Ushauri kwa wauzaji wa maduka ya bidhaa mbalimbali muhimu kipindi hiki cha mlipuko wa #COVID19

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
Wakati dunia nzima ikiendelea kupambana na ugonjwa huu, maduka ya bidhaa mbalimbali yameendelea kuwa wazi ili wananchi wapate mahitaji ya muhimu

Zingatia kanuni zifuatazo ili kuhakikisha usalama wako kama muuzaji au usalama wa wafanyakazi wako kama mmiliki wa biashara

1. Hamasisha huduma ya “delivery” kwa kupitia mtandao. Hivi sasa mtandao umerahisisha mawasiliano na hivyo kwa wafanyabiashara wenye uwezo, hii ni njia salama zaidi ambayo itapunguza kiwango cha uchangamano wa muuzaji na wanunuzi

2. Zingatia umbali kati ya muuzaji na mnunuzi. Suala la umbali ni gumu kuzingatia hususani kwa mazingira ya maduka mengi ya Tanzania hivyo barakoa na gloves zivaliwe muda wote kuzuia unyevu kutoka wala kuingia

3. Weka maji tiririka na sabuni na sanitizer katika eneo la nje ya biashara yako na uhamasishe matumizi yake ili kujilinda endapo kutakuwa na mgusano kati ya mnunuzi na muuzaji

4. Epuka kushika maeneo ya usoni. Ingawa barakoa hufunika mdomo na pua, virusi vinaweza kuhama kutoka kwenye pesa na kuhamia mikononi kisha kuingia kupitia machoni endapo muuzaji atagusa maeneo hayo

5. Tumia hand sanitizer kila baada ya kupokea kitu chochote kutoka mtu mwingine. Pesa ziwekwe kwenye chombo kimoja na mwisho wa siku zihifadhiwe kwa namna ambayo haitoruhusu kusambaa kwa maambukizi

#JFCOVID19_Updates #CoronaVirus
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom