Ushauri kwa Wizara ya Afya

Yuyo Ahumile Shamalendi

JF-Expert Member
Mar 10, 2018
993
782
Wana Jf habari, ngoja niende kwenye mada moja kwa moja

Kama kichwa husika hapo juu, nimeamua leo nitoe ushauri kwa Wizara yetu ya Afya kuhusu wataalamu wa maabara, naomba niseme hivi ili kuondoa mkanganyiko wa wagonjwa tunaomba Wizara yetu ya Afya ibadili utaratibu wa maabara na wataalamu wake.

Angalau maabara iwe na wataalamu wasiopungua watatu huku wakiwa kila mtu na vitendea kazi vyote vya maabara.

Kwani kumekua na usumbufu mkubwa kwa wagonjwa kupimwa na kukutwa hawana ugonjwa wakati huo mgonjwa yuko hoi, ila atakapoondoka na kwenda Hosipitali nyingine akipimwa anakutwa na ugonjwa kwa vile vile vitu walivyompima kwenye Hospitali ya kwanza, sasa hii tuseme ni ubovu wa vipimo au wataalamu?

Ndiyo maana nikasema wawepo wataalamu wasiopungua watatu na vitendea kazi kila mtu awe navyo ili kila mtu ajirishishe kwenye vyombo vyake kama ni kweli hamna ugonjwa.

Nawasilisha
 
Unaenda na mgonjwa wako hospitalin mnaxhukua vipimo pengine damu na mkojo, halafu majibu yanakuja hana ugonjwa, unapewa panadol za kushusha homa, mnaambiwa mrudi nyumbani wakati huo mgonjwa hawezi kutembea.

Mnaondoka huku mmehuzunika, mnaenda hospitali nyingine tena ndogo kabisa kuliko ile, wanachukua vipimo, majibu yanarudi amegundulika ana tatizo, kulingana na tatizo alilo nalo anatakiwa apigwe sindano za masaa, baada ya kumaliza dozi mgonjwa kapona! Sasa kwanini wasiwepo wataalamu wengi ili akishindwa kuchunguza mtaalamu wa kwanza wajaribu na wengine hapo hapo kwenye vyombo vyao kabla hamjaenda hospitali nyingine.
 
Back
Top Bottom