SoC01 Ushauri kwa waliomaliza Kidato cha Sita na hawakufaulu kuendelea na Elimu ya Juu

Stories of Change - 2021 Competition
Jul 14, 2021
5
13
Kijana ambae umemaliza KIDATO Cha sita na hukufaulu kujiunga na elimu ya juu yaani chuo kikuu kutokana na kutokufikisha alama sitahiki kwa ajili ya kujiunga chuo kikuu zingatia haya yafuatayo

1.Jipe moyo mkuu na usikate tamaa kwa kuwa na mtazamo hasi kuwa bila shule hakuna maisha anza kufikilia njia ya pili ya kupambana na kufikia malengo yako hata hao ambao wanaenda chuo wakimaliza wote mtakutana mtaani mkipamban na mishe za hapa na pale kutafuta ajira au kufanya kazi mbalimbali hivyo unatakiwa kutumia elimu ulioipata japo kuwa hukufaulu. Buni njia sahihi ya wewe kuingiza kipato ili uje uajiri wenye degree

2.Kama una Nia na moyo wa kusoma au unaamini katika elimu rudia shule yaani Kidato Cha sita na ufanye Tena mtihani au uende vyuo vya diploma na baadae usome degree sawa nawengine ni suala la muda tu lakini kama unamalengo na elimu mda sio kitu unaweza kusoma na ukatimiza ndoto zako kupitia elimu kama unavyo amini

3.Lakini pia kwa wewe kijana mwenzangu ambae hukufaulu kwenda chuo kikuu unaweza kwenda veta na kupata mafunzo ya mda mfupi au mda mrefu na ukaanza kuutumia ujuzi ulioupata veta KUTENGEZA kipato kuliko kufa moyo na kukaa nyumbani au mitaani.

Unaweza kujifunza ufundi magari,umeme,mwashi,seremala au uchomeleaji vyuma na ukajiajili mwenyewe na watakao maliza chuo watakukuta unaajira wakati wao wakihangaika na soko la ajira hivyo unaweza kuwaajili katik ofsi yako mfano wewe ukienda chuo mwaka mmoja na ukajifunza KUTENGEZA magari au umeme na ukapambana miaka mitatu katika kazi hiyo kijana aliechuo kikuu akimaliza atakukuta mbali Sana hivyo usikate tamaa

4.Epuka makundi ya vijanaa wasiofaa au wasio na USHAURI chanya kwako ukimaliza Kidato Cha sita hata Kama hukufaulu tayari una maalifa yakufanya Mambo makubwa. Makundi yasiyofaa yatakudidimiza kwa kukupa USHAURI mbaya Kama kuiba au kukaba kwa vijana wa kiume au kufanyaa ukahaba kwa vijana wa kike hivyo epuka kuwa na marafiki ambao watatumia udhaifu wako wa kufeli shule kukushauri Mambo yasiyofaa ili upoteee hivyo kuwa makini na watu wa Aina hiyo kaa nao mbali wewe jipe moyo kuwa huenda shule haikua sehemu sahihi ya wewe Kutimiza ndoto zako tazama upande wa pili wa kujiajiri pamoja na frusa zilizo mbele yako

5.Usikubali kukaa bila kazi nyumbani ukisubiri ugali wa baba na mama hangaisha kichwa na akili ni vipi unaweza kujirisha na kuwasaidia wazazi wako wako . Kumbuka kuwa unapokaa nyumbani unawapa watu maneno ya kusema mala oooh alijiona anaakili na mengine mengi wewe chapa kazi usisikilize maneno ya watu kwani mitihani shuleni inapima akili ya darasani na sio ujuzi na maalifa ya kazi umiza kichwa unaweza kufanya kitu gani ili watakao maliza shahada zao wakukute pengine na ukiwa mtu mwingine

Kijana mwenzangu ambaye hukufaulu, huu sio muda wa wewe kunung'unika ni muda wa wewe kupambana na frasa zilizopo mbele yako na kuamini katika upande wa pili kutimiza ndoto zako ambao sio shule Wala elimu pambana,jipe moyo,usikate tamaa na mtengemee mungu
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom