Ushauri kwa UKAWA kuelekea 2020 kuhusu stahiki,haki na maslahi ya watumishi wa umma


S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Messages
31,906
Likes
65,609
Points
280
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2012
31,906 65,609 280
UKAWA,watumishi wa umma ni kundi ambalo mkilitumia vizuri mnaweza kuvuna kura nyingi sana mwaka 2020 maana hii kundi lina matatizo mengi ambayo yanatokana na kukosekana kwa sera na sheria rafiki kwa kundi hili.

Mfano mzuri ni hili swala linalohusu ulipaji wa malimbikizo ya mishahara kwa wafanyakazi baada ya mtumishi husika kupandishwa cheo.

Inashangaza sana mtumishi wa umma anapandishwa cheo kwa mfano mwezi wa sita lakini mshahara mpya unaotokana yeye kupanda cheo anakuja kuupata mwezi December wa mwaka husika yaani miezi sita baadae.

Kama haitoshi na kibaya zaidi,malimbikizo yake hayo ya miezi sita wala hajua atayapata lini na sidhani hata kama kuna sheria inayomlinda katika hili zaidi ya kusubiri uamuzi au huruma ya serikali kwamba mwezi huu tumlipe mtumishi wa Taasisi "X" na mwezi ujao tumlipe mtumishi wa Taasisi "Y". Kwakweli yataka moyo sana.

Kutokana na tatizo hili kuwa sugu serikalini, nawashauri viongozi wa UKAWA mliingize katika ilani yenu ya mwaka 2020 kwa kuahidi kulitungia sera na sheria maalumu itakayosaidia kupambana na tatizo hili.

Nawashauri mje na sheria itakayotamka kuwa mtumishi yeyote atakaecheleweshewa mshahara wake pasipo sababu za msingi,basi serikali imlipe mtumishi huyo mshahara wake pamoja na penalty ya asilimia 20 ya basic salary kwa kila mwezi ambao hakupata mshahara wake kwa wakati.

Hata hivyo,kwa kuanza sheria inaweza kutoa grace period ya miezi mitatu tangu mtumishi apate promotion na baada ya miezi hiyo mitatu kupita pasipo mtumishi husika kulipwa mshahara wake mpya, sheria itamke moja kwa moja kuwa sasa mtumishi huyo atapaswa kulipwa mshahara anao dai pamoja na riba ya asilimia 20 ya basic salary yake.

Naamini sheria hii itailazimisha serikali kuepuka hasara ya kulipa watumishi wake na hivyo kuifanya iwe makini kulipa watumishi wake kwa wakati.

Au tunaweza kuna na sheria inayotamka kuwa mtumishi atapaswa kuanza kulipwa mshahara wake mpya pamoja na malimbikizo yake ndani ya muda fulani tangu apandishwe cheo na muda huo ukipita serikali itapaswa kumlipa huo mshahara na penalty juu.

Sometimes huwa najiuliza hivi matatizo ya aina hii yako pia katika nchi nyingine duniani na ni kwanini wahusika wasiende kujifunza kutoka katika mataifa yasiyo na tatizo la aina hii ili kumaliza kabisa kero hii kama wao kweli wameshindwa kulitatua bila ya msaada wa watu wengine?Je,ni kweli tatizo hili limewashinda kiasi hiki au tu wamekosa dhamira?

Pia, sheria iangalie namna ya kuwabana watendaji wanaosababisha kuwepo malimbikizo hayo maana wakati mwingine matatizo hayo huenda yanasababishwa na uzembe wa watu wachache na ikiwezekana adhabu iwe ni mtumishi wa aina hii kukatwa mshara ikithibitika amezembea na adhabu hii iwe ni ya kisheria.

Kama serikali inatoza penalty wananchi wake mfano kwa kuchelewa kulipa kiwanja ni kwanini na yenyewe isitozwe penalty pale inapochelewa kulipa watumishi wake kwa wakati?

Vile vile fanyeni utafiti kuhusu hii habari isiyo rasimi kuwa mtumishi anapotaka kujiendeleza kwa kiwango cha kupata shahada ya kwanza,basi atalazimika kuomba likizo ya bila malipo.

Nawashauri iwapo mtabaini kuna ukweli juu ya jambo hili,basi 2020 njooni na sera ya kufuta kabisa utaratibu huu na badala yake mtoe ahadi ya serikali kuendelea kugharamia watumishi wake wanaojiendeleza na pia watumishi waruhusiwe kuomba mikopo kutoka bodi ya mikopo ya Elimu ya juu.

Yangu hi hayo tu kwa leo.
 
M

mzalendo15

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Messages
1,367
Likes
1,005
Points
280
M

mzalendo15

JF-Expert Member
Joined Sep 16, 2015
1,367 1,005 280
Nyongeza Elimu bure mpaka vyuo vikuu itawapa kura nyingi sana.
Kwani kuna watumishi ambao wanategemea kujiendeleza Elimu ya juu ilihali kipato chao ni kidogo hivyo kushindwa kumudu kulipa ada.
 
kipara kipya

kipara kipya

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2016
Messages
5,444
Likes
5,452
Points
280
kipara kipya

kipara kipya

JF-Expert Member
Joined May 2, 2016
5,444 5,452 280
Wazo zuri kwetu,lakini sehemu nzuri ya kupangia mashambulizi sisi tumepakimbia,tena kisa mwanamke tu!
 

Forum statistics

Threads 1,238,682
Members 476,113
Posts 29,326,400