Ushauri kwa Serikali: Mh. Rais Magufuli, Waziri wa TAMISEMI (Jaffo), Waziri wa Ardhi (Lukuvi)

Ngokongosha

JF-Expert Member
Feb 9, 2011
3,402
7,567
Waheshimiwa poleni na majukumu, kazi mnayoifanya si ndogo ingawa wengine wanabeza.

Napenda kushauri yafuatayo yawezekana mkawa tayari mnayafanyia kazi but kama yataonekana ni mawazo mapya yenye kujenga nalo ni jambo jema. Naona ni vizuri tuwepo hata wale tunaoweza kushauri bila matusi naamini hii ni njia njema yenye kulinda heshima na utu.

JAFFO
Nimeisikiliza hotuba yako nashukuru kuna mambo mengi yanazidi kufanyika, naomba kushauri yafuatayo:

Katika ujenzi wa shule nashauri serikali ipitishe ramani moja itakayotumika kwa shule zote nchini Kama mlivyofanya kwenye vituo vya afya. Sasa hivi halmashauri, wananchi na serikali naona kila mtu na ramani yake mwingine unakuta ramani ya Treni, mwingine mraba, mwingine msitatili nk.

Ujenzi wa Stendi za mabasi
Nashauri zijengwe za kisasa kila pale sehemu mradi upo, Stendi hizi zinakuwa na gates na bus zinakuwa zinasimama kwenye gate inapohitajika, Kama file airport basi linakuja linaegesha watu wanapanda au kushuka kisha linapisha jingine, sehemu ya abiria kungojea kunakuwa na maduka na restaurants na si wamachinga kupunguza usumbufu na wizi kwa abiria, pia screens kuonyesha muda wa basi kufika au kuondoka, na speakers PA system kwa ajili ya matangazo nk.

Miradi ya barabara kwenye miji, halmashauri, manispaa na majiji
Napongeza huu mradi ila nashauri iboreshwe hasa maeneo ya mjini serikali iweke utaratibu wa barabara za mjini, mfano miji mikubwa hasa majiji yana kitu kinaitwa Central Business District (CBD), sasa unakuta barabara zinajengewa zina mifereji ya maji iliyo wazi, hii tayari ni uchafu na haisaidii miji yetu kupendeza, nashauri barabara angalau za mijini hasa CBDs mifereji ifunikwe, ziwe na taa, ziwe na paved pedestrian walks, na ziwe na alama zote za barabarani ikiwemo majina ya mitaa, wamachinga wadhibitiwe kupanga biashara kwenye nguzo za majina ya mitaa au alama za barabarani ili watumiaji wa barabara wazione kwa urahisi,

JAFFO & LUKUVI

Mipango miji

Nashauri tuangalie matumizi Bora ya Ardhi na utunzaji wa mazingira, miji kukua haina maana maeneo yaliyo karibu yageuzwe makazi hata Kama yanafaa zaidi kwa Jambo jingine, nitatolea mfano mwanza eneo la nyamhongholo hili lilikuwa ni eneo lenye Ardhi nzuri kwa kilimo ila liligeuzwa kuwa makazi nafikiri ilikuwa vizuri kulihifadhi kwa kilimo hata cha mbogamboga na watu wangepimiwa kujenga eneo la kisesa. Kuwa na maeneo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya mashamba mjini yanafanya hata miji ipumue, ukizingatia hata viwanja tunavyopima hatuweki utaratibu wa kuacha eneo kwa ajili ya recreation.

Maeneo ya milimani na mabondeni ambayo hayafai kwa ujenzi yaainishwe na watu wa Ardhi ngazi ya halmashauri wawe wanapita kukagua na kuzuia ujenzi wowote ulioanza, barabarani kuna polisi na traffic officers ndio maana madereva wanatii sheria, wizara ya Ardhi na watu wa mipango miji barabara zenu ni maeneo yote ya Ardhi yanayotakiwa kusimamiwa angalau mzunguke mara moja kwa mwezi, ukimkuta mtu kajenga msingi ukambomolea Kesho yake hatafanya hivyo, na atakuwa Askari akimuona mtu mwingine atampa tahadhari ila Kama wahusika wanakaa ofsini tu informal settlements zitazidi kuongezeka kwa Kasi.

Upimaji viwanja nashauri uwe wa kisasa, viwanja nyetu kila vikipimwa vina mtindo wa box yaani barabara nne zimezunguka, hivi architects wetu style Yao hi nyumba hii na nyumba hii zitegeane matako, na nafasi Kati ya nyumba ni ndogo, natolea mfano ihumwa satellite, safari city Arusha, kawe city dar, michoro ya hizi projects ni mizuri nashauri wapima ramani wa halmashauri wajifunze na pia vitu Kama chemichemi, miti ya kipekee, na hata vichaka visiharibiwe Bali vijumuishwe kwenye upimaji na viwe protected sio lazima tujenge kila mahali.

Nashauri NHC waanze kujenