Ushauri kwa serikali: Wenye nyumba za kupangisha walipe kodi ya mapato

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,359
692
Kwa miaka mingi sasa wananchi wengi na hasa vigogo wa CCM na serikali wamejikita ktk biashara ya nyumba za kupangisha na wanawanyonga kweli wapangaji. Cha kusikitisha ni kwamba watu hawa wenye majumba hawalipii kodi kipato hicho wanacho pata kutokana na tozo la pango.

Ushauri wangu kwa serikali ni kwamba badala ya kumbebesha mzigo mkubwa wa kodi mfayakazi, basi na nyumba zote zinazopangishwa zisajiliwe na serkali za mtaa na hapo wenye nyumba lazima walipe kodi ya mapato kwani ni biashara hiyo wanafanya.

Hakuna suala la kusema ni vigumu kusajili wakati serikali za mitaa zipo na viongozi wa mitaa wananjua ni numba ipi inapangishwa na ipi anaishi mwenyewe.

Inasikitisha kuona kwa miaka 40 iliyopita bado chanzo hiki cha mapato serikali ya CCM haija kiona au vigogo wa CCM ndo wanaofaidika na ukwepaji kodi huu??
 
Mbona walioko ughaibuni hamtoi mawazo yenu kuhusu hoja hii? Je, huko wapangisha nyumba hawalipi kodo pia?
 
Umesikia wapi serikali itajiwekea utaratibu unaowabana wao wenyewe? Serikali nzuri za kifisadi ni makini kuhakikisha sheria yoyote inayotendewa kazi (achilia mbali kutungwa) inawanufaisha wao walioko juu kwanza na kuwa-control wananchi wa kawaida. Makali yoyote lazimayawape mgongo wao. Ndio maana wamachinga wanashughulishwa sana kwa ajili ya shilingi mia kwa kuwa wanaingilia mapato ya shughuli za wakubwa mitaani kiasi kwamba watu hawaendi madukani ambako ndio njia nyepesi ya wakubwa kupata keki zao.

Sana sana wenye nyumba za mgongo wa tembo na mbavu za mbwa ndio watatungiwa sheria kuhakikisha wanalipia vibanda vyao TRA. Sasa wameanza kuchunuza hizo mbavu za mbwa ndani yake kuna nini wakadirie kuvuna zaidi. Wamegundua kwamba mbavu zingine ni ndananya toto tu, ndani yake mmmm!

Ndio maana kila kiongozi mpya ni lazima ahakikishe maslahi ya anayemtangulia yanalindwa na ndio chanzo cha chaind leadership style za mtu mweusi. Ukitaka kuwa kiongozi ni lazima upate baraka za aliyekutangulia.
 
Mbona kodi zanazohusiana na nyumba zipo? Kodi ya majengo, ardhi ilipojengwa nyumba, nk?. Pamoja na hayo gharama za viwanja na ujenzi zimepanda sana. Mimi nafikiri serikali ifute hizi kodi ili rent zishuke na watu wanaotake kuwekeza kwenye ujenzi wa nyumba wahamasike kujenga. Kwani hamuoni kwamba wakiongeza kodi atakayeumia ni mpangaji? Ni maoni yangu msininyonge
 
Mbona walioko ughaibuni hamtoi mawazo yenu kuhusu hoja hii? Je, huko wapangisha nyumba hawalipi kodo pia?

nijuavyo mimi kwa UK mwenye nyumba binafsi hatozwi kodi yoyote kutokana na pango analochaji,ila analipa council tax kwa ajili ya huduma kama kuzoa taka,kufagiliwa barabara/mitaa na vitu kama hivyo.
ila kuna estate agent ambao wanapangisha nyumba nafikiri hawa wanalipa kodi kama biashara yoyote ile.
 
FYI . Nyumba za kupangisha ni subject to VAT of 18% na walipaji ni hao hao wapangaji na sio wenye nyumba zao. Walala hoi tuna taabu nyingi mbaya.
 
Back
Top Bottom