USHAURI KWA WADOGO ZANGU MNAOTAKA KUUNGANISHA CPA BAADA YA CHUO

Singida ndio home

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,192
3,353
Hello wanafunzi wa vyuoni hususani wa degree za accounting, poleni na mihangaiko ya quizzes, tests, assignments, presentations, discussions bila kusahau misuli ya mwisho mwisho kupukuta gpa.

Kwa sasa hali inavyoenda kwenye taaluma hii ya uhasibu degree zimekuwa kitu cha kawaida sana bila kusahau serikali ilitoa tamko kwamba hakuna kumtambua muhasibu mwenye degree bila cpa, kwa ufupi cpa ndo imekua new era ya kazi za uhasibu hapa nchini na hata katika matangazo mengi ya kazi za uhasibu vigezo huwa ni kuwa na degree + cpa.

Niende moja kwa moja kuendana na kichwa cha habari, kutokana na hayo niliyoyasema hapo juu kwa sasa wanafunzi wengi hususani wa degree za accounting wamekuwa wanaunganisha moja kwa moja kuanza kusomea cpa, baada ya kumaliza mitihani july au august wanafunzi wanaunganisha moja kwa moja cpa ili wafanye sitting ya November ama wanapumzika kidogo na kuanza kujiandaa januari kwa mitihani ya May.

Wengi wamejikuta wakifanya sitting nyingi mno, wengine kusimamishwa baada ya kufanya sitting zaidi ya sita na wengine hadi kuacha wenyewe kwa hiari yao mitihani, I have to be honest maana cpa ni ngumu na ni lazima uelewe unachosoma tofauti kabisa na vyuoni ambako possible questions zilikuwa zinaotewa, course works zilikua zinabeba watu, group discussions wavicu walichukua marks pasipo kudiscuss, n.k. Cpa ni tofauti sana maa marks zote 100 zinatafutwa katika chumba cha mtihani katika sittings mbili kila mwaka may na November.

MASOMO:
B1 finacnial management
B2 financial accounting
B3 audit 1
B4 tax 1
B5 perfomance management
B6 business etthics
C1 finacnial accounting 2
C2 audit 2
C3 corporate finance
C4 tax 2

KWA WALE WANAO UNGANISHA MOJA KWA MOJA ILI WAFANYE PEPA NOVEMBER

Kundi hili huwa na muda mchache wa maandalizi, cpa watu wanaanza kujiandaa mwishoni wa mwezi june ila hawa huanza kujiandaa july ama june na hapo hawajapata hata likizo wameunganisha moja kwa moja,

kundi hili inabidi lifanye masomo manne ambayo ni b3, b4, b5 na b6. Combination hii masomo ambayo watu wenye mda mchache watamudu.

Mitihani ya November mara nyingi humalizika tarehe 5, jipe ya mwezi, mwezi,Mwezi December unapoanza tu anza hapohapo masomo mawili b1 na b2.

Mwezi wa 12 mwishoni matokeo yakitoka fanya masomo haya mwezi may kwa mtiririko huu:

Kama umepita masomo yote fanya b1, b2, c1 na c4

kama umefelei somo moja fanya b1, b2, c4 na somo ulilofeli,

Kama umefeli masomo mawili fanya b1, b2 na hayo masomo mawili uliyofeli.

Baada ya hapo utakua mzoefu, sitting zinazofata annza kufanya unavyoamini wewe.

KWA WALE WANAO UNGANISHA MOJA KWA MOJA ILI WAFANYE PEPA MAY.

Hili ni kundi lenye mda wa kutosha sana tofauti na wenzao wanaounga moja kwa moja, kwa hili kundi watavyomaliza vyuo july au august nawasihi wapumzike mpaka October katikati ya mwezi, ifikapo tarehe 16 inabidi maandalizi yaanze kwa ajili ya mtihani wa may mwakani.

Kwa vile hili kundi lina mda wa kutosha inabidi wafanye masomo matano (5), masomo hayo ni b1, b2, b3, b4 na b6.

Mwezi wa 6 mwishoni matokeo yakitoka fanya masomo haya mwezi NOvember kwa mtiririko huu:

Kama umepita masomo yote fanya b1, c1, c2 na c4

kama umefelei somo moja fanya b1, c2, c4 na somo ulilofeli,

Kama umefeli masomo mawili fanya b1, c4 na masomo mawili uliyofeli.

Kama umefeli masomo matatu au zaidi fanya kwanza hayo uliyofeli

MBONA NIMEONA WANARUHUSU KUFANYA HATA MASOMO SITA KWA MIGO?

Ndio wanaruhusu na kuna watu wachache mno wanaofaulu yote kwa mpigo, katika watu 2,000 wanaowezaga kutushangaza wanakuaga hawazidi watano mara nyingi, hata ukifatilia historia za hawa watu ni vichwa sana toka shule ya msingi, ni watu ambao wana upeo usio wa kawaida wa kuelewa, hapa ndo wale wazee wa first class za 4.8, kwa kweli hadi ujaribu kufanya masomo sita ujijue kabisa wewe ni genius na wala sio wa kawaida au kilaza, Ukilazimisha kufanya hivi unaweza kufeli yote(nimeona mara nyingi) kwasababu unapoteza concetration.

RATIBA YANGU IWAJE ILI NIFAULU C.P.A?
Kama nilivyowaambia awali, CPA SIO LELEMAMA, NI KUKAZA MPAKA MWISHO, nashauri uwe unaamka saa 11 kamili asubuhi bampa to bampa mpaka saa nne usiku,tenga muda wa masaa yasiyozidi mawili kupumzika na siku ya jumamosi au jumapili upumzike, Kupumzika muhimu.

Nisome review classes au private?
Binafsi review classes naona ni kawaida tu, cha muhimu ni group discussions na kufanya maswali mengi sana. Lipia review classes somo moja tu gumu ili tu ujuane na wanafunzi wa hapo wakupenyeze hadi kwenye group discussions ya masomo ambayo hujalipia.

Material ntatoa wapi??
-group discussions and review classes
-Vitabu vya cpa: cpa blog
-past papers za cpa, acca, cpa Ireland na ca india
 
Madudu magumu ukimaliza hela hakuna, ukipata kazi unakuja pambikiziwa makesi ya uhujumu uchumi, dunia hii Haina heri
Mkumbuke ajira hakuna pia
Nani kakwambia kuwa certified public accountant unategemea ajira pekee?? Nani kakwambia kwamba ajira zinasumbua kwa cpa??

Kazi zipo na mshahara ni mnono, nakukumbusha tu C.A.G ambae pia ni C.P.A ndie anaefichua madudu ya ibadhilifu wa pesa katika serikali.

Siwezi kutype vingi, bado tunaendelea ma maombolezo ya marehemu C.P.A(T) Reginald Mengi
 
Nani kakwambia kuwa certified public accountant unategemea ajira pekee?? Nani kakwambia kwamba ajira zinasumbua kwa cpa??

Kazi zipo na mshahara ni mnono, nakukumbusha tu C.A.G ndie anaefichua madudu ya ibadhilifu wa pesa katika serikali.

Siwezi kutype vingi, bado tunaendelea ma maombolezo ya marehemu C.P.A(T) Reginald Mengi

Ujielewi
 
Hello wanafunzi wa vyuoni hususani wa degree za accounting, poleni na mihangaiko ya quizzes, tests, assignments, presentations, discussions bila kusahau misuli ya mwisho mwisho kupukuta gpa.

Kwa sasa hali inavyoenda kwenye taaluma hii ya uhasibu degree zimekuwa kitu cha kawaida sana bila kusahau serikali ilitoa tamko kwamba hakuna kumtambua muhasibu mwenye degree bila cpa, kwa ufupi cpa ndo imekua new era ya kazi za uhasibu hapa nchini na hata katika matangazo mengi ya kazi za uhasibu vigezo huwa ni kuwa na degree + cpa.

Niende moja kwa moja kuendana na kichwa cha habari, kutokana na hayo niliyoyasema hapo juu kwa sasa wanafunzi wengi hususani wa degree za accounting wamekuwa wanaunganisha moja kwa moja kuanza kusomea cpa, baada ya kumaliza mitihani july au august wanafunzi wanaunganisha moja kwa moja cpa ili wafanye sitting ya November ama wanapumzika kidogo na kuanza kujiandaa januari kwa mitihani ya May.

Wengi wamejikuta wakifanya sitting nyingi mno, wengine kusimamishwa baada ya kufanya sitting zaidi ya sita na wengine hadi kuacha wenyewe kwa hiari yao mitihani, I have to be honest maana cpa ni ngumu na ni lazima uelewe unachosoma tofauti kabisa na vyuoni ambako possible questions zilikuwa zinaotewa, course works zilikua zinabeba watu, group discussions wavicu walichukua marks pasipo kudiscuss, n.k. Cpa ni tofauti sana maa marks zote 100 zinatafutwa katika chumba cha mtihani katika sittings mbili kila mwaka may na November.

MASOMO:
B1 finacnial management
B2 financial accounting
B3 audit 1
B4 tax 1
B5 perfomance management
B6 business etthics
C1 finacnial accounting 2
C2 audit 2
C3 corporate finance
C4 tax 2

KWA WALE WANAO UNGANISHA MOJA KWA MOJA ILI WAFANYE PEPA NOVEMBER

Kundi hili huwa na muda mchache wa maandalizi, cpa watu wanaanza kujiandaa mwishoni wa mwezi june ila hawa huanza kujiandaa july ama june na hapo hawajapata hata likizo wameunganisha moja kwa moja,

kundi hili inabidi lifanye masomo manne ambayo ni b3, b4, b5 na b6. Combination hii masomo ambayo watu wenye mda mchache watamudu.

Mitihani ya November mara nyingi humalizika tarehe 5, jipe ya mwezi, mwezi,Mwezi December unapoanza tu anza hapohapo masomo mawili b1 na b2.

Mwezi wa 12 mwishoni matokeo yakitoka fanya masomo haya mwezi may kwa mtiririko huu:

Kama umepita masomo yote fanya b1, b2, c1 na c4

kama umefelei somo moja fanya b1, b2, c4 na somo ulilofeli,

Kama umefeli masomo mawili fanya b1, b2 na hayo masomo mawili uliyofeli.

Baada ya hapo utakua mzoefu, sitting zinazofata annza kufanya unavyoamini wewe.

KWA WALE WANAO UNGANISHA MOJA KWA MOJA ILI WAFANYE PEPA MAY.

Hili ni kundi lenye mda wa kutosha sana tofauti na wenzao wanaounga moja kwa moja, kwa hili kundi watavyomaliza vyuo july au august nawasihi wapumzike mpaka October katikati ya mwezi, ifikapo tarehe 16 inabidi maandalizi yaanze kwa ajili ya mtihani wa may mwakani.

Kwa vile hili kundi lina mda wa kutosha inabidi wafanye masomo matano (5), masomo hayo ni b1, b2, b3, b4 na b6.

Mwezi wa 6 mwishoni matokeo yakitoka fanya masomo haya mwezi NOvember kwa mtiririko huu:

Kama umepita masomo yote fanya b1, c1, c2 na c4

kama umefelei somo moja fanya b1, c2, c4 na somo ulilofeli,

Kama umefeli masomo mawili fanya b1, c4 na masomo mawili uliyofeli.

Kama umefeli masomo matatu au zaidi fanya kwanza hayo uliyofeli

Baada ya hapo utakua mzoefu, sitting zinazofata annza kufanya unavyoamini wewe.

MBONA NIMEONA WANARUHUSU KUFANYA HATA MASOMO SITA KWA MIGO?

Ndio wanaruhusu na kuna watu wachache mno wanaofaulu yote kwa mpigo, katika watu 2,000 wanaowezaga kutushangaza wanakuaga hawazidi watano mara nyingi, hata ukifatilia historia za hawa watu ni vichwa sana toka shule ya msingi, ni watu ambao wana upeo usio wa kawaida wa kuelewa, hapa ndo wale wazee wa first class za 4.8, kwa kweli hadi ujaribu kufanya masomo sita ujijue kabisa wewe ni genius na wala sio wa kawaida au kilaza, Ukilazimisha kufanya hivi unaweza kufeli yote(nimeona mara nyingi) kwasababu unapoteza concetration.

RATIBA YANGU IWAJE ILI NIFAULU C.P.A?
Kama nilivyowaambia awali, CPA SIO LELEMAMA, NI KUKAZA MPAKA MWISHO, nashauri uwe unaamka saa 11 kamili asubuhi bampa to bampa mpaka saa nne usiku,tenga muda wa masaa yasiyozidi mawili kupumzika na siku ya jumamosi au jumapili upumzike, Kupumzika muhimu.

Nisome review classes au private?
Binafsi review classes naona ni kawaida tu, cha muhimu ni group discussions na kufanya maswali mengi sana. Lipia review classes somo moja tu gumu ili tu ujuane na wanafunzi wa hapo wakupenyeze hadi kwenye group discussions ya masomo ambayo hujalipia.

Material ntatoa wapi??
-group discussions and review classes
-Vitabu vya cpa: cpa blog
-past papers za cpa, acca, cpa Ireland na ca india
Mkuu Kwann watu walosoma degree mbali na uhasibu wanafanya CPA kwa lengo gn???
 
Back
Top Bottom