Ushauri kwa Washauri wa Rais ili Wakamshauri Rais wetu kuhusu Maendeleo ya Taifa letu Tanzania

S.N.Jilala

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
540
507
Ushauri kwa Washauri wa Rais ili Wakamshauri Rais wetu kuhusu Maendeleo ya Taifa letu Tanzania.

Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ndiyo roho au injini imara kabisa walizotumia/wanazozitumia nchi za Ulaya, Marekani, China, Urusi na nchi zote zilizoendelea katika maendeleo yao.

Katika sayansi, tunajifunza vitu vya asili na visivyo vya asili. Hapa ili nieleweke nitaongelea vitu vya asili katika kumanisha nini maana ya sayansi. Sayansi hapa naongelea vitu vilivyopo katika Dunia hii hasa vya asili. Kwa mfano, sayansi ya Wanyama na Mimea. Kwa hiyo, sayansi ni maisha ya vitu au ni vitu vilivyo, asili yake na vinavyoishi kiasili.

Tunaweza kuwa na sayansi ya udongo, binadamu n.k. Kwa hiyo, kama Taifa kama tunataka maendeleo lazima tuwekeze kwa asilimia kubwa katika sayansi ya asili.

Teknolojia yenyewe ni mchanganyiko wa mbinu, ujuzi, maarifa, njia na michakato mbalimbali inayotumika katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali na utoaji wa huduma mbalimbali. Tukiongelea teknolojia tunaongelea mambo ambayo mwanadamu anaweza kuyatengeneza katika Dunia hii.

Kwa mfano, unaweza kutengeneza teknolojia ambayo itarahisisha wanyama wetu kuishi maisha mazuri na yenye furaha porini. Na teknolojia hii inaweza ikawa katika muktadha wa kuwapatia Maji kama kuna ukame zaidi, malisho pia au kuwapatia dawa za kujikinga na madawa.

Tukiongelea kuhusu viwanda tunaongelea teknolojia katika nyanja kama NNE hivi;

1. Teknolojia ya kutengeneza vyuma. Huwezi kuwa na viwanda bila kuwa na vyuma vya kuzitengeneza machine.

2. Teknolojia ya kutengeneza kemikali. Huwezi kuwa na machine ambayo inafanya kazi bila kuunganishwa kemikali.

3. Teknolojia ya Injinia. Huwezi kutengeneza kwa mfano, daraja, kiwanda na mambo mengi ya ujenzi bila kuwa na teknolojia ya injinia.

4. Pia, ili hayo mambo yaende tunahitaji Viongozi wenye maono hayo na wakayaweka katika uhalisia.

Na Ubunifu ni nini?

Ni kitendo au mchakato wa kubadirisha mawazo uliyo nayo, bidhaa iliyopo kwa sasa katika vitendo zaidi hasa wa kuifanya bidhaa hiyo ionekane au iwe ya thamani zaidi ukilingaisha na awali.

Ili mambo yako yaende vizuri kuanzia kwenye familia, kazini, na mambo yote ya Kitaifa ni vyema kusisitiza katika ubunifu zaidi na zaidi.

Mwana Uchumi Robert Solows Mwanauchumi mashuhuri ambaye alikuja kupewa Nobel Prize alinena kuwa 15% tu ya uchumi wa Marekani kuanzia 1870-1950 umetokana na Marekani kuwekeza katika nguvu kazi na kuwa na mitaji. Na teknolojia katika ubunifu ilichangia kwa 85%.

Nesta UK Kingdom Innovation nao wakafanya utafiti 2000-2008 na kuja kuhitumisha kuwa 63% ya uchumi wa UK umechangiwa na teknolojia katika ubunifu wa mambo na 37% inatoka katika kuwekeza katika kuandaa rasilimali watu na kuwa na mitaji ya kuwekeza.

China hii ya Leo yenye maendeleo ya juu kabisa kiuchumi ni zao la Sayansi, teknoloji na Ubunifu. Urusi inayotamba katika kuwa na jeshi la kisasa zaidi ukiacha Marekani zao la kukumbatia sayansi, teknolojia na ubunifu. Nchi yenye uchumi imara Duniani na jeshi imara katika kuwa na vifaa vya kisasa yaani Marekani ni zao la kukumbatia sayansi, teknolojia na ubunifu.

Kwa hiyo hata mkiwa na Mali asili nyingi kiasi gani kama Taifa, kama hamjawekeza muda, akili, ujuzi na maarifa kwenye sayansi, teknolojia na ubunifu safari ya maendeleo tunayoitaka ni ndefu.

Kwa hiyo basi, kama Taifa tuna wajibu mkubwa kujikita katika Tafiti ambazo zina uwezo wa kubadirisha mawazo hayo kuwa bidhaa, huduma na namna ya kufanya vitu tofauti zaidi na zaidi na hii ndiyo siri kubwa wanazotumia nchi zilizoendelea.

Simon Ngusa Jilala
04/04/2017
 
Back
Top Bottom