Ushauri kwa Waziri wa Afya: Andaa na Kupeleka Waraka wa kuanzisha Tume ya Kupambana UVIKO katika Baraza la Mawaziri

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,477
Kwa mujibu wa mchakato wa utafiti wa kisayansi, bila kuchukua vipimo kwa ajili ya kuthibitisha usahihi wa rai (hypotehsis) kwamba Tanzania kuna UVIKO ni vigumu kukanusha usahihi wake.

Taifa lilifanya vizuri miaka ya 1980 pale janga la VVU na UKIMWI lilipozuka.

Tuliunda TUME YA TAIFA YA KUPAMBANA NA AIDS (TACAIDS).

Tuliunda tovuti ya TACAIDS na kukiri kwamba "Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoshambuliwa sana na janga la VVU na UKIMWI".

Tovuti hiyo hadi leo inatunza sera ya taifa kwa ajili ya kupambana na UKIMWI, Taarifa ya utafiti kuhusu madhara ya UKIMWI, na mfumo wa kimkakati kwa ajili ya kupambana na UKIMWI.

Nilifurahi sana Dkt. Gwajima alipojitangaza kuwa ni FIELD MARSHAL WA HEALTH SECTOR MANAGEMENT.

Basi, namwomba aonyeshe ufield marshal huo kwa vitendo kwa kuiga yaliyofanyika kwa ajili ya kupambana na UKIMWI.

Sasa alisaidie Taifa kuwa na Tume ya Taifa ya Kupambana na UVIKO (TACCOVID).

Kwa ajili hii aandike. Ministerial paper na kujenga hoja kifield marshal mbele ya mwenyekiti wa kikao cha Baraza la Mawaziri akianza presentation yake kwa kusema kuwa

"Kwa mujibu wa vipimo vya kisayansi kutoka maabara ya Taifa, Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoshambuliwa na UVIKO".

Naomba kuwasilisha hoja.

Karibuni Sumbawanga
 
Rais wa nchi ameshasema tumuegemee mwenyeziMungu maana hili tatizo hatuliwezi ..mbona siku hizi watu wabishi Sana kuelewa?
 
Changamoto za magonjwa kama vile malaria, UKIMWI, polio, kansa, kifua kikuu, nyumonia, na UVIKO ni tatizo pana la kiteolojia katika sura hasi.

Changamoto hizi zinaleta ushahidi mpya wa kuimarisha hoja ya kupinga uwepo wa Mungu ambaye ni all powerful, all knowing, all present, all loving (OMNIPOTENT, OMNISCIENT, OMNIPRESENT, and OMNIBENEVOLENT)

Naongelea hoja hii:

-- Kama Mungu angekuwa, OMNIPOTENT, OMNISCIENT, OMNIPRESENT, na OMNIBENEVOLENT, basi angezuia maovu ya kifizikia kama vile UVIKO na magonjwa mengine.

-- Mungu hazuii maovu ya kifizikia kama vile UVIKO na magonjwa mengine.

--;Kwa hiyo Mungu sio OMNIPOTENT, sio OMNISCIENT, sio OMNIPRESENT, sio OMNIBENEVOLENT, sio OMNITEMPORAL.

Hivyo, nasita kuunga mkono uamuzi wa serikali kutumia hoja ya kiteolojia kama sehemu ya mkakati wake wa kupambana na magonjwa.

In terms of subject juriadiction, a secular government, such as the one that obtains in Tanzania, is simply incopetent to counter this theological critique.

Lakini Dr. Gwajima anaweza kutekeleza ushauri huu:

"Fumbua kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu, uwatetee watu wote walioachwa peke yao. Fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki, uwapatie maskini na wahitaji haki yao” (Mith 31:8-9).

Katika kiwango hiki teolojia inaweza kuwa chachu kwa serikali kuchukua hatua za kisayansi, na sio kujielekeza vinginevyo.

NB:

Non-overlapping magisteria (NOMA) is the view that was advocated by Stephen Jay Gould that science and religion each represent different areas of inquiry, fact vs. values, so there is a difference between the "nets" over which they have "a legitimate magisterium, or domain of teaching authority", and the two domains do not overlap.

He suggests, with examples, that "NOMA enjoys strong and fully explicit support, even from the primary cultural stereotypes of hard-line traditionalism" and that it is "a sound position of general consensus, established by long struggle among people of goodwill in both magisteria."
 
Mama Amoni hii kitu imekuwa ngumu sana kuizuia sijuwi watatumia njia gani kuikabili?
Watu wametumia pesa nyingi sana kuokoa maisha yao dhidi ya covid ila wamedunda?
Nini kifanyike tujifungie ndani?
 
Tume tena!

Zille strategies za Ummy haiwezekani kuziendeleza?

Mnataka kuanzisha upya 'mchakato' badala ya kuendeleza pale alipoishia aliyepita!
 
Waziri wa afya huyo aliyegeuka futuhi kwa kunywa ushirikina mbele ya umma kuwa ndio tiba ya Covid? Waziri aliyeshikiwa akili anaweza kufanya hilo toka lini? Nyie covid-19 subirini mkirudi bungeni mwishoni mwa Machi mkapendekeze hii idea yako, kama kuna mtu anawasikiliza huko kwenye bunge kibogoyo.
 
Kwa mujibu wa mchakato wa utafiti wa kisayansi, bila kuchukua vipimo kwa ajili ya kuthibitisha usahihi wa rai (hypotehsis) kwamba Tanzania kuna UVIKO ni vigumu kukanusha usahihi wake.

Taifa lilifanya vizuri miaka ya 1980 pale janga la VVU na UKIMWI lilipozuka.

Tuliunda TUME YA TAIFA YA KUPAMBANA NA AIDS (TACAIDS).

Tuliunda tovuti ya TACAIDS na kukiri kwamba "Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoshambuliwa sana na janga la VVU na UKIMWI".

Tovuti hiyo hadi leo inatunza sera ya taifa kwa ajili ya kupambana na UKIMWI, Taarifa ya utafiti kuhusu madhara ya UKIMWI, na mfumo wa kimkakati kwa ajili ya kupambana na UKIMWI.

Nilifurahi sana Dkt. Gwajima alipojitangaza kuwa ni FIELD MARSHAL WA HEALTH SECTOR MANAGEMENT.

Basi, namwomba aonyeshe ufield marshal huo kwa vitendo kwa kuiga yaliyofanyika kwa ajili ya kupambana na UKIMWI.

Sasa alisaidie Taifa kuwa na Tume ya Taifa ya Kupambana na UVIKO (TACOVID).

Kwa ajili hii aandike. Ministerial paper na kujenga hoja kifield marshal mbele ya mwenyekiti wa kikao cha Baraza la Mawaziri akianza presentation yake kwa kusema kuwa

"Kwa mujibu wa vipimo vya kisayansi kutoka maabara ya Taifa, Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoshambuliwa na UVIKO".

Naomba kuwasilisha hoja.

Karibuni Sumbawanga
smartest opinion..... ntamfikishia muhusika
 
UVIKO ni kitu gani,Rais amesema mafua ya kubana wataalamu wanasema changamoto ya kupumua hiyo UVIKO umetoa wapi mama?.(sumbawanga hatuji ng'o).
 
Ameshafeli kabla hata hajaanza, ule mchanyiko alikua anaunywa mbele ya kamera kwa sisi walaji wa kitimoto tumekua tukiutumia miaka mingi sana kwa ajili ya kulainishia nyama yetu pendwa.

Mpaka sasa ukifanya ulinganifu wa jinsi alivyoshugulikia hili swala kati yake na waziri Ummy utaona amepigwa K.O.

Nje ya mada ; hapo sumbawanga unafanya shuguli gani mama Amoni.
 
