Ushauri kwa wanaopanga safari/ wanaosafiri kati ya Arusha-Dar

MAKOLE

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
617
500
Kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha, kumekuwa na mkwamo wa safari haswa kuanzia Korogwe Mjini ambapo leo 26/10/2019 barabara hiyo imefungwa na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wanaosafirisha huduma, bidhaa na watu.

Hii ni kutokana na kipande cha barabara ya Segera-Korogwe kuwa na maeneo matatu yaliyojaa maji ambayo ni Daraja la Kilole (Korogwe Mjini), Daraja la Mto Mnyuzi (Mpaka wa Korogwe na Handeni kwa njia kuu ya Arusha-Dar) na daraja la Mandera.

Vilevile, njia ya Korogwe-Handeni-Mkata nayo imefungwa kutokana na kujaa maji na kusombwa kwa daraja. Aidha, njia ya mkato ya kuzungukia Korogwe-Mnyuzi/Muheza- Tanga au Korogwe- Mnyuzi-Segera-Chalinze nayo imejaa maji kwa baadhi ya maeneo.

USHAURI:
  1. kama huna safari ya lazima sana kwa siku mbili hizi basi unaweza kuahirisha safari kuepuka usumbufu.
  2. Kama una safari ya lazima unaweza kupitia barabara ya Arusha - Dodoma ambayo huenda kwa wakati huu ipo salama.
  3. Safiri na fedha ya kutosha kwani kwa kipindi hiki bei za huduma na bidhaa zimepanda kwa baadhi ya wafanyabiashara.
  4. Kabla ya kuanza safari ni vyema kuwasiliana na viongozi wa usalama barabarani mkoa wa Tanga ama Wilaya ya Korogwe kwa ajili ya kupata uhakika wa safari (ingawa maji hayana muamana maana yanaweza kujaa katika eneo fulani in 30 minutes time pakawa hapapitiki)
  5. Kwa nia njema, unaweza kuwasiliana kwa nambari ya POLICE KOROGWE ambayo ni 0652449324, ili kuweza kuulizia hali ya usalama barabarani.

ALLAH ATULINDE KWA SAFARI ZETU!
 

Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
7,002
2,000
Labda na sisi wa huko watatufikiria ingawapo madaraja, bila mikasa kama hii nani atatukumbuka?
 

MTOCHORO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
4,033
2,000
Kuna watu walitarajia Kuzika leo hadi sasa mwili haujawasili, kuna waliokuwa wasafirishe miiili leo wote wamekwama
 

Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
12,561
2,000
Nakumbuka pale Dakawa Mto Mkondoa ulikata Daraja Waziri wa Ujenzi alienda kulala (kufanya kazi usiku mchana) likakamilika.
  • ile barabara ilikuwa muhimu kwa Nchi kukatiza kwenda Dom-Tbr-Mwz Burundi Rwanda? kuliko hii ya Milimani mpaka Kenya
  • Hakuna Waziri wa Ujenzi mwenye weledi km yule
  • Mkoa wa Tanga TANROAD sio weledi km Morogoro?
sijui mvua za mwaka huu hazitabiriki Mvua za milima ya Ukaguru bado msimu
hebu wapitie Dodoma Babati warudi Arusha Moshi Same
 

Halaiser

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
2,752
2,000
Halafu TANROAD/ TARURA wapo kimyaaaa kana kwamba hamna tatizo
Wote wako kwenye mapokezi ya ndege mpya. Haya mengine sio vipaumbele vyao.
Si unajua majina lazima yaitwe na mkuu pale uwanjani. Usipoonekana pale kibarua kinaweza ota nyasi.

Jiulize kwanini hakukuripotiwa na chombo chochote cha habari toka jana tukio lile la abiria toka Ars, Msh to Dar kukwama na kulazimika kulala pale Korogwe?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom