tanzania walimu 8 kati ya 10 walipenda kuwe na vazi rasmi la kazi kwa sababu zifuatazo:
1. Vazi rasmi linapunguza gharama za kununua mavazi mengi, mfano kwa mwalimu wa kike angetamani kuwa nadhifu muda wote awapo kazini, ili kuepusha fedheha ya kurudia mara kwa mara nguo fulani analazimika kuwa na nguo nyingi, katika hali hiyo ina maana pia bajeti yake ya mavazi inaongezeka.
2. Kuweka hali ya Usawa kwa walimu wote izingatiwe kuwa watoto ni wepesi kusoma muonekano wa mavazi ya mwalimu ikiwa na maana mwalimu anayetoka katika familia yenye kipato mavazi yake yanaweza kuwa na thamani kubwa kuliko wenzie.
Hali hii inaondoa usawa wa kifikra kwa walimu na bila shaka unaondoa namna fulani ya kujiamini kisaikolojia hasa kwa walimu wa kike.
3. Kutunza nidhamu na haiba kunapokuwa na vazi maalumu au sare ni rahisi kutunza haiba na muonekano wa mwalimu ambapo ni tofauti na sasa ambapo kila mwalimu huja na vazi ambalo yeye anaona lina mpendeza na limemkaaa, hapa inategemea sana na hekima ya mwalimu wapo wanaovaa nguo ambazo haziko sawa kwa maadili ya watoto japo sio wote.
4. Kama serikali ikiwa na mfumo rasmi hili ni soko tayari kwa viwanda vyetu vya ndani ambapo idadi ya walimu nchi nzima, wakiwa na sare kuna uhakika wa kuuza nguo zinazotengenezwa hapa hapa nchini kwetu.
Mwisho ipo mifano ya nchi ambazo walimu wana vazi lao rasmi mathalani ukitembelea karibu shule zote za serikali Zambia walimu wana vaa makoti Meupe kama yale ya madktari wawapo kazini.
Ama kule Zanzibar kuna shule ambazo wao tayari wana utaratibu wao wa sare za kazi.
Isisahaulike kuwa walimu hawa siku ya maadhimisho ya wafanyakazi wanavaa sare ama katika sherehe mbalimbali kuna sare zinavaliwa hivyo haiwezi kuwa ajabu wao kuwa na vazi ama sare yao maalum inayowatambulisha.
Nawasilisha natumai ushauri huu utazingatiwa karibuni kwa mjadala.
Sent using Jamii Forums mobile app