Ni mwalimu shule ya SIMBAWANGA
 
Mama Amoni hii kitu imekuwa ngumu sana kuizuia sijuwi watatumia njia gani kuikabili?
Watu wametumia pesa nyingi sana kuokoa maisha yao dhidi ya covid ila wamedunda?
Nini kifanyike tujifungie ndani?

Rais amesema hii ni vita. So,

- tujue adui yuko upande gani

- tuchague grand military strategy (taayri: non-quarantine g/Strategy)

- tuchague strategies

- tuchague tactics

- tuchague methods.

NB:

-- kila mtu aheshimu subject jurisdictional boundary ya mwenzake.

-- tutashinda vita kwani sasa tunajua casualties ni 3.5% ya waathirika. Nasi tuko 60 milioni.
 
Kwa mujibu wa mchakato wa utafiti wa kisayansi, bila kuchukua vipimo kwa ajili ya kuthibitisha usahihi wa rai (hypotehsis) kwamba Tanzania kuna UVIKO ni vigumu kukanusha usahihi wake.

Taifa lilifanya vizuri miaka ya 1980 pale janga la VVU na UKIMWI lilipozuka.

Tuliunda TUME YA TAIFA YA KUPAMBANA NA AIDS (TACAIDS).

Tuliunda tovuti ya TACAIDS na kukiri kwamba "Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoshambuliwa sana na janga la VVU na UKIMWI".

Tovuti hiyo hadi leo inatunza sera ya taifa kwa ajili ya kupambana na UKIMWI, Taarifa ya utafiti kuhusu madhara ya UKIMWI, na mfumo wa kimkakati kwa ajili ya kupambana na UKIMWI.

Nilifurahi sana Dkt. Gwajima alipojitangaza kuwa ni FIELD MARSHAL WA HEALTH SECTOR MANAGEMENT.

Basi, namwomba aonyeshe ufield marshal huo kwa vitendo kwa kuiga yaliyofanyika kwa ajili ya kupambana na UKIMWI.

Sasa alisaidie Taifa kuwa na Tume ya Taifa ya Kupambana na UVIKO (TACCOVID).

Kwa ajili hii aandike. Ministerial paper na kujenga hoja kifield marshal mbele ya mwenyekiti wa kikao cha Baraza la Mawaziri akianza presentation yake kwa kusema kuwa

"Kwa mujibu wa vipimo vya kisayansi kutoka maabara ya Taifa, Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoshambuliwa na UVIKO".

Naomba kuwasilisha hoja.

Karibuni Sumbawanga
Kwa imani tuliyojengewa na walio serikalini na zaidi huko afya kwenyewe hilo laweza kufanyika ila sioni dalili leo wala kesho labda kwa shinikizo.
 
Ni mwalimu shule ya SIMBAWANGA
I missed you miserably. Bali nimeshtuka sana. Na si siku nyingi kulikuwa na habari humuhumu jf kwamba kuna mwalimu ana phd na anafundisha shule ya msingi. Alianza kazi ya ualimu kwa kiwango cha cheti. Akajiendeleza hadi kufikia phd. Ruhusu ya kwenda kwenye hayo masomo yake alikuwa akipata kutoka kwa huyo mwajiri wake. Bado yupo shule ya msingi na akilipwa mshahara wa mwalimu wa cheti.
Ulipojibu swali la unafanya nini Sumbawanga, kidogo nizimie. Bado sijawa sawa kwa kuhisi isije ikiwa wewe ndiye. Nitatulia nikijua ni shule gani hiyo yenye bahati ya kuwa na mwalimu wa tafakuri tunduizi! Shule zenyewe hizi za bongo flava? Mwalimu mwenyewe kama wewe? Jinamizi wallah!
 
Kuna Miaka mitatu ya kutosha tangu hili janga liikumbe dunia.., kuliko kuanzisha waraka, Tume n.k. za kupiga hizi kodi zetu ni bora tu tukaungana na mataifa yote ya dunia nzima tukachangia nguvu zetu kwa pamoja... Jungu Kuu halikosi Ukoko, Tatizo la Dunia litatatuliwa Kidunia
 
Back
Top Bottom