Ushauri kwa Viongozi wa Vyama vya Upinzani juu ya waliounga juhudi na wametoswa Kura za Maoni

famicho

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
2,192
2,827
Habari wanaJF,

Kuna hawa akina Lijuakali na wenzake ambao wameunga Juhudi kwa kebehi, dharau na Tambo nyingi juu ya Vyama vyao ambavyo viliwakuza hadi kuonekana watu kwa jamii lakini malipo yao yakawa hivyo.

Baada ya kuliwa vichwa wengi wao wametamani kurudi walikotoka (Nina uhakika na hili), lakini mkakati wa Vyama vya Upinzani ni kutowapokea tena by any means.

Binafsi si mchangiaji Sana wa masuala ya siasa zaidi ya kuwa msomaji Ila katika hili napenda kushauri yafuatayo;

1. Wapokeeni ila wawe wanachama tu wakawaida, muwaambie mnawaweka kwenye uangalizi Kwanza.
Sababu, mkiwaacha wabakie kule wanaweza tumika kama silaha za kuwapiga nyie kwani wanajua Siri zenu nyingi ingawa ni za sebleni

2. Mshiwahusishe na masuala yoyote juu ya mipango yenu ya ushindi kwani bado hawaeleweki

3. Mkiwapokea ndo inakuwa mwisho wao wa siasa kwani hawatoaminika tena(wanakufa kisiasa)

4. Watumieni kipindi baada ya uchaguzi muwadampo.

Kwenye maboresho, ushauri jazieni ili kuuweka ushauri huu vizuri.

Nawasilisha
 
Embu jiulize kwanini walienda sisiem?
Nadhani jibu ni rahisi tu, kusaka tonge si ndiyo?

Sasa wakirudi chadema bila kuambulia nyadhifa wanaweza wakakaa?

Hao wanaitwa wanasiasa maslahi, ni sawa na wanajeahi mamluki ama wachezaji wa mpira ambao huweza chezea timu 'A' na kesho timu hasimu 'B' bila soni macho yakiwa makavu kabisa, hawana ushabiki wa timu, wao ni maslahi mbele.
Hivi mwanamke malaya hufuata penzi kwa danga au mfukowe?

Nyie acheni jamani!
 
Back
Top Bottom