Ushauri kwa waajiri katika swala la matangazo ya ajira

Tom26

New Member
Jul 15, 2021
3
3
Mimi ni kijana mtanzania ambaye nimemaliza elimu ya chuo kikuu kada ya ualimu wa sayansi na nimehudhuria usaili mara kadhaa na leo nataka nizungumzie swala la matangazo ya ajira kwa taasisi zinazotoa ajira.

Ajira ni changamoto ambayo inatukabili vijana wengi sana na inapotokea tangazo la ajira hasa kwa kada ambayo umesomea unajipa moyo kutuma maombi na kutumia muda mwingi kujiandaa na pia hata fedha kwa ajili ya kutoa kopi za vyeti, na wasifu, na kwa ajili ya nauli kufika sehemu ya tukio kwa ajili ya usaili.

Lakini hali na mategemeo yanakuwa tofauti unapofika eneo la tukio ambapo wakati unafanya usaili unakutana na maswali ambayo yanakuonyesha kuwa kuna mtu ambaye wanamtafuta mfano wa maswali hayo ni umetokea sehemu fulani (anaitaja)?

Unamjua fulani? Pia unakutana na maswali hata hayaendani na kazi husika. Mwisho wa siku wanakuambia nenda tutakupigia simu, lakini baada ya muda ukiulizia unaambiwa bado tunajiandaa na tutawaita. Siku zinaenda na ukimya uko pale pale unaamua kuuliza wafanyakazi wa pale unaambiwa tayari mtu ameshaajiriwa na ukifwatilia ni mtu kutoka sehemu uliyoulizwa na anafahamiana na mtu uliyeulizwa kuwa unamfahamu. Hii inajenga picha kuwa tayari walishachagua mtu na usili ilikuwa ni geresha tu.

Kijana huyu amepoteza muda, fedha, na pia huenda akaanza hata kukata tamaa ya kuomba kazi.

Ushauri wangu kwa wenye taasisi na hasa watu wa rasilimali watu.
1. Kama unatambua tayari nafasi iliyopo kwenye taasisi yako kuna mtu yupo kuijaza, haina haja ya wewe kutoa tangazo la hiyo kazi. Hii itaokoa muda wako na wa watu ambao wanakuja kufanyiwa usaili.

2. Hakikisheni maswali ya usaili hayaendi nje ya kazi ambayo umetangaza.

3. Kuweni wawazi kama mtu amefanya usiili na hana vigezo mnavyohitaji basi mwambieni pale pale na ikiwezekana mpeni ushauri kuwa wapi anakwama hata Mungu atawabariki. Na kama ukimwambia tutakupigia simu kukupa majibu basi hakikisheni mnampigia na kumpa majibu hata kama ni ya hapana.

4. Kila mmoja wetu ni binadamu hakikisheni mnapofanya usili lugha zenu za mwili (body languages) zisiwe za kumkatisha tamaa mtu anayefanyiwa usili na usimtoe mtu kwenye mstari.

5. Matumizi ya lugha ya kiingereza: hapa inatakiwa mtumie utu na mtambue kuwa si wote ambao wanaofahamu kiingereza wanajua kukiongea vizuri kama wanavyoongea kiswahili, kwa hiyo wapeni vijana muda wanapowajibu maswali.

Mwisho niwaombe tuthamini muda na fedha za vijana wetu ambao bado wanatafuta sehemu za kupatia riziki.
 
pole kijana kwa changamoto unayopitia, ni suala la muda tu, nayo itapita. Ushauri, jitahidi kutafuta hata njia nyingine ya kukuingizia kipato kama huna wakati unasubiri ajira muhimu usichague cha kufanya ilimradi iwe halali na kikubwa usikate tamaa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom