Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,021
- 2,478
Kwa mujibu wa mchakato wa utafiti wa kisayansi, bila kuchukua vipimo kwa ajili ya kuthibitisha usahihi wa rai (hypotehsis) kwamba Tanzania kuna UVIKO ni vigumu kukanusha usahihi wake.
Taifa lilifanya vizuri miaka ya 1980 pale janga la VVU na UKIMWI lilipozuka.
Tuliunda TUME YA TAIFA YA KUPAMBANA NA AIDS (TACAIDS).
Tuliunda tovuti ya TACAIDS na kukiri kwamba "Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoshambuliwa sana na janga la VVU na UKIMWI".
Tovuti hiyo hadi leo inatunza sera ya taifa kwa ajili ya kupambana na UKIMWI, Taarifa ya utafiti kuhusu madhara ya UKIMWI, na mfumo wa kimkakati kwa ajili ya kupambana na UKIMWI.
Nilifurahi sana Dkt. Gwajima alipojitangaza kuwa ni FIELD MARSHAL WA HEALTH SECTOR MANAGEMENT.
Basi, namwomba aonyeshe ufield marshal huo kwa vitendo kwa kuiga yaliyofanyika kwa ajili ya kupambana na UKIMWI.
Sasa alisaidie Taifa kuwa na Tume ya Taifa ya Kupambana na UVIKO (TACCOVID).
Kwa ajili hii aandike. Ministerial paper na kujenga hoja kifield marshal mbele ya mwenyekiti wa kikao cha Baraza la Mawaziri akianza presentation yake kwa kusema kuwa
"Kwa mujibu wa vipimo vya kisayansi kutoka maabara ya Taifa, Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoshambuliwa na UVIKO".
Naomba kuwasilisha hoja.
Karibuni Sumbawanga