Kwanza kabisa HERI YA MWAKA MPYA. Wadau wapenda elimu tunakupongeza sana kurudi Wizara ya Elimu baada ya kutolewa NECTA na Serikali ya awamu ya nne bila sisi kupenda. Nakushauri kwa yafuatayo:-
- Fumua mitaala ya elimu ili iendane na mazingia ya sasa.
- Rekebisha madaraja ya ufaulu kwa wanafunzi ili yaendane na ushindi wa kweli na siyo kuwafurahisha wanafunzi.
- Simamia vitabu vya elimu ya msingi na sekondari na usikubali vitabu vinavyochapishwa na wafanyabiahara(makajanja) kwa minajili ya kupata faida bila ubora wowote.
- Hakikisha walimu kweli wnafundisha tofauti na sasa. Wengi wa walimu ni wafanyabiashara. Ni walimu wachache ambao hawana boda boda. Tembelea Vjijini uone kwa macho yako.
- Hakikisha walimu wanapata stahili zao mfano :- Uhamisho, kupanda madaraja, likizo, matibabu n.k.
- Ufuatiliaji wa karibu kwa fedha zinazopelekwa mashuleni kwa ajili ya matumizi ya kila siku katika maeneo yao.
- Ufuatiliaji wa karibu uwepo kwa wakaguzi hasa wa shule za msingi na wapewe fedha za kutosha siyo kama Serikali ya awamu ya nne ambapo wastani kwa kila Halmashauri walipewa milioni nne kwa mwaka na huku kukiwa na ufujaji wa kutisha.