Ushauri kwa TRA: Biashara nyingi rasmi zitaendelea kufungwa

Basically sio sawa kulalamika kwa kukata tamaa kwamba hali haiwezi kuwa nzuri kwa kuwa kuna nyakati hali ni mbaya.

Msingi wa biashara ni kuzalisha na kupata faida. Kama ambavyo mfanyakazi anakwenda kazini mwezi mzima na kwa kutumia nguvu yake au akili ndio mwisho wa mwezi anapata ujira.

TRA ni mamlaka ya kukusanya mapato ya serikali katika biashara ambazo zinatoa huduma au kuuza bidhaa.

Viwango vya makadirio ya kodi vinaweza kuwa sio sawa kwa biashara moja kwenda biashara nyingine.

Na tukiwa wakweli sio wananchi wote wana biashara kubwa za kuweza kumudu kulipia tax consultant ili asimamie hesabu na biashara/kampuni.

Mabenki yana idara za
mikopo midogo zaidi (micro loans)
Mikopo midogo (small loans)
Mikopo ya kati (medium loans)

Sasa iko haja maafisa wetu TRA wange-specialize kwenye ku-deal na scale za biashara.

Na sio sifa kumtoza mfanyabiashara kodi kubwa ambayo inaweza kuathiri "operating capital expenses"

Operating expense ndio damu ya biashara na faida ikipatikana ni haki kabisa TRA kuchukua chake.

Makadirio ya mapato, ndani ya miezi 3 mtu alipe kwa new business ni muda mfupi sana. Ni sawa na juajiri new staff then unataka output yake iwe sawa na experienced staff kwenye deliverables.

Au ni sawa kuna mtu anafanya biashara ya kilimo cha mchicha anavuna in 3 weeks unata kodi ya mauzo iwe sawa na mkulima wa matunda ya embe ambapo inachukua miaka 3 hadi mitano kupata matunda; na huyu wa miaka 3-5 anatakiwa kufanya palizi, kuweka mbolea na Ulinzi ili wezi wasikwibe au wachoma moto mashamba wasipite.

Kamishna Jenerali wa TRA ni PhD holder; tunaomba ujue biashara zina operate kwa law of relativity.

Sio sawa hata kidogo kuwa na equal treatment kwa biashara.

Mwisho, tuishi kidugu, tujadiliane maana kesho muembe ukizaa matunda yake tutavuna kwa muda mrefu na TRA atapata tu na huenda kama shamba ni kubwa tunaweza kupata kuwanda cha juice.

Ila tuki-suffocate working capital ili tu kupata kodi; sio sawa maana biashara hii ikifa, sio TRA anakosA, wenye kupangisha biashara wanakosa mpangaji, TANESCO anakosa mlipa ankara, Maji anakosa mlipa ankara, kampuni za ulinzi wanakosa;

Bado tuna imani na serikali kufanya facilitative role biashara zi-bloom ili mwenye biashara apate na TRA na sekta zingine wapate.

Tusifikie pahala biashara hasa ndogo na za kati directors wasifanye major role ya ku-strategize kukuza biashara wabaki wanafikiria natoa wapi kodi kwa kumega working capital.

Kila la kheri kwenye kuijenga Tanzania
 
Ushauri kwa TRA:

1. Wajitahidi kuwa na kipaumbele indirect taxes mipakani,bandari na viwandani.

2. Usawa kukusanya kodi iwe ni sheria kutumia efd/VAT kwa biashara bidhaa aina fulani.

3. Rais aombwe atoe ufafanuzi tafsiri, mipaka, ukomo mfanyabiashara mdogo

4. Itumike busara kudai madeni ya zamani 2010. Mfumo wa awali manual records mapungufu nyaraka anabeba adhabu mlipa kodi kulipa upya. Tena kwa agency notice pin akaunt ya bank.

5. Undeni team ya wataalam kupitia sheria na kanuni za kodi. Baadhi ya sheria mfano ukiuza na kununua dai na toa risiti hazitekelezeki katika baadhi ya bidhaa na mazingira ya Watanzania wengi 80%.
Namba tano inawezekana tuu kwa kuamuru MACHINGA wote waondoke barabarani.
 
Ushauri kwa TRA:

1. Wajitahidi kuwa na kipaumbele indirect taxes mipakani,bandari na viwandani.

2. Usawa kukusanya kodi iwe ni sheria kutumia efd/VAT kwa biashara bidhaa aina fulani.

3. Rais aombwe atoe ufafanuzi tafsiri, mipaka, ukomo mfanyabiashara mdogo

4. Itumike busara kudai madeni ya zamani 2010. Mfumo wa awali manual records mapungufu nyaraka anabeba adhabu mlipa kodi kulipa upya. Tena kwa agency notice pin akaunt ya bank.

5. Undeni team ya wataalam kupitia sheria na kanuni za kodi. Baadhi ya sheria mfano ukiuza na kununua dai na toa risiti hazitekelezeki katika baadhi ya bidhaa na mazingira ya Watanzania wengi 80%.
Kwa matamko ya leo tiari hiyo kauli imeshaatengeneza panic kwa wafanyabiashara , bishara si hemu ya kutengenezea tahruki ni sehem inayotakiwa ikwe natural growth na iwe harmonized na watu
 
Suala la efd ndio mtihani kabisa! Nimekwenda kuupdate mashine yangu mwisho was cku nikaambiwa kampuni niliyonunua wakayi huo imeshafungwa au haipo sasa naambiwa ninunue mashine nyingine ambayo ni sh 590000! Sasa najiuliza kosa langu ni lipi? Kama kampuni ishafungwa kwa nini kusitafutwe utaratibu wa kuupdate? Maana mashine yangu ni nzima ina maana nukaitupe je c kunionea huku? Naomba msaada kwa yeyote atakayenipa ufumbuzi maana usawa huu 590000 na biashara yenyewe ilivyo ngumu ni MTIHANI MKUBWA SANA KWANGU
 
Back
Top Bottom