Ushauri kwa wenye vibanda vya biashara katika miji mbalimbali hapa nchini

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Kumekuwa na matukio ya kusikitisha ya kuungua kwa vibanda katika maeneo mbalimbali hapa nchini na kupelekea wamiliki kupata hasara kubwa na kuwaingiza katika umaskini mkubwa.

Binafsi nina ushauri kwa Serikali kama mamlaka na wenye vibanda husika.

(1) Serikali ihakikishe kuwa ni sharti kila mwenye kibanda anakata bima ya moto na siyo vinginevyo.

Bima ya kibanda chenye thamani ya Tshs.100,000,000 nina hakika haizidi Tshs.100,000.

Kwa utaratibu huu pakitokea kwa bahati mbaya ikatokea ajali ya moto basi wahusika watalipwa hasara waliyoipata kupitia bima walizoweka.

(2) Wafanyabiashara wapewe elimu juu ya majanga ya moto na wawe na semina maalum kuhusu athari ya moto.

Wapate elimu ya kuwa na bima ya moto.

(3) Mamlaka kama Halmashauri ihakikishe kuwa kila kibanda kinakuwa na chombo cha zima moto.

(4) Uongozi wa Masoko uhakikishe kuwa kila jioni matangazo yanapita kwa wenye vibanda kuhakikisha kuwa hakuna majiko ya moto au vifaa vya moto vinavyoachwa kwenye vibanda.
 
Sahihi kabisa.. Lakini pia ikumbukwe Hayo matukio ya mabanda kuungua moto mengi yanafanywa makusudi kabisa na sirikali kwa malengo fulani, aidha kupunguza mabanda kwenye miji au kuwalazimisha wenye vibanda(wamachinga) kuhamia kwenye eneo tengwa maalum.
Mfano mzuri SIDO Mbeya na ujenzi wa soko la mwanjelwa
 
Back
Top Bottom