Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 46,991
- 144,322
Kupitia mtandao huu, napenda nitoe wazo/ushauri kwa Benki za kibiashara, hasa Benki za NMB na CRDB, benki ambazo zinaonekana kushindana kuvutia watumishi wa umma kupitishia mishahara yao katika benki hizo.
Kwa mfano,hizi benki mbili kwa sasa zote zimeanzisha huduma ya salary advance, huduma ambayo licha ya kuwa ni ya kibiashara, bila shaka ina lengo lingine la kuvuti watumishi wa umma kupitishia mishahara yao katika Benki hizo.
Si hivyo tu, hivi sasa mtumishi anaetaka mkopo katika mojawapo ya mabenki haya, moja ya shariti ni mshahara wa mtumishi husika ni lazima kwanza upite katika benki yao na kama haupiti, basi utatakiwa kubadili akaunti ya mshahara kuweza mshahara upite katika benki uliyoombea mkopo.
Leo hii napenda niwape wazo la kibiashara ambalo litawezekana iwapo Benki hizi na Taasisi za serikali(hapa kama waajiri) watakaa pamoja na kukubaliana na kisha kuwashirikisha wafanyakazi.
Nachotaka kusema ni nini hasa?
Kwakuwa kuna baadhi ya Idara na Taasisi za serikali ambazo hutoa malipo(posho kwa kila mwezi) kwa wafanyakazi wake mbali na mishahara, lakini malipo hayo mara nyingi hutoka kwa kuchelewa, mabenki haya yanaweza kutoa malipo hayo kila mwezi katika tarehe iliyokusudiwa ila kwa shariti kwamba mshahara na malipo mengine yote ya mtumishi husika lazima yapite katika benki hiyo. Benki husika itakata fedha fedha zake pale mwajiri anapowasilisha malipo ya wafanyakazi wake katik benki hiyo.
Kinachotakiwa hapa ni mabenki haya kukaa chini na waajiri na wakisha kukubaliana, wanashirikisha wafanyakazi ambapo benki zitaanza kushawishi wafanyakazi kujiunga na benki yao na kufaidika na huduma hiyo hasa kwa waajiriwa wapya na wale watakaokuwa teyari kubadili account zao za mishahara(kwa wale ambao teyari ni waajiriwa).
Ulkweli ni kwamba, hela anayopata katika tarehe ya kuelewaka kila mwezi, ni rahisi kuipangia mipango na matumizi kwani inakuwa ni ya uhakika bila kujali ni ndogo au kubwa mradi unaipata katika tarehe ya kueleweka.
Na leo naomba niipongeze serikali ya Marehemu Magufuli kwa kuwa consistency katika tarehe ya kulipa mishahara ya watumishi wa umma kwani katika hili, wamejitahidi sana na hakika wanastahili pongezi ingawa kwa miaka sita mshahara umebaki ni ule ule(holi ndio tatizo).
Nitoe wito pia kwa Mama Samia kusimamia na kuendeleza utaratibu huu wa kuwa consistency katika tarehe ya kulipa mishahara ya watumishi wa umma kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake, Marehemu Magufuli.
Hivyo, nashauri mabenki kutazama fursa hii kwa lengo la kusaidia watumishi husika kupata malipo yao katika tarehe ile ile kila mwezi na pia mabenki husika nayo kupata faida kwani mtumishi huyu atapoenda kuchukua fedha zake iwe ni kupitia ATM au ndani ya benki, atatozwa gharama na hapo benki nayo itakuwa imefaidika pia.
Vile vile, Vyuo Vikuu na Bodi ya Mikopo(HESLB), wanaweza kufanya jambo kama hili hasa kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanaofungua akaunti za kupitishia mikopo yao mara wanapowasili vyuoni kuanza masomo.
Nawaachia wahusika.