USHAURI KWA SERIKALI: Mikoa kame Tanzania iwekewe lengo la upandaji miti ili kurudisha hali ya jangwa

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
5,278
2,000
Ni ukweli kwamba Mikoa kama Singida, Dodoma,Sehemu za Manyara,Shinyanga,Chunya na Tabora inakabiliwa na ukame au hali ya jangwa iliyokithiri kiasi kwamba maeneo haya yamekuwa yakiathiri upatikanaji wa mvua katika sehemu kubwa ya nchi.

SASA, Ninaishauri serikali iweke mkakati wa kuhakikisha mikoa hii inapanda miti alau milioni 3 kila mwaka hadi kiasi kinachostahili kifikiwe....serikali za wilaya,tarafa,kata na vijiji husika kwenye mikoa tajwa zipewe agizo kuhakikisha kila mwananchi kwenye maeneo hayo anatunza angalau miche miwili ya miti jirani na maeneo yake ya makazi kwa kipindi chote cha mwaka...kwa kufanya hivi nina uhakika ndani ya miaka mitano hadi kumi tatizo la ukame litaondoka na mvua zitarudi kwa wingi hatimae wananchi kuneemeka.

Kwa mujibu wa tafiti rasmi ukiwemo utafiti wa IntactForests.org, sababu kuu zinazochangia upotevu wa misitu ni pamoja na:

1. Uvunaji miti kwa ajili ya Mbao (37%),
2. Upanuzi wa mashamba kwa ajili ya KILIMO (28%),
3. Wanyamapori (21%),
4. Ujenzi wa miundombinu hasa barabara na migodi,mabomba,umeme nk (12%).

Hivyo basi serikali ifikirie kuweka mikakati kabambe itakayozuia upotevu wa miti kwa kuweka adhabu kali kwa yeyote atakaepatikana na kosa la kukata mti.

Aidha uwekwe mkakati anuai wa kuwafunza wananchi matumizi ya nishati mbadala za kupikia kwani mkaa na kuni ni sababu kubwa ya upotevu wa misitu.

Tunaihitaji sana misitu kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho......ushahidi upo wazi mikoa ya Tanzania yenye uoto wa kutosha wa misitu imekuwa ikipata mvua kwa kiasi cha kadri au kuridhisha.....hivyo mkakati huo uende kwenye mikoa hiyo niliyoitaja..............kwa kuanzia Halmashauri kwenye mikoa inayokabiliwa na tatizo la ukame ukiwemo mkoa wa Dodoma zinaweza kwenda kujifunza katika Mkoa wa Kilimanjaro ambao umekuwa na sheria madhubuti za utunzaji misitu na miti....

SERIKALI ILICHUKUE SUALA HILI KWA UZITO UNAOSTAHILI IKIWA TUNA NIA NJEMA NA VIZAZI VIJAVYO VYA TANZANIA
 

mtzedi

JF-Expert Member
Dec 13, 2011
3,693
2,000
Kurudisha hali ya jangwa?
Au ulimaanisha kupunguza hali ya jangwa?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom