Ushauri kwa Serikali: Nashauri Serikali iwanyang'anye passport za kusafiria wale wote waliotukana, kudhihaki na kumsema vibaya Rais wetu

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
5,975
7,731
Kwako serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Mimi ni kijana mzalendo, niliyepata mafunzo ya kijeshi nikafundishwa kupenda taifa letu, nikafundishwa kulinda upendo na amani ya nchi yetu.

Ninao uchungu mkubwa juu taifa langu. Nimekuwa nikikerwa sana juu ya ndugu zetu wengine ni viongozi wale wanaoishi ughaibuni.

Hawa mabwana wamekuwa wakitukana, kudhihaki na kumdharau sana Rais wa nchi yetu na wamekuwa wakifanya hivyo kupitia mitandao ya kijamii.

Binafsi nimekuwa nikikerwa sana na hawa watu waliokosa hekima na hata chembe ya heshima na adabu ndani ya mioyo yao.

Pengine ni mihemuko ya kiasiasa walio nayo kutokana kujenga mifumo ya siasa za kishabiki ndani yao.

Mimi kama raia mwema na mzalendo wa kweli, nimekuwa nikiwaza kitu kwamba mbali na adhabu za kuwapeleka mahakamani naishauri serikali yangu iwaongezee na adhabu nyingine ya kuwanyang'nya passport zao za kusafiria kwasababu passport ni mali ya serikali kupitia taasisi yetu ya uhamiaji.

Hivyo nawaomba uhamiaji wawanyang'anye passport hizo kwasababu wemeshindwa kuzitumia kwa heshima na adabu.

Lakini pia nawashauri TCRA watafute vijana wabobezi kwenye fani ya mitandao ili wawafuatilie watu kama hawa popote walipo. Kwasababu haya mambo yanawezekana.

Mbali na kufuatilia wezi wanao tutapeli fedha kwenye mitandao, tafadhali TCRA isaidieni serikali kufuatilia taarifa za watu wanamna kama hiyo. Kama mmekosa vijana hao mnaweza kuomba ushauri kwenye kitengo cha mawasiliano nchini China wao wanafanyaje.

Ningependa swala la kunyang'nya passport lihusiane na watuhumiwa ambao wanaitukana Serikali wakiwa nje ya Tanzania. Pamoja na watuhumiwa ambao wanamtukana Rais wakiwa nje ya mipaka ya Tanzania.

Mfano mtuhumiwa anayewaita waandishi wa habari na kumtukana Rais pamoja na serikali ya Tanzania mbele ya waandishi wa habari hao nje ya mipaka ya Tanzania. Sasa kwa vile passport ambayo ni mali ya serikali ndio imempeleka huko na hiyo passport ni mali ya serikali, sio vibaya mtuhumiwa huyo akanyang'anywa hiyo passport.

Pili mtuhumiwa anaye kwenda kwenye kituo cha kurusha matangazo ya habari nje ya mipaka ya Tanzania na kuanza kulisimanga vibaya taifa letu pamoja na kumsimanga vibaya Rais wetu.
Sasa kwa vile passport ambayo ni mali ya serikali ndio imempeleka huko na hiyo passport ni mali ya serikali, sio vibaya mtuhumiwa huyo akanyang'anywa hiyo passport.

Kwa hivyo ili kumfunza adabu mtuhumiwa huyo inatakiwa anyang'anywe passport ili abaki ndani ya mipaka yetu ajifunze jinsi kuheshimu taifa lako akiwa nje ya mipaka ya taifa letu.

Mtuhumiwa mwengine ni yule ambaye anatukana viongozi kwa njia ya mtandao ila akiwa nje ya mipaka ya Tanzania. Anapata uhuru wa kufanya hivyo eti kwa vile yuko nje ya Tanzania.
Sasa huyu naye inatakiwa anyang'anywe passport ya serikali ili atulie ndani ya mipaka yetu ajifunze jinsi ya kuheshimu taifa letu.

Kama hujanielewa naomba urejee hii attachment.
From Huawei P40 Pro.png

Wenu katika ujenzi wa taifa,
Meneja wa Makampuni.
 
Napinga na kutokuunga mkono mtu yeyote kutukanwa, achilia mbali Rais. Hilo halikubaliki katika jamii yeyote ile ya wastaarabu. Lakini pia inategemea unatafsiri vipi matusi?

Hao TCRA wanahangaishwa na vitapeli vinavyoibia watu kwa sms za miamala na mambo madogomadogo ya uhalifu wa kimtandao sijui hadi na hilo hadi Rais awatishie?

Rais ajikite kwenye mambo ya msingi akiongozwa na katiba, sheria na kufuata utawala bora, atapunguza kwa kiasi kikubwa sana matusi ya rejareja.

Hayo mapendekezo yako ya hati za kusafiria ni mchakato wa kisheria. Watatolea maelezo wataalam.
 
Sioni kama serikali inaweza tumia rasilimali zake kumfuatilia kila mtu anayeitukana nchi na viongozi wake akiwa nje ya nchi au nyuma ya keyboard. Kuna mambo mengi sana ya kufanya kuiletea maendeleo nchi kwa faida ya wananchi wanaoishi nchini
Wanaotukana ni wa kupuuzwa kwani wanaamini huko waliko ndio kwao
 
We ni mgambo tu tena uliefundishwa na mgambo mwenzio , mzalendo halisi hawezi kuwa empty hivi wazalendo tunawajuwa na tabia zao za kizalendo zinaonekana unatetea matapeli wenzio ujiite mzalendo????
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom