Ushauri kwa viongozi wa Umma kuepuka kutumbuliwa na Rais Samia Suluhu

Samia anaakili na ni mstarabu wewe,hawezi kamwe kufata ujinga wa magu,magu alikuwa mfano mbaya katika jamii ya wastaarabu
Siongelei majungu na sina muda nayo naongelea performance output ya kuhudumia wananchi walio wengi ambao ndio wapiga kura serikali zilizopita zilikuwa za viongozi sio za wananchi zilikuwa za akina una unanijua mimi nani mimi ni shemeji au hawara na bosi nk shenzi type kura upewe na wanyonge halafu uwatishie nyau .Magufuli aliua hiyo na isijirudie .Mama Samia hili usikubali kuwa serikali iwe ya viongozi iwe ya wakipa kodi ya wanananchi sio wananchi utapata shida
 
Rais Samia Suluhu Hassan atafanya jambo jema kwa wananchi kama ataendeleza tabia aliyokataa Magufuli ya kumrundikia vyeo chungu nzima mtu mmoja! Huko nyuma mtu mmoja aliweza kuhodhi vyeo hata kumi ili mradi walikuwa kipenzi cha mtawala. Magufuli alifuta kabisa tabia hiyo na ikawa cheo kimoja kwa mtu mmoja, hivyo Rais Samia aendeleze utamaduni huo.

Rais pia aachane na hulka ya kuteua watu kwa kigezo cha kujipendekeza na kusifia badala ya kufuata weledi wa wahusika. Huko nyuma walioimba nyimbo za kumsifia mkuu ndio walionekana bora kuliko watendaji wengine na ndio hapo likazuka tabaka la wateuliwa hasa MaDC na MaRC ambao walikuwa hawana heshima kwa wakubwa zao isipokuwa Rais mwenyewe na hii ikapelekea hawa wateule kuwa Miungu watu kwenye sehemu zao za kazi. Mifano ipo wazi sina haja ya kuorodhesha hapa!!
Tabia hii lazima ikomeshwe; MaDC na MaRC wawajibike kwanza kwa Waziri wa Serikali za mita na Waziri Mkuu kabla ya kukimbilia kwa Rais, hili litampunguzia kazi Rais ambazo wasaidizi wake wanatakiwa kuzishuhulikia.
 
ali
Na kemeeni rushwa!
Toka tupate Uhuru kila Kiongozi wa nchi amekuwa akikemea rushwa bila mafanikio hata ya kupunguza tu achilia mbali kukomesha kabisa mpaka sasa imekuwa wimbo lakini tatizo liko palepale. Hao wanaokemea rushwa ndo wanaodai (hawaombi) na kupokea kwa kwenda mbele bila wasiwasi wowote kwa sababu wamatengeneza njia salama za kupokea bila kukamatwa na wakikamatwa kinga imara zimetayarishwa ndo maana wanaokamatwa ni vidagaa wanaopokea rushwa ndogondogo ambazo hata wenyewe haziwatoshi au wale wanaotoa chini ya viwango vinavyodaiwa. Karibuni tu Twaweza kila mwaka walikuwa wanatoa tathimini ya mwenendo wa vita dhidi ya Rushwa katika taarifa ya mwisho kabla hawajafungiwa walisema Rushwa kwa ujumla imepungua lakini vinara bado wanaongoza Polisi wakifuatiwa na Mahakama wakifuatiwa na Afya lakini sote tunajua kilichowapata. Taasisi yakupambana na Rushwa ilianzishwa wakati mbalimbali lakini mafanikio yake labda kubadilisha jina mara kuwa mara mpaka Wafanyakazi wake wachache nao wakajiingiza kudai Rushwa. Tatizo, kama kawaida yetu Watanzania, tunaangalia tulipoangukia badala ya tulipojikwaa ndo maana tunaendelea kujikwaa Awamu baada ya Awamu. Wahusika wajiulize nani wanaopokea Rushwa na kwa nini, nani wanatoa na kwa nini?
 
Atakayefanya kazi kwa speed ya JK ametoboa
huko sahihi migomo kibao kila kona ya madaktari watu wanakufa kwa spidi ya Kikwete haikubaliki

Kikwete aliendekeza mgomo wa madaktari wauaji kwa kisingizio cha Demokrasia Nilipoteza shangazi yangu kipindi cha mgomo wa madaktari kipindi cha Kikwete na upole wake na kijifanya kwake kuwa anataka demokrasia ya Magharibi siji kumsaau loo Kikwete kwenda zako huko loo
 
Muda utasema...
Ila tunamtakia kila la heri kwenye utendaji
Wake.....wengine sahvi tumeachagua kuwa
Neutral

Ova
 
Viongozi wa umma nawapa ushauri wa bure kuepuka kutumbuliwa na Raisi Mpya Samia

1. Spidi mliyokuwa nayo kipindi cha Rais Magufuli msiache mkiacha wananchi watatungua kilio kumlilia kumkumbuka Magufuli kuwashtaki kwa Raisi mpya kuwa angekuwepo tungepata huduma kwa wakati na spidi nk hivyo Raisi atawachukulia kama mnamhujumu au kumdharau kwa kuwa ni mwanamke lazima atawatumbua.

2. Angalieni foleni zitakazo huduma kwenye taasisi zenu ukiona foleni ndefu au mafaili ya kero mengi tafuta ufumbuzi haraka kabla wananchi hawajampigia yowe Raisi akutumbue.

Kila moja awe Magufuli kwa spidi ileile kutatua kero bila kusubiri Raisi aje au apelekewekero na wananchi.Utatumbuliwa.Uwe na antenna zako mwenyewe kama mkuu wa taasisi au idara au wilaya au mko au wizara au shiriki au kitengo kujua kuna kero gani zipo za kukera wanamchi zinazotakiwa zitatuliwe na uzitafutie ufumbuzi haraka kama huna mamlaka andika shauri upesi mbele kwa waluo juu yako kwa maandishi ili likibuma usije kuwa mbuzi wa kagara kuwa ohh sijui sheria za bunge sijui taratibu ndivyo zinasema hivi nk wakati zinaumiza wananchi peleka ushauri mbele haraka.

3. Heshimu Rais Mpya hata uwe mjuaji vipi Mama Samia ndie Rais

4. Uwe mbunifu kutatua kero na kubana matumizi na kubuni njia za kuongeza mapato ya serikali kwenye eneo lako biña kuumiza wananchi wanyonge ambao ndio majority wapiga kura.Mfano halmashauri wawe wabunifu wa miradi miongeza ajira na mapato na kupunguza kodi korofi kwa wanyonge.

5. Kila mkuu awaze je mimi nitapunguzaje kero za wanyonge na kuongeza mapato ya serikali bila kuumiza mnyonge na kuwe na weekly report ya hilo.

6. Taasisi zote zifanye kazi kama timu moja ya serikali wasitupiane mpira kukiwa kuna mgongano watafute solution pamoja sio ohh mimi hili halinihusu ni la fulani kwangu nimemeliza.

Wengine ongezeni nimeitwa kuna kikao nitaandika mengine baadaye.
acha kutisha viongozi wetu kila zama na kitabu chake,unataka kusema mzee baba hakuongeza salary na madaraja ishu kwa watumishi na hao viongozi waendeleze moto uleule? mh amirat wetu hapangiwi cha kufanya ye mwenyewe anajua na atapangua mdogo mdogo hadi ngosha members waishe,chapa kazi mama niko bega kwa bega na wewe ,japo chama changu pendwa ni mlengo wa kushoto,hainizuii kukusapoti,ombi binafsi kwako mama ajira ya 2014 tunasotea madaraja mwaka wa 7 tuhurumie familia zetu kubwa maisha yametukaba madeni hayaishi,salary advance ndo inatufuta machozi
 
Viongozi wa umma nawapa ushauri wa bure kuepuka kutumbuliwa na Raisi Mpya Samia

1. Spidi mliyokuwa nayo kipindi cha Rais Magufuli msiache mkiacha wananchi watatungua kilio kumlilia kumkumbuka Magufuli kuwashtaki kwa Raisi mpya kuwa angekuwepo tungepata huduma kwa wakati na spidi nk hivyo Raisi atawachukulia kama mnamhujumu au kumdharau kwa kuwa ni mwanamke lazima atawatumbua.

2. Angalieni foleni zitakazo huduma kwenye taasisi zenu ukiona foleni ndefu au mafaili ya kero mengi tafuta ufumbuzi haraka kabla wananchi hawajampigia yowe Raisi akutumbue.

Kila moja awe Magufuli kwa spidi ileile kutatua kero bila kusubiri Raisi aje au apelekewekero na wananchi.Utatumbuliwa.Uwe na antenna zako mwenyewe kama mkuu wa taasisi au idara au wilaya au mko au wizara au shiriki au kitengo kujua kuna kero gani zipo za kukera wanamchi zinazotakiwa zitatuliwe na uzitafutie ufumbuzi haraka kama huna mamlaka andika shauri upesi mbele kwa waluo juu yako kwa maandishi ili likibuma usije kuwa mbuzi wa kagara kuwa ohh sijui sheria za bunge sijui taratibu ndivyo zinasema hivi nk wakati zinaumiza wananchi peleka ushauri mbele haraka.

3. Heshimu Rais Mpya hata uwe mjuaji vipi Mama Samia ndie Rais

4. Uwe mbunifu kutatua kero na kubana matumizi na kubuni njia za kuongeza mapato ya serikali kwenye eneo lako biña kuumiza wananchi wanyonge ambao ndio majority wapiga kura.Mfano halmashauri wawe wabunifu wa miradi miongeza ajira na mapato na kupunguza kodi korofi kwa wanyonge.

5. Kila mkuu awaze je mimi nitapunguzaje kero za wanyonge na kuongeza mapato ya serikali bila kuumiza mnyonge na kuwe na weekly report ya hilo.

6. Taasisi zote zifanye kazi kama timu moja ya serikali wasitupiane mpira kukiwa kuna mgongano watafute solution pamoja sio ohh mimi hili halinihusu ni la fulani kwangu nimemeliza.

Wengine ongezeni nimeitwa kuna kikao nitaandika mengine baadaye.
Pisikali kama pisikali mnashauriana utopolo wenu,mataga hamjawahi kua na akili
 
Back
Top Bottom