Ushauri kwa tusiokuwa na ajira

MissM4C

JF-Expert Member
Aug 31, 2012
1,740
1,004
Wakuu nawasalimu.....

Najua Hali ni tete kwa kila ajiitae msomi (graduate kuanzia 2015 na hadi wa mwaka Jana, hakuna ajira, jamaa wanabadilisha agenda kila uchao leo madawa kesho akina james delicious hakuna anaeongelea janga la un-employment, watoto wa maskini ambao wazazi wao hawana mitaji ya kuwasaidia wanalia, imewabidi walaminate vyeti na kuvificha kwenye makabati au chini ya magodoro,,,,, nimewaza na kuwazua nikana niwashirikishe katika hili kama litawafaa

1. KUUNGANISHA NGUVU NA KUJIAJIRI

Mkiwa watano kila mmoja akatafuta Kiasi cha milioni 1, mki-sum up mna m5, kama ni walimu mnaenda vijijini(atleast mini centres) mnakodi au anajenga Banda la tuisheni 24*7 mnapiga piga haswa lazima mtoke

Kama ni Madaktari CO/MD mkiunganisha nguvu mkawa na takribani 10M mkaenda maeneo kama mlimba, mpanda, vawa na mengine amvayo yametelekezwa na serikali kwa huduma za Afya mnatoka

Kodi jengo usjali hata la tope, kwa miezi 6 weka reception yenye bench la mabanzi, tenga cube ya dawa, tia ngazi na DAWA zile essential tu kisha tenganisha pawe na consultation room, injection room na kachumba kamoja au viwili vya bed rest(me/ke patient) na dressing room

Anza mdogo mdogo lazima utoke t maana vichwa ni vingi

Pesa ya kuunganisha nguvu itatoka wapi? uza asset shamba la ukoo, kopa Benki au kwa mtu anayekuamini weka Dhamana hata vyeti

Pia unaweza andaa business proposal ukawapa akina mengi, manji, au mbunge wako akiikubali ndo pa kutokea


Kama si kujiajiri wazo la pili ni

2. TUKOMAE KUTAFUTA FURSA NJE.

Nchi kama Rwanda, Kenya na Uganda bado wanThamini sana taaluma za watu, cha kufanya tafuta passport japo tempo ibuka Nchi husika kwa kisingizo cha mwaliko, tafuta leseni ya kufanya kazi huko(nilipita na inategemea) na lazima uwe na status au recommendation letter toka nchi yako.... ukipewa anza kazi hata kama ni private. East Africa haibaguani katika employment opportunities

Note ;- Lazima uwe na mwenyeji nchi husika

Bila hivi tutakufa, ajira zitatoka 2019 ili muwape tena 2020 na hata mkipata no salary increment na makato kibao ikiwemo HESLB
mi nimestuka soon nitaiga bongo.

Najua it is easier said than done! Ila tukiweka nia tuantoboa.

Tafakuri Njema Wakuu
 
Njooni mjiiunge na helping hands international, au mradi Wa Kuku 07696359670
 
Shukuruni mungu kuw mmekosa nafasi ya kuwa watumwa hivo jalibuni kujiajil hata kama ni katika ishu ambayo unahs utadhalaulika katika jamii,sio kila ishu itahtaj mtaji mkubwa kwahyo acheni kutoa kizingzio cha mtaj

Mimi nilmaliza chuo kikuu nikakora ajila nkajiajil then watu walipoona juhudi zangu wakaniwezesha zaid kipesa,

NB:KUKOSA AJILA SIO KILEMA CHA KUKUFANYA UISHI MAISHA YA HUZUNI,LAWAMA NA KUTEGEMEA KUONEWA HURUMA NA JAMII
Umenena vyema mkuu, kuna jamaa alisoma law akaamua akajiajiri kufuga nguruwe yuko mbali na amefungua zahanati huko ulaya ya kilosa inaitwa mico-mzuma akikusimulia huwezi amini
 
Back
Top Bottom