Ushauri kwa Wabunge chini ya Spika Ndugai na Naibu wake Tulia Ackson

Enzi na Enzi

JF-Expert Member
May 29, 2020
888
821
Kwa heshima kubwa naleta ushauri huu kwenu, nikiwa kama

BUNGE ni chombo au ni sauti ya watanzania walio zaidi ya milioni 50.
Bunge ni chombo kinachojitegemea ambacho kinatakiwa kuisimamia Serikali, hivyo Bunge lina nguvu yakikatiba kutetea wananchi wake ambao ni wakulima na wafanyakazi.

Mwaka huu 2020 to 2025 chama changu cha CCM ndio kinachotawala Bunge lote kuliko miaka yote iliyopita tangu tuanze mfumo wa vyama vya siasa.

USHAURI :
Spika na wabunge wetu, sasa hivi katika nchi hii kunakundi linaonekana halina mtetezi, nalo ni kundi la WAFANYAKAZI ukiondoa Majeshi yetu na Taasisi zake, labda na baadhi ya sekta chache sana kama TRA.

Takriban miaka mitano sasa, wafanyakazi hawana mtetezi, maana hata vyama vyao navyo ni kama vimeogopa maana nao ni waajiriwa.

Naamini Bunge likiwa pamoja chini ya Spika kama kipindi cha Samweli Sitta wakati wanasimamia ufisadi wa DOWANS na Richmond hawa wafanyakazi watapata mtetezi.

Wabunge mna uwezo wa kusema, ama Bungeni au katika vikao vyenu vya Wabunge wa CCM.

Wafanyakazi saivi, wanatukanwa hadharani, lakini pia hata taratibu za kiutumishi hazifuatwi.

Wateteeni wafanyakazi wanao onewa, wasiosikilizwa, simamieni viongozi wanaowaonea wafanyakazi hawa! Maana nao ni binadamu, wanaweza kuwepo kazini jina tu. Kazi usipoipenda huwezi kuifanya kwa moyo!

Maana viongozi wakubwa saivi wanawatetea wakulima peke yao, lakini wakulima hawa hata matokeo hawayaoani maana watendaji wako fastreted

Anapokuwepo kiongozi mmoja ambaye anaweza kuamua lolote, muda wowote, na jambo lolote, hii ni hatari sana.

Kama tatizo ni katiba, Waziri wa Katiba ashirikiane na Spika na baadae Bunge zima wabadilishe hii katiba.

MAANA KAMA HAYA YANAYOFANYIKA YANAFANYIKA KWA MUJIBU WA KATIBA BASI KUNA KILA SABABU YAKUMPUNGUZA NGUVU YA RAIS

Naona hatari yakuja kupata Rais ambaye atakuwa anaamua mambo atakavyo k ilivyo sasa.

Bunge lisiposimama kama Bunge, itakuwa hakuna kimbilio jingine zaidi ya Rais

Ndo maana watu wenye shida huwa wanamfuata Rais popote alipo, maana walishajua hakuna chombo wala kiongozi anayeweza kuwasaidia, nguvu iko kwa mtu mmoja.

Huu ni ushauri , unaweza kuchukuliwa au kuachwa, ila kiukweli yawezekana nitume tu ndo inakipa kutawala chama changu cha CCM .

Bado mnao muda wakujisahihisha ,
Enzi na Enzi
Dec 2020.
 
Zaidi ya 60% ya wabunge wa hilo bunge wamepata ubunge kwa maagizo ya rais. 30% wamepata kwa udhaifu wa mfumo na kutoa rushwa. 10% tu ndio wako kihalali hapo bungeni nao hawajiamini. Unapokuwa na bunge la hivyo usitegemee kama watakuwa na ajenda yoyote tofauti na aliyo nayo rais. Kama watajadili basi ni petty issue hasa zile za kuwakomoa walio kinyume na watawala, lakini hawana uwezo wowote wa kulinda maslahi ya mtu kama rais hana utashi huo kwa sasa.

Na kama watabadili hiyo katiba kama inavyoshauriwa, basi sio kupunguza madaraka ya rais, bali watamuongezea muda wa kukaa madarakani, ili awalipe fadhila ya kuwa wabunge tena kwa ajili ya kulinda matumbo yao. Kwa ujumla hakuna bunge hapo, bali kina kundi la wanaccm watoa rushwa, na wapenda madaraka ili wabadilishe maisha yao.
 
UMEMALIZA MKUU...

Yaani hii ni fasiri iliyokwenda skuli! Waongezee Dozi hao mkuu maana tuna TIKITI sio Bunge
 
Back
Top Bottom