Story of Change Ushauri kwa waliomaliza Kidato cha 6 (baada ya matokeo): Nini cha kusomea Chuo Kikuu Kupambana na Soko la Ajira

Khadija Mtalame

Senior Member
Jul 14, 2021
124
500
Habari wanajukwaa;

Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa kunipa afya na wakati mwema Kama huu,ili niweze kutoa upako wa kweli kuhusu hatma ya wanafunzi waliomaliza KIDATO cha 6 kuhusu nini cha kusomea baada ya Necta kutangaza matokeo yao.

Pili na mwisho katika utambulisho,hongereni sana vijana wote mliofanikiwa kufaulu mtihani huo na kufanikiwa kutimiza ndoto zenu.

Mambo yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa katika kuelekea kuchagua masomo ya chuo kikuu,

MOJA,

Vijana wote wanaotaka kufanya maombi ya chuo kikuu wanatakiwa kuhakikisha kwamba WANAISHI NDOTO ZAO, kutokana na kuwepo kwa shida ya ajira ambapo kumekuwa na wahitimu wengi ambao wameshindwa kujiajiri na kuajirika kutokana na namna elimu walivyopata.

Mwanafunzi au mtu yoyote anaetaka kufanya chaguzi ya fani ya kusomea chuo kikuu anatakiwa kwanza kujipima na kuangalia Nini anapenda maishani mwake? Na sio akasomee kitu gani chenye ajira. Mfano, unaweza kukuta kipaumbele Cha serikali ya JMT Ni afya na ualimu sayansi na ukaamua kwenda kusoma katika kada hizo,lakini mwisho wa siku ukamaliza na ukasubiriwa kuajiriwa na endapo hutaajiriwa elimu yako itapotea pia utakuwa umepoteza ndoto zako.

Lakini, endapo mtu ukaamua kusoma kitu unachokipenda moyoni mfano, endapo unapenda kuwa fundi mshonaji wa nguo tangu ukiwa mdogo,Ni lazima uhakikishe kwamba unachagua masomo ambayo ukienda kusoma darasani utakuwa na amani ya moyo na utayapenda sana ,ambapo mwisho wa siku utaelewa na hautakuwa mzigo mtaani Mara utakapomaliza masomo yako.

Hivyo,nawashauri sana vijana muombe vitu ambavyo mnavipenda kutoka moyoni na sio vitu ambayo unahisi au umeshauriwa vina ajira endapo utamaliza,siku hizi hakuna kitu utasoma kitakupa ajira moja kwa moja, hata aliesomea Udaktari anaweza kumaliza na asiajiriwe lakini endapo utasoma Udaktari kwa kupenda hata usipoajiriwa utaweza kujiajiri mwenyewe.

Hivyo napenda kuwaasa, vijana na watanzania wote kwamba ILI TUWEZE KUPAMBANA NA AJIRA KWA WAHITIMU WA VYUO VIKUU,tafadhali tuhakikishe kwamba tuwaambie vijana wetu wakasome vitu wanavyovipenda na sio kitu ambacho anahisi ataweza kuajiriwa endapo akimaliza masomo yake.

PILI, ni ndoto ya kila mwanafunzi anaposoma anakuwa amedhamiria kuwa nani na kwasababu gani. Kwa kuzingatia hilo nipende kuwaambia vijana waliomaliza kidato Cha sita elimu ya chuo kikuu siyo "fashion" kwamba ilimradi nimesoma elimu ya chuo kikuu, jipe nafasi jitafakari angalia mbele miaka 3/4/5 ijayo unataka kuwa nani, hakuna kinachoshindikana, kuamua, kudhamiria na kuchukua maamuzi ni sehemu muhimu katika maisha yenu yote hivyo basi ni vyema kuwa makini zaidi katika wakati wote ambao unajitizama baada ya miaka 3/4 ya kumaliza chuo utakuwa wapi na unafanya nini!

Usikubali kubaki ulipo, usikubali kurudishwa nyuma na marafiki ulionao, amka simama imara chagua kitu kitakachokufanya baada ya miaka 3/4 ya chuo kikuu unakuwa kweli watofauti kubwa.
Ni kweli ajira hakuna hasa zinazotoka serikalini kwa maana ni chache na zina ushindani mkubwa, kama lengo lako hasa ni ukimaliza upate ajira serikalini basi utakuwa hujaamua kuwa nani baada ya miaka ya chuo.

Tuwe na tabia ya kujitizama na kujiwekea malengo makubwa lakini yanayofikika katika maisha yetu ya Chuoni na yakila siku, kwa kuzingatia hili tuwe tayari kuweka mawasiliano sahihi na watu sahihi kwa muda sahihi, tujitahidi kutafakari pale unarudi nyumbani baada ya miaka ya chuo na upo upo tu unaangalia wazazi, tukumbuke suala la kujituma kwa moyo wa dhati liwe kipaumbele chetu kikubwa.

Kumbuka; nyakati zinabadilika Ila mtazamo wa wewe uwe nani baada ya miaka ya chuo unao wewe na wewe ndo kiongozi mkubwa.

Usiende chuo kikuu kwasababu nimechaguliwa kwenda lazima niende, hapa naelezea kidogo jambo, elimu ya chuo kikuu siyo fashion kwamba baada ya miaka 3 ukiona ulichosoma hakifai utarudi tena ukasome kingine, mafanikio yako unayo wewe fanya maamuzi sahihi leo ili kesho ukawe mshindi katika jamii yako na familia yako. Acha kufuata mkumbo.

Leo nakupa kazi ya kufanya kijana uliyechaguliwa kwenda chuo kikuu, tenga saa moja kaa pahala patulivu kuwa na notebook yako na kalamu, zima simu yako, sali kwa imani yako kisha anza kuandika unataka nini baada ya miaka 3 /4 ya chuo kikuu kisha tafakari je ninachoomba kitanifikisha hapo?

Halafu kesho tutaelezeana humu humu kwa comments je tunajionaje baada ya miaka 3/4 ya chuo.

Mwisho kabisa, kumekuwa na wanafunzi wengi waliomaliza michepuo mbalimbali wakiomba ushauri juu ya nini cha kusomea chuo kikuu na ambapo akimaliza ataajiriwa,nawaomba sana tuwaambie wakasome vitu wavipendayo na sio vitu vitakavyowapa ajira ya kuajiriwa wakimaliza masomo yao mfano,Kuna mwalimu wa wito na mwalimu alietaka sehemu ya kuajiriwa tu.

Nawasilisha.
 
Upvote 190

The Boldly

JF-Expert Member
May 21, 2017
2,378
2,000
Khadija Mtalame

Samahani.....kwa mfano mimi nilitala kusomea Uandishi wa habari,nilipenda.

Lakini aliyetakiwa kunisomesha alinichagulia cha kwenda kusoma.Huoni kuwa bado hatujafikia huko ambako mtoto ndiye mwenye mamlaka ya kupanga??
 
The book,

Ndio maana nikaja na Uzi huu ambao lengo lake kuu Ni kuhakikisha kwamba,kila mtanzania mzazi/mwanafunzi wanatambua njia Bora ya kuenenda ili baadae kuajiriwa isiwemo akilini mwa mwanafunzi/muhitimu na aweze kujiajiri
 
The Boldly

JF-Expert Member
May 21, 2017
2,378
2,000
The book,

Ndio maana nikaja na Uzi huu ambao lengo lake kuu Ni kuhakikisha kwamba,kila mtanzania mzazi/mwanafunzi wanatambua njia Bora ya kuenenda ili baadae kuajiriwa isiwemo akilini mwa mwanafunzi/muhitimu na aweze kujiajiri
Mkuu,

Upo sahihi,ila inawezekana vipi??

Kwa mfano,nimesoma uhandisi....nitaweza kukiajiri bila mtaji wa maana??
 
Khadija Mtalame

Senior Member
Jul 14, 2021
124
500
Mkuu,

Upo sahihi,ila inawezekana vipi??

Kwa mfano,nimesoma uhandisi....nitaweza kukiajiri bila mtaji wa maana??
The Book

Unajua kinachoharibu vijana wa Sasa hivi Ni kusomea kitu na kutaka sifa ya kuitwa mfano. Dr.. injinia, nk. Ni kweli kwa kuwa elimu yetu inathaminiwa kwa vyeti , mtu huyu lazima atakariri ili tu aitwe injinia au Dr.,na mwisho atakaa kusubiri kuajiriwa,

Lakini,endapo utasoma kwa kupenda kutoka moyoni hata Kama wewe Ni injinia Nakuhakikishia Nikikupa 10000, inaweza kuwa mtaji mkubwa sana wa kujiajiri ,

Mtaji sio lazima upate 1000000 hata tshs 1000 Ni mtaji mkubwa sana hasa Kama unapenda unachokifanya

"Passion first and everything will fall into place"
 
Unajua mkuu,

Haya mambo ni rahisi sana kuongea,kiuhalisia ni ngumu mno.
 
Gwamanga

Member
Jun 25, 2021
65
150
Suluhisho la tatizo la Ajira linaweza taftiwa Mwarobaini tukiungana pamoja kutafta suluhu, Hongera kwa Andiko murua.
Pia pita hapa upate perspective nyingine!👏👏👏
 
Khadija Mtalame

Senior Member
Jul 14, 2021
124
500
Suluhisho la tatizo la Ajira linaweza taftiwa Mwarobaini tukiungana pamoja kutafta suluhu, Hongera kwa Andiko murua.
Pia pita hapa upate perspective nyingine!👏👏👏
Exactly Kaka,tupo pamoja
 
Marjo Mlekwa

Member
Jul 18, 2021
38
125
Habari wanajukwaa;

Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa kunipa afya na wakati mwema Kama huu,ili niweze kutoa upako wa kweli kuhusu hatma ya wanafunzi waliomaliza KIDATO cha 6 kuhusu nini cha kusomea baada ya Necta kutangaza matokeo yao.

Pili na mwisho katika utambulisho,hongereni sana vijana wote mliofanikiwa kufaulu mtihani huo na kufanikiwa kutimiza ndoto zenu.

Mambo yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa katika kuelekea kuchagua masomo ya chuo kikuu,

MOJA,

Vijana wote wanaotaka kufanya maombi ya chuo kikuu wanatakiwa kuhakikisha kwamba WANAISHI NDOTO ZAO, kutokana na kuwepo kwa shida ya ajira ambapo kumekuwa na wahitimu wengi ambao wameshindwa kujiajiri na kuajirika kutokana na namna elimu walivyopata.

Mwanafunzi au mtu yoyote anaetaka kufanya chaguzi ya fani ya kusomea chuo kikuu anatakiwa kwanza kujipima na kuangalia Nini anapenda maishani mwake? Na sio akasomee kitu gani chenye ajira. Mfano, unaweza kukuta kipaumbele Cha serikali ya JMT Ni afya na ualimu sayansi na ukaamua kwenda kusoma katika kada hizo,lakini mwisho wa siku ukamaliza na ukasubiriwa kuajiriwa na endapo hutaajiriwa elimu yako itapotea pia utakuwa umepoteza ndoto zako.

Lakini, endapo mtu ukaamua kusoma kitu unachokipenda moyoni mfano, endapo unapenda kuwa fundi mshonaji wa nguo tangu ukiwa mdogo,Ni lazima uhakikishe kwamba unachagua masomo ambayo ukienda kusoma darasani utakuwa na amani ya moyo na utayapenda sana ,ambapo mwisho wa siku utaelewa na hautakuwa mzigo mtaani Mara utakapomaliza masomo yako.

Hivyo,nawashauri sana vijana muombe vitu ambavyo mnavipenda kutoka moyoni na sio vitu ambayo unahisi au umeshauriwa vina ajira endapo utamaliza,siku hizi hakuna kitu utasoma kitakupa ajira moja kwa moja, hata aliesomea Udaktari anaweza kumaliza na asiajiriwe lakini endapo utasoma Udaktari kwa kupenda hata usipoajiriwa utaweza kujiajiri mwenyewe.

Hivyo napenda kuwaasa, vijana na watanzania wote kwamba ILI TUWEZE KUPAMBANA NA AJIRA KWA WAHITIMU WA VYUO VIKUU,tafadhali tuhakikishe kwamba tuwaambie vijana wetu wakasome vitu wanavyovipenda na sio kitu ambacho anahisi ataweza kuajiriwa endapo akimaliza masomo yake.

PILI, ni ndoto ya kila mwanafunzi anaposoma anakuwa amedhamiria kuwa nani na kwasababu gani. Kwa kuzingatia hilo nipende kuwaambia vijana waliomaliza kidato Cha sita elimu ya chuo kikuu siyo "fashion" kwamba ilimradi nimesoma elimu ya chuo kikuu, jipe nafasi jitafakari angalia mbele miaka 3/4/5 ijayo unataka kuwa nani, hakuna kinachoshindikana, kuamua, kudhamiria na kuchukua maamuzi ni sehemu muhimu katika maisha yenu yote hivyo basi ni vyema kuwa makini zaidi katika wakati wote ambao unajitizama baada ya miaka 3/4 ya kumaliza chuo utakuwa wapi na unafanya nini!

Usikubali kubaki ulipo, usikubali kurudishwa nyuma na marafiki ulionao, amka simama imara chagua kitu kitakachokufanya baada ya miaka 3/4 ya chuo kikuu unakuwa kweli watofauti kubwa.
Ni kweli ajira hakuna hasa zinazotoka serikalini kwa maana ni chache na zina ushindani mkubwa, kama lengo lako hasa ni ukimaliza upate ajira serikalini basi utakuwa hujaamua kuwa nani baada ya miaka ya chuo.

Tuwe na tabia ya kujitizama na kujiwekea malengo makubwa lakini yanayofikika katika maisha yetu ya Chuoni na yakila siku, kwa kuzingatia hili tuwe tayari kuweka mawasiliano sahihi na watu sahihi kwa muda sahihi, tujitahidi kutafakari pale unarudi nyumbani baada ya miaka ya chuo na upo upo tu unaangalia wazazi, tukumbuke suala la kujituma kwa moyo wa dhati liwe kipaumbele chetu kikubwa.

Kumbuka; nyakati zinabadilika Ila mtazamo wa wewe uwe nani baada ya miaka ya chuo unao wewe na wewe ndo kiongozi mkubwa.

Usiende chuo kikuu kwasababu nimechaguliwa kwenda lazima niende, hapa naelezea kidogo jambo, elimu ya chuo kikuu siyo fashion kwamba baada ya miaka 3 ukiona ulichosoma hakifai utarudi tena ukasome kingine, mafanikio yako unayo wewe fanya maamuzi sahihi leo ili kesho ukawe mshindi katika jamii yako na familia yako. Acha kufuata mkumbo.

Leo nakupa kazi ya kufanya kijana uliyechaguliwa kwenda chuo kikuu, tenga saa moja kaa pahala patulivu kuwa na notebook yako na kalamu, zima simu yako, sali kwa imani yako kisha anza kuandika unataka nini baada ya miaka 3 /4 ya chuo kikuu kisha tafakari je ninachoomba kitanifikisha hapo?

Halafu kesho tutaelezeana humu humu kwa comments je tunajionaje baada ya miaka 3/4 ya chuo.

Mwisho kabisa, kumekuwa na wanafunzi wengi waliomaliza michepuo mbalimbali wakiomba ushauri juu ya nini cha kusomea chuo kikuu na ambapo akimaliza ataajiriwa,nawaomba sana tuwaambie wakasome vitu wavipendayo na sio vitu vitakavyowapa ajira ya kuajiriwa wakimaliza masomo yao mfano,Kuna mwalimu wa wito na mwalimu alietaka sehemu ya kuajiriwa tu.

Nawasilisha.
Safi
 
Mwamba 777

JF-Expert Member
Nov 23, 2020
1,303

tatizo la elimu ya Tz ni theoretically, sio practically, walimu wanatoa course work kibao, wanafunzi nao wanakariri na kumeza desa kama lilivyo ili wapate GPA kubwa. Mwisho wa siku kujiajiri hawawezi na mtaji hawana. Mi naona elimu ya Tz ilisha expire.

Elimu ya form four inatosha. Wazazi badala ya kuangaika kusomesha hizo fedha wawape na wawasimamie watoto wafanye kazi/ biashara au wawekeze kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo.
 
Khadija Mtalame

Senior Member
Jul 14, 2021
124
500
Kusoma chuo kikuu ni msingi bora wa ajira? Acha kufananisha ajira na vitu vya ajabu ajabu! Ni wahitimu wangapi wapo mtaani na vyeti vyao mikononi?
Horseshoe Arch

Ukilisoma andiko langu, linatoa direction way path wapi pa kupita na njia zipi za kuzifata ili ufanikiwe,

Ktk maisha Kuna watu waliosoma na ambao hawajaenda shule,

Ukiona mtu kasoma ushauri wangu utamfaa zaidi na atafanikiwa,Kama mtu hajasoma..,afanye pia akipendacho lazima atoboe
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom