Ushauri kwa wahanga wa bomoabomoa na watanzania wote

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Mimi binafsi naamini serikali ilipotoka katika suala la bomoa bomoa. imani yangu hiyo inatokana na kujua ukweli kuwa hakuna mwananchi anayependa kujenga sehemu isiyofaa na ama kuhatarisha maisha yake au kuhatarisha maisha ya wengine au viumbe wengine.

Jukumu la kuhakikisha wananchi hawa wanakaa kwa ustaarabu huo liko kwa serikali na serikali inaposhindwa kutimiza wajibu wao huo matokeo yake ni vurugu katika makazi kila mmoja anajiamulia ajenge wapi na kwa vipi.

Ki msingi wananchi hawa waliojenga mabondeni na wengine kuvamia hata viwanja vya umma ni wahanga wa uzembe wa serikali na hawa hawawezi kuchukuliwa kama ndio wavunja sheria na kuwabomolea au kwa maneno mengine kuwatwisha dhamana ya makazi holela tuliyo nayo.

Mimi swali langu kwa serikali ni je wanatambua tatizo hili wanalotatua kwa kuendesha bomoa bomoa limetokana na nini? sijui kama watanijibu lakini mimi naamini limetokana na wao kuwa wazembe kwa kuacha kupima miji yetu na kuweka utaratibu ambao wananchi wangeufuata. kama wanabishi waseme ndani ya miaka tuseme kumi iliyopita wamepima viwanja vinagapi na watueleze ukuaji wa miji yetu inakua kwa kasi kiasi gani kulinganisha na kasi yao ya kupima viwanja au kutoa mwongozo wa makazi?

Mbali na uzembe kuna ufisadi pia kwa wachache kutumia ofisi za umma kufanya ufisadi. eti kupima viwanja mpanga tukakope mabilioni benki ya dunia kuendesha mradi wa kupanga makazi yetu. kwenye viwanja vilivyopimwa tujiulize ni viwanja vingapi vimechukuliwa na watumishi wa sekita zinazohusika na kupima na kuanza kufanya biashara kwa kuviuza kwa bei kubwa.

Bado kuna wengine walikuwa na dhamana ya kupima lakini wanamiliki vitega uchumi katika maeneo machache yaliyopimwa na kutokana na uchache wa maeneo yenye ustarabu wanapata biashara nzuri tu kama kupangisha majengo kwa gharama kubwa. na kwao hawa kupanga maeneo mengi kungemaanisha kuharibu baishara zao binafsi hivyo walikwepa kuandaa mipango ya kuboresha makazi yote ili kulinda biashara zao katika maeneo machache yenye ustarabu.

Unatoka hapo unasema mwananchi huyu aliyeshindwa kuelekezwa la kufanya na watumishi hawa akajenga nyumba yake eneo la bonde unatuma wenye makosa hawa kumbomolea mhanga huyu.

Serikali ya leo inadhani yenyewe ni polisi wa kukamata waovu katika sekita ya makazi lakini bahati mbaya pilisi hawa hawatumii busara kabisa wao wanaangalia ni nani yuko mahali pasipostahili bila kujiuliza kwa nini huyo yuko hapo?

Ushauri wangu
1. Serikali jambo la kwanza la kufanya ni kutambua tatizo linaloleta makazi holela kuwa ni wao kutokutimiza wajibu wao wa kuwa viongozi katika makazi kwa kuanza kutunga sheria na kupanga makazi yote.

2. Serikali kutambua kuwa wale walio sehemu zisizostahili ni wahanga wa tatizo sio wahalifu hivyo kwa kuwa hatuwezi kuvumilia makazi holela basi serikali itoe miongozo na kipindi cha mpito cha kama miaka mitano au saba ili wananchi hawa waweze kupata mda wa kujiandaa kubadilisha makazi.

3. Kupanga makazi yetu sio lazima tulenge kuwapa wananchi hati kama ni gharama kubwa bali tuweke hata arrangemet on ground kwa kupanga program zinazoweza kujiendesha zenyewe kwa wananchi kuchangia kidogo sana

Mwisho ni kuwauliza serikali ya awamu ya tano kuwa tangu wameingia madarakani wamepima viwanja viwangapi ili kutatua tatizo la ujenzi holela? na kama hamjapima mnabomolea waliojenga ovyo mnadhani wanaohitaji kujenga kwa sasa wanajenga wapi? kama sio kuwaacha wananchi wajenge wanavyotaka alafu unaangalia katika bahati nasibu zao hizo nani kabahatisha kujenga sehemu sahihi na aliyebahatisha sehemu isiyofaa unambomolea. hii kwa kingereza huitwa corrective approach ambayo mara nyingi hutumiwa na watu wanaofanya wasichokijua hivyo husubiri matatizo yatokee alafu wanaanza kuyatatua.

Tunataka serikali ya awamu ya tano ijielekeze katika preventive approach kwa kutatua matatizo ya makazi kabla hayajatokea. wataalamu wakae waplani na kuweka utaratibu alafu wananchi wanatekeleza na hapo kweli wanaokiuka wanakuwa ni wahalifu na sio wahanga na serikali inawajibika kuwawajibisha.

Kama serikali haitimiza wajibu wake tunategemea mihimili mingine iwakumbushe hawa wajibu wao.
 
mjadala umefunguliwa hivyo mnaruhusiwa kuchangia mawazo yenu pia
 
Back
Top Bottom