Uchaguzi 2020 Ushauri kwa vyama vyote kuelekea ukingoni mwa uchaguzi: Tupande Uhuru na Haki tukavune Amani na Mshikamano kwa taifa letu

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
8,433
2,000
Mabibi na mabwana heshima kwenu.

Hapa ni ushauri wa bure kwao vyama vyote watia nia kuelekea lala salama katika uchaguzi huu.

Zimekuwapo changamoto nyingi katika kufikisha ujumbe kwa wapiga kura. Pana vyama waziwazi vimekuwa vikibebwa na vyombo vya habari (vya umma na hata vya binafsi hali vingine vikiminywa).

Yote kheri, sera zote kwa hakika zimeshawafikia wapiga kura vilivyo. Hayupo mpiga kura ambaye hadi leo kuwa ati hajui chama gani kina simamia nini.

Hakuna asiyejua kuwa vyama vyote vinasimamia maendeleo. Hakipo chama kisichokuwa na neno maendeleo au mipango ya maendeleo katika sera zake.

Hakuna asiyejua kuwa tofauti ya CCM na vyama vingine ipo kwenye masuala ya "haki na uhuru" wengine wakiita haya kuwa ni "bata."

Kwa vile yote haya yanajulikana vilivyo, ilikuwa ni muda sasa kupeleka ujumbe lengwa unakokosekana na mahali unapohusika.

Tuelekeze sasa kampeni kwa tume na wote wanaohusika na usimamizi wa uchaguzi huu.

Vyama na vipaze sauti ya kutosha sasa kwa mamlaka hizi na hasa tume kama sehemu ya kampeni, kuhitaji amani kwa taifa hili. Kazi hii isiachiwe asasi za dini peke yake.

Wanasema waungwana, "Common sense is not so common to everyone" ila amani itakatokana na uchaguzi utakaokuwa "huru na wa haki."

Chama kitakachojikita kwenye kudai uchaguzi huru na wa haki (free, fair and credible election) kwa hakika kitavuna vilivyo.

Watanzania tunataka amani hali tukijua tutavuna tunachopanda.

"Tupande uhuru na haki katika uchaguzi huu tukavune amani na mshikamano kwa taifa letu."

Tunataka amani na mshikamano kama taifa.

Hayo ni matunda ya haki.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
8,433
2,000
Magufuli, Lissu, Maalim, Membe, Spunda, Mrema, Mbatia nk, tuungane sote kuwataka tume na wote waliopewa mamlaka ya kusimamia uchaguzi huu kuwa tunataka uchaguzi ulio huru na wako.

Mgombea asiyeuona umuhimu wa uchaguzi uliohuru na wa haki, hatufai!

Vivyo hivyo chama kisichouona umuhimu wa uchaguzi uliohuru na wa haki, basi nacho kitakuwa hakitufai!

Amani haidondoki kama ya mvua.
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,461
2,000
Mithali 34:14
Haki huinua Taifa na dhambi ni aibu kwa watu wote

Vile vile Imenenwa kuwa AMANI NI TUNDA LA HAKI
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
8,433
2,000
Mithali 34:14
Haki huinua Taifa na dhambi ni aibu kwa watu wote

Vile vile Imenenwa kuwa AMANI NI TUNDA LA HAKI

Ajabu na kweli kuna mijamaa ya chama fulani likiwamo hili YEHODAYA, yanachukia na kufura kwa hasira yakisikia au kuona ukweli kama huu ukijadiliwa.
 

omujubi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
4,166
2,000
Kweli kabisa.

Nimefuatilia kauli za 'wazalendo', zaidi ya 95% wanasisitiza amani na ni chini ya 5% wanaokumbushia HAKI.
Iko hivi, HAKI ni kitu kinachotakiwa kufanywa/kutolewa na mtu lakini amani huitendi bali inatokea kielelezo kuwa lazima kuwe na inputs zitakazopelekea iwepo.

Wajinga wachache tukijidanganya kuwa amani itaendelea kuwepo bila kutenda haki tutaingia rasmi kwenye vitabu vya historia. 2020 imekaa vibaya sio kwa hapa kwetu tu bali duniani kote.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
8,433
2,000
Chadema mtajuta kusimamisha msaliti wa Nchi Lissu apeperushe bendera ya Chadema Akiwaletea Chadema hata wabunge wawili mkatambike

Comment hii huwa una copy na ku paste au ni ubingwa wa kuikariri na kuinukuu papo?

Naomba nitabiri - "uta post tena comment nyingine kwenye uzi mwingine ambayo ni identical and onto this one."

Au ndiyo kuishiwa na kurokota yale mananihii?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom