Ushauri kwa vijana wasio na ajira

SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
4,040
8,888
Kijana usio na ajira zingatia haya yatakusaidia na yametusaidia kaka zako:

1. Ukiwa huna ajira usikatae kazi yoyote halali, hata kama mshahara ni mdogo anza na hiyo wakati unatafuta kazi ya ndoto zako.

2. Tumia vizuri mitandao ya kijamii katika kufanikisha ndoto zako. Achana na mitandao ya umbea, majigambo, ngono n.k
Tumia bando lako kwa faida.

3. Usione aibu kurudi nyumbani kwenu (kurudisha mpira kwa kipa) wakati unajipanga na mambo yapo ovyo. Hata kama una kiasi kidogo rudi nacho nyumbani kitakusaidia nauli ya kwenda kwenye interview au hata kufungua biashara ndogo hapo nyumbani.

Wazazi na jamii inajua jinsi ajira zilivyo ngumu ukirudi kwenu watakuelewa tu kuliko kuendelea kutia aibu mjini huku ukijiita mpambanaji. Sasa hivi hata kazi za ulinzi hamna, rudi kwenu usione aibu.

Pia achana na story za mitandaoni kuwa kuondoka home ndio uanaume. Ondoka home ukijua unaenda wapi. Hii ni karne ya 21. Zamani ukija dar tu hata kariakoo sokoni utalala ila si sasa hivi, wenye nyumba wanataka kodo+umeme+maji n.K.

4. Kujitolea ni jambo la msingi ili kupata uzoefu. Marafiki wengi na michongo mingi utaipata ukiwa unajitolea.

5. Epuka ulevi, ngono na matumizi mabaya ya fedha.

6. Usiache kusoma neno la mungu maombi na kuhudhuria ibada. Ukosefu wa ajira unaleta stress nyingi na shetani anaweza kutumia huo mwanya akakupa hata mawazo ya kujiua.

7. Usikate tamaa songa mbele hata kama umepigika kiasi gani.

Mungu awabariki!
 
Nifikiri...

Nidhamu ya fedha na watu wa rika lote, juhudi/bidii katika kila jambo ama kazi ambayo kijana anaifanya, kusali na kua mwenye hofu ya Mungu yaweza mfikisha kijana mbali zaidi
 
Nifikiri.....
Nidhamu ya fedha na watu wa rika lote, juhudi/bidii katika kila jambo ama kazi ambayo kijana anaifanya, kusali na kua mwenye hofu ya Mungu yaweza mfikisha kijana mbali zaidi
Kweli mkuu
 
Back
Top Bottom