Ushauri kwa waliooa tu: Mke wangu anavaa nguo zilizochakaa

nditolo

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
3,718
4,256
Mke wangu nguo anazo nyingi tu lakini hazivai. Yeye anavaa nguo zilizo chakaa tu. Mpaka anakosa mvuto. Ananifanya nichepuke sana. Ukimwambia ni mbishi mno.
 
Nguo zake halafu zinakufanya uchepuke?? Ha ha ha bro hapo utakua unaihalalisha tabia yako mbaya kwa kumsingizia mkeo.. Source ya chochote ni muhusika mwenyewe.. We unatabia hizo toka zaman so umezoea kuona michepuko yako inayokuchuna inaenda kununua nguo tu inapendeza unataka na mkeo awe kama wao,,hakuma kitu kibaya kama kumfananisha mkeo na michepuko yako,,maana unajenga fikra hizo na leo unaona hafai.. Na mbaya unaona dawa ni kuchepuka.. Kama unampenda akiwa hata uchi ni mvuto gani unaoutaka zaid??
 
Make wangu nguo anazo nyingi tu lkn hazivai. Yeye anavaa nguo zilizo chakaa tu. Mpk anakosa mvuto. Ananifanya nichepuke sana. Ukimwambia no mbishi mno.
Hivi.......
Kama wewe unajiita mwanaume, na ukashindwa ku handle mambo madogo kama haya, hadi uanzishe Uzi...
Je siku ukikutana na majanga kama yangu, sindio utaita press kabisa..
 
Make wangu nguo anazo nyingi tu lkn hazivai. Yeye anavaa nguo zilizo chakaa tu. Mpk anakosa mvuto. Ananifanya nichepuke sana. Ukimwambia no mbishi mno.

Mnunulie nyingine mpya za kumtosha..na nzuri

halafu baki njia kuu..nguo tu unachepuka! Akiugua si ndio utamfukuza kabisa
 
Hivi.......
Kama wewe unajiita mwanaume, na ukashindwa ku handle mambo madogo kama haya, hadi uanzishe Uzi...
Je siku ukikutana na majanga kama yangu, sindio utaita press kabisa..
Stooop!! hebu ngoja kwanza, tupe angalau kiduchu hayo majanga yako ili tujue tunamtukana vipi huyu dogo.
 
Make wangu nguo anazo nyingi tu lkn hazivai. Yeye anavaa nguo zilizo chakaa tu. Mpk anakosa mvuto. Ananifanya nichepuke sana. Ukimwambia no mbishi mno.

Yawezekana mna mitizamo tofauti, yeye anapenda kuvaa magauni marefu, wewe unataka avae mafupi, SWALA LA KWAMBA ANAVAA nguo zilizochanika si la kweli, na kama ni kweli, basi akaombewe ana mapepo. Kuna nguo ambazo mke wangu akivaa mi nafurahi, ila yeye anaona hazipendi, sasa inakuja swala la priority, ANAVAA KUMFURAHISHA NANI? LABDA KUNA WATU WA NJE anaowapendeza akivaa hivyo, AND WAO NDO KIPAUMBELE CHAKE ... USINGOJE USHAURI, ANGALIA STATUS AND ACT ....
 
Kuchepuka ulishazoea kabla hujaingia ndani ya ndoa, kuto kuvaa vizuri sio sababu ya kuchepuka ingawaje haipendezi kuvaa ovyo...
 
Msifie urembo wake,mwambie unachokipenda,mathalan akivaa nguo ya aina fulani inamtoa na dawa kubwa ya ndoa ni kufunguliana mioyo, na sumu kubwa ya ndoa ni michepuko,japo sometimes unajikuta umetumbukiamo labda safarini umekaa wiki....zidisheni "pillow talk" kuambiana,sio unakuta mmepiga mzungu wa4 halafu utegemee ndoa iendelee.
 
Make wangu nguo anazo nyingi tu lkn hazivai. Yeye anavaa nguo zilizo chakaa tu. Mpk anakosa mvuto. Ananifanya nichepuke sana. Ukimwambia no mbishi mno.
Mke ni SAWA na mwanafunzi,usichoke kumfundisha, lakini usimfundishe kwa hasira,kwa kuwa ni mke wako, naamini unamjua vilivyo,siku ukitambua ni mwenye furaha hiyo ndio nafasi nzuri ya kumuelekeza hilo, ukitambua hana mood nzuri muache.

Kuchepuka ;
hilo ni tatizo lako kaka
 
Make wangu nguo anazo nyingi tu lkn hazivai. Yeye anavaa nguo zilizo chakaa tu. Mpk anakosa mvuto. Ananifanya nichepuke sana. Ukimwambia no mbishi mno.
Muwe munaangalia na wake wa kuoa. Ukimkuta, ukioa mke aliefundishwa umuhimu wa kuishi na mme, wewe mwenyewe utamkubali anavyo jipenda, kukupenda. Na kukutimizia kila unalomuambia.
 
Back
Top Bottom