SoC01 Ushauri kwa wahitimu wa vyuo na wanaotarajia kujiunga na vyuo mbalimbali nchini

Stories of Change - 2021 Competition

Mirr

Member
Jul 14, 2021
16
30
Ndugu wana jukwaa amani iwe juu yenu!

Hakika kama tujuavyo elimu imekuwa chanzo cha maarifa tangu kuanza kwa historia ya mwanadamu lakini pia katika baadhi ya vitabu vya imani vimeandika "MKAISHIKE ELIMU" kwa maana msisitizo nikwamba elimu yenye tija na malengo ina manufaa kwa jamii na taifa kiujumla.

Leo hii elimu ambayo mwanadamu alitakiwa kuipata imusaidie imegeuka shubiri kwa kuleta changamoto ya kushindwa kuwanufaisha wasomaji na jamii iliyokusudiwa kwa kwasababu wahitimu wengi baada ya kumaliza vyuo wanategemea wapate ajira ili walitumikie taifa lao,pengine hii dhana imeshapitwa na wakati hivyo kwa hiki kipindi wahitimu wanatakiwa kubadili dhana kujieletea manufaa.

Ushauri kwa wanachuo wanaohitimu vyuo mbalimbali nchini Tanzania.

Naomba niwe tofauti kimtazamo na wahitimu wengi kipindi hiki kwamba "Siku hizi elimu haina faida".

Kwanza kabisa, kwa wahitimu wote unapofanikiwa kumaliza masomo yako, jaribu kutumia marafiki zako kupeana michongo yenye faida. Vyuo vinakusanya wanafunzi wa aina mbalimbali hivyo wengine wanakuwa na frusa ama connection kupitia ndugu zao kwenye mashirika mbalimbali kama vile mashirika yasiyo ya kiserikali. Kosa kubwa wengi hufanya baada ya kumaliza chuo ni kushindwa kuendelea kuwasiliana ili kupeana frusa maeneo tofauti tofauti. Hivyo wengi wao hufuta namba za marafiki wa vyuoni, kujiondoa kwenye magroup ya watsapp na majukwaa mengine ya kielimu yanayounganisha wanachuo mbali mbali wa vyuo tofauti tofauti, wanakuwa busy katika kutafta maisha aidha kwa kuoa na kuolewa na kuendelea kulaumu suala la ajira kumbe pangekwepo na ushirikiano baada ya chuo huenda frusa na mawazo mengi yangesaidia kubuni na kugundua frusa kwa urahisi.

Pili, ukimaliza chuo usikae sana nyumbani kwenu kama haupo tayari kuchakarika kwa kuogopa watu watakuonaje pengine kwa kufanya kazi isiyo hadhi yako. Kwa kuondoka nyumbani kwenda mikoa mingine itakupa ujasiri wa kutokuchagua kazi kwasababu pengine haujulikani sana hilo eneo itasaidia kufanikiwa haraka. Usiogope kwenda mbali na nyumbani kwenu katika kutafta maisha maana hata Mungu anasema "ardhi yake ni pana hivyo sio lazima uishi sehemu moja,mungu hampendi mtu anayekaa sehemu moja isiyo na ridhiki alafu aanze kulaumu na kukufuru wakati dunia ni kubwa sana.

Ushauri kwa wanaotegemea kujiunga na vyuo mbalimbali nchini.

Kwanza kabisa kwa wote mnaotegemea kwenda vyuoni,msisikilize maneno ya wahitimu waliokata tamaa. Wao huwakatisha tamaa kwa kuwaambia hakuna ajira baada ya chuo, mara kozi ni ngumu, wengine wanawapangia vitu vya kwenda kusomea pasipo kutazama vipawa vyenu. Hawajui katika harakati za kielimu tunatengeneza connection na marafiki mbali mbali chuoni ambapo baadaye ikitumika vizuri itakuwa rahisi kufanikiwa kwenye maisha mbali na suala la ajira.

Jambo la pili, ukifanikiwa kuingia chuoni jaribu kuishi vizuri na wenzako, soma kwa kushirikiana ili mtengeneze habit(tabia) hata baada ya chuo mfanye kupeana madili ya maisha bila kuchukiana. Hii pia itasaidia mfaulu na kumaliza kwa mwaka mmoja pasipo kukariri mwaka miongoni mwenu hivyo itawapa mda mzuri kupambana na maisha mengine mtaani kwa muda mwafaka na kupata dili kwa pamoja kuliko kusubiriana kwa uzembe wa miongoni mwenu kukariri mwaka.

Tatu, mkienda chuo mkaepukane na tabia ambazo hazikubaliki kwenye jamii ya watanzania kama vile ulevi, uasherati, ujambazi, na tabia zingine ambazo sio hulks ya jamii iliyostaarabika. Kwasababu matokeo ya hizi tabia itapelekea kupata madhara makubwa kama vile magonjwa sugu mfano UKIMWI ambao bado unaisumbua dunia na kupelekea kukatisha ndoto zenu mlizozikusudia.

Mwisho, mkumbuke kila mmoja wenu atatoka familia tofauti tofauti, kuna wengine watakuja na magari, ama vitu vya gharama hivyo hivyo visiende kukupa msongo wa mawazo ama kuwaza sana kupelekea uanze kuwaiga au kutamani maisha wanayoishi wao hakika nakwambia hautamaliza chuo kwa furaha. Kikubwa malengo yawe katika kukamilisha ndoto yako na usiende kufuatilia maisha ya watu wengine chuoni, hakika utamaliza chuo salama salmini na mungu atakuruzuku kadri awezavyo.

Nahitimisha kwa kusema WAHITIMU NA WANAOTARAJIA kwenda chuo,endeleeni kumuweka MUNGU mbele katika kila changamoto inayotokea na muamini Mungu ndio mjuzi wa kila mnalopitia.

Asanteni sana.
mirajihathuman@gmail.
0765568050
 
Back
Top Bottom