Ushauri kwa vyama vya upinzani bila tume huru ya uchaguzi msishiriki uchaguzi, mnahadaiwa na CCM

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,073
Nadhani kwa wenye akili kubwa watakuwa wameelewa kwanini suala la upatikanaji wa tume huru ya uchaguzi linasuasua huku muda wa kufanya uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ukikaribia. Badala ya kuharakisha mchakato CCM inapanga viongozi wapya wa tume ya uchaguzi iliyopo leo kaapishwa mkurugenzi.

Wa tume ya uchaguzi kwa utaratibu ule ule wa kuteuliwa na mwenyekiti ambaye chama chake kitashiriki uchaguzi. Binafsi niliamini mpaka sasa kama CCM ina dhamira ya dhati ya kupata tume huru ya uchaguzi. Ingekuwa na nia hiyo basi muswada ungekuwa umefika bungeni kipitishwa na baadhi ya marekebisho ya sheria kanuni yafanyike na kisha rais kuusaini ili tume huru ya uchaguzi ianze kazi..

Ushauri kwa vyama vya siasa, kumbukeni suala la tume huru sio la CCM hivyo kuiachia CCM iharakishe upatikanaji wa Tume huru ni kichekesho kwani tume ya uchaguzi iliyopo ndio siri ya ushindi wa CCM kwa miaka yote hivyo CCM haiwezi kuhangaika na tume huru kwani itakuwa imejikaanga na mafuta yake hivyo nguvu kubwa ya ndani inahitajika kinyume chake bila tume huru hakuna uchaguzi.
 
Back
Top Bottom