Ushauri kwa Wakuu wa Mikoa na wakurugenzi wa Manispaa/ Jiji wanaohangaika na suala la “Wamachinga”

Yaleyale

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
1,588
2,000
Nianze kwa kuwapa hongera na kuteuliwa na Mh. Rais kuchaguliwa katika majukumu hayo. Siku za karibuni Mh. Rais alitoa maelekezo kuwa wamachinga waachwe kufanya shughuli zao katikati ya Miji. Sina sababu ya kuhoji maelekezo haya ya Rais maana sio mteule wake. Aidha, ni imani yangu kuwa mmeelewa vyema ndiyo maana hakuna mteule aliyeachia ngazi majukumu yake kama njia ya kutokubaliana na Rais.

Baada ya kauli ile, baadhi ya vyombo vya habari zilichapisha “wamachinga” wakiwa wamefurika mitaani kwenye baadhi ya Mitaa ya Miji Mikuu. Kuzagaa kwa “wamachinga” wale kila sehemu inaweza kutafsiriwa kuwa mmeshindwa kazi maana Rais hajasema wamachinga wazagae hovyohovyo bali wapatiwe fursa ya kufanya shughuli zao katikati ya Miji lakini kwa utaratibu unaokubalika. Kuendelea kuzagaa mitaani wakati viongozi mpo ni dalili mbaya sana kwa weledi wa watendaji na hata wateule wa Mh. Rais. Hivyo, sitashangaa mtu akitumbuliwa kwa kukosa kutekeleza maagizo la Mh. Rais.

Tatizo ninaloona hapa kwetu ni jamii hasa viongozi kuona “wamachinga” kama mzigo kwa taifa na sio fursa. Kama mtaalam wa mambo ya miji, napenda kutoa pendekezo kwenu wateule wa Rais namna ya kutoa fursa kwa hawa “wamachinga” kuendelea kufanya shughuli zao mijini wakati mnaendelea na taratibu za kuwaandalia maeneo mazuri ya kufanyia kazi zao bila kuzagaa kila sehemu.

Nitatolea mfano wa Kariakoo, Watendaji wa Mamlaka za Jiji na Manispaa ya Ilala wanaweza kufanya TIA (Traffic Impact Assesment) kwenye mitaa ya Kariakoo walikozagaa “wamachinga” bila utaratibu. Wakaja na pendekezo ya kufanya barabara kadhaa kuwa one way kwa magari na kuondoa on street parking. Kwa kufanya hivyo, utapata eneo la kutosha kuwapanga “wamachinga” wakiwa na baiskeli/ vitoroli vya kufanyia biashara zao (mfano wa baiskeli zinazotumiwa na Azam kuuza ice cream barabarani). Vitoroli vile vinaweza kusimamishwa sehemu ya ukubwa wa mita moja za mraba tu (1sqm). Hivyo ukiwa na barabara za jumla ya mita 3,000 unaweza kuweka “wamachinga” 2600-2800. Wamachinga hawa wanatambuliwa na wanapaswa kulipia kodi ya angalau Tsh 1000 kwa siku. Kufanya hivi una uhakika wa kukusanya takriban Mil 80 kwa kwezi ambazo ni sawa na Mil. 960 kwa Mwaka.

Kwa kufanya hivi, utaweza kukusanya mapato kwenye halmashauri yako na bado ukatekeleza maelekezo ya Mh. Rais ya kuwaruhusu wamachinga kubaki Mjini. Otherwise, kinachofanyika sasa ni uholela usiyo na tija yoyote kwa Taifa.

Ni wazo tu wateule wa Rais.
 

Void ab initio

JF-Expert Member
Mar 1, 2015
5,653
2,000
Wamemsusia mkuu, yeye si katoa go ahead. Lakini kwakweli kwasasa imekuwa kero katikati ya mji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom