Ushauri kwa wasomi wenzangu na hasa mliopo vyuoni na matumizi mazuri hili jukwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri kwa wasomi wenzangu na hasa mliopo vyuoni na matumizi mazuri hili jukwa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Maganga Mkweli, Oct 26, 2011.

 1. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Wengi wenu humu ni wageni na wengi wenu mnaonekana either mpo chuo au ndio mmeingia chuo sasa mimi ni mambo machache nataka kushare na nyinyi ndugu zangu
  1. ushindani wa chuo unachosoma
  2. upataji wa habari hasa za vyuo
  3. umuhimu wa wewe kama msomi na ndani ya jamii ya inayokuzunguka
  4. uchaguzi wa kozi unayosoma na wigo wa ajira
  5. maisha ya chuo na changamoto zake


  ushindani wa chuo unachosoma

  nimekuwa nilifuatilia recently maada nyingi ni za majivuno ya chuo unachosoma mara ulinganishaji wa kozi hii chuo hichi na chuo hichi jambo la msingi na la muhimu kwako wewe msomi ni kujitambua kumbuka elimu dhumuni lake kubwa ni kukomboa kifikra na kukusaidia kupambana na changamoto nyingi za maisha ya kila siku na si kushindana kwa minajiri ya kuwa wa kwanza (ingawa hii inakupa motivation ya kusoma) au chuo fulani bora ya kingine so what alaaah ? Jitambue kama msomi wewe

  upataji wa habari hasa za vyuo


  tatizo jingine ambalo nimeliona ni jinsi ambavyo wanajamii wengi hasa ndani ya hili jukwa wanavyokuwa na watafuta habari za chuo anachosoma kwa wale wa mwaka wa kwanza vyuoni siwezi walaumu sana ila ningependa kuwapa maangalizo yafuatayo chuo ni institute kubwa sana kwa hiyo upatikanaji wake wa habari hasa za ndani masuala ya test ,mikopo ,ada na mambo mengine ya kiutawala huwa yana patikana kwenye notisi board hasa za department husika au college husika kutokana na ukubwa wa chuo pia kwa sasa vyuo vingi vina tovuti zake hivyo basi jitahidini kutumia mitandao kupata habari za vyuo vyenu .missinformation chuo ina madhara mengi sana na hili naomba mlitilie maanani..(watu wengi wadiscontinue sana kwa missinformation)

  umuhimu wa wewe kama msomi katika jamii

  hili ni jambo la msingi sana naona vijana wengi siku hizi atuelewi kabisa dhima ya elimu jitahidi kustaarabika kimawazo ili tofauti yako na mtu ambaye ajaenda shule ambaye anahitaji msaada wako aweze upata .wewe kama msomi ni chombo muhimu sana kwenye jamii inayokuzunguka hivyo basi jitambue …(FIKRA CHANYA)

  uchaguzi wa kozi unayosoma NA wigo wa ajira

  hii ndio changamoto kubwa sana hasa kwa wale ambao huwa wako mwaka wa mwisho vyuoni au ndio wamemaliza hili ni tatizo kubwa sana hasa kwa nchi yetu hii yenye wasomi wachache sasa tulio wengi tunaenda kozi fulani ama kwa mkumbo ama kwa kutojua kutokana ufinyu wa habari za kozi husika hili nalo ni tatizo kubwa sana . Hapa natoa rai kwa wasomi wa nyanja zote waweze kuwaelimisha wadogo zetu hasa wale walio masekondari na vyuo vya ufundi kuhusu uchaguzi kozi hasa anapokuja kuomba ushauri jaribu kuwa muwazi mueleze experience yako na hiyo kozi na wigo wake wa ajira kwa ujumla na manufaa yake …haiingii akili unakuta watu 20 wanatoka shule moja eti wote mfano wanataka kusoma sheria,bcom,telecom nk..

  maisha ya chuo na changamoto zake

  mliopo na mliopita chuo mnajua changamoto zinazoikabili elimu yakitanzania na wasomi wake hapa nafiriki watu wengi wanaweza kuwasilisha michango yENU.............
  nawatakia masomo mema ili tuje tukomboe taifa letu ambalo bado sana liko gizani kifkra
  tumieni hili jukwa kwa manufaa sio majingambo na tambo zisizo na maana..
  jiulize haya maswali ya msingi
  mimi kama msomi nafasi yangu katika jamii nini?
  Kwanini nasoma hii kozi ?

  Hosea 4: 6 (KJV) My people perish from a lack of knowledge.

  Nawasilisha
   
 2. Nyaluhusa87

  Nyaluhusa87 JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 1,288
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Asante sana mkuu kwa ku2elimisha.
   
 3. m

  micro_almunia Senior Member

  #3
  Oct 26, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hoja bora!
   
 4. TWALICIOUS

  TWALICIOUS Member

  #4
  Oct 27, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  100 ya 100
   
 5. CR wa PROB

  CR wa PROB Senior Member

  #5
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kazi nzuri sana!!!! sema mambo mengine yanayoulizwa yapo nje ya uwezo wanajamvi kwani yapo kiutawala zaidi.
   
 6. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  wewe kichwa mkuu!
   
 7. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #7
  Oct 28, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Hua ni faraja saana ukiona Thread hasa ambayo inahusu wasomi na iko accurate.
   
 8. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  mpendwa inabidi tusaidiane maana humu jamvini tupo watu wa namna tofauti .
  Unaweza wapa na wewe maunjanja mengine wanajamii hasa wasomi waliopo vyuoni...
  Wanasema sharing is caring..
   
 9. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #9
  Oct 28, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Huo muongozo uliotoa ume-cover yalo ya msingi... ni mengi na ni first step, inasikitisha tu kua ajabu ni kwamba ni walengwa wachache wataona... na wataoona ni wachache watasoma... na watao soma ni wachache watazingatia. BUT hata kama watapatikana kumi wataozingatia katika jopo la watu woote hawa then sio mbaya....
   
 10. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  unenena vyema mpendwa ,wanasema sote ni ndugu .
  jambo la msingi tu ni msomi mwenyewe kujitambua na kuzingatia kanuni .
  kama msomi huoni thamani yako kati watu million 40+ wakati kwa makadirio watu wenye degree tu hapa tanzania hawafiki laki mbili...
  na thamani yako nini basi? ni kumbananua mambo kwa upeo na kuweza kuzikabili changamoto (wanaita fikra chanya)...
  NATUMAINI WACHACHE WATAOPITA HAPA WATAFIKISHA HUU UJUMBE KWA WENGINE
  NAWASILISHA..
   
 11. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Very good! That's nice for JF health
   
 12. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #12
  Oct 28, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180


  Maganga wanaojiuliza hayo maswali/maswala ya msingi ni wachache mpaka waweza pasuka kwa hasira!! Tatizo elimu yetu ni ya kukariri mno sio ya kuisomea katika vitabu; Kwamba msomi atasoma the related topic kwa vitabu mbali mbali akitumia wasomi mbali mbali na schools of thoughts mbali mbali.... Haipo. Kazi kukalili madesa tu, hio inafanya wasomi walo wasomi wawe kwa uchache saana. Tunabaki na watu wengi wenye shahada za chuo lakini ambao sio wasomi.... Sad.
   
 13. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  hii ni changamoto mpendwa mfumo wa elimu yetu ya kitanzania una changamoto nyingi mojawapo ni hii ya ukariri (madesa orientanted ) baadala ya kutumia vitabu nakumbuka wakati naingia mlimani mwaka wa kwanza wakati tunapitishwa orientation LIBRARY nikasikia wajamaa zangu hasa wa uhandisini(FOE/coet) huko ni kwa mangwini (social science na bcom) wakati kunareserve ya vitabu kwa ajili ya engineers ( wanaita science collection unapata useful materials) haya sasa na hao ngwini ambao si engineer tulisema library ni kwa ajili yao nao nowdays huko library imekuwa sehemu ya kutongozana na kuonyeshana style za mavazi
  mfumo wa elimu yetu ya kitanzania unahitajika kufumuliwa sana ili kuokoa kizazi hichi. kumbuka elimu ya juu ina dhana pana sio kuwa na first class isiyokuwa na mchango wowote kwenye society
  "...intellectuals have a special contribution to make to the development of our nation, and to Africa. And I am asking that their knowledge, and the greater understanding that they should possess, should be used for the benefit of the society of which we are all members." -Julius Kambarage Nyerere, from his book Uhuru na Maendeleo (Freedom and Development), 1973.
   
 14. o

  ommy15 Senior Member

  #14
  Oct 28, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Mganga waukweli,kwanza nashukuru kwakua open na mpenda mabadiliko. kwakweli kama kuna jukwaa kwenye hii jf linalo kera basi ni hili la elimu,kwani wengi wawadau ni kama hatujitambui kwani mada na michango ya huku haireflect uhalisia wa wahusika yaani wanafunzi/wasomi ambao ndo wadau wakubwa. so naomba tujaribu kuangalia mada zetu na michango kama mtu huna mchango soma tu pita sio lazima kuchangia.
   
 15. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  ni kweli mkuu kuellimishana muhimu naamini tutaelewana tu na watu wajua majukumu yao............
   
 16. d

  dy/dx JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 622
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  asante sana kwa mchango wako bora sana,nitajitahidi kuufatilia vyema.Be blessed mkuu.
   
 17. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  pamoja sana mkuu, ubarikiwe na wewe pia tukomboe nchi yetu..
   
 18. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #18
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  again please spare your time soma hii thread hasa kwako wewe mgeni hili jukwa na kwa wale wadogo na ndugu zangu mnao tarajia kwenda mavyuoni mwaka huu..
  kumbukeni kuuliza si ujinga ..ila jitahidi kutafuta habari
  mshukuru mungu kwa kila jambo usijalaumu sana kama utakosa kozi fulani maana wakati unajaza hiyo kozi uliyopata huku ijaza kmakosa na kama ulijaza kimakosa usiogope utasahihisha makosa cha muhimu na cha msingi jitahidi kuwa mwepesi kupata UPDATE za kozi yako kwenye ulimwengu wa sasa na fursa zilizizopo..
   
 19. Timoso

  Timoso Senior Member

  #19
  Aug 13, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 142
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Darasa tosha
   
 20. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2012
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  take your time soma hii kitu hope utapata kitu hasa kwa WALE MNAOINGIA VYUONI..
   
Loading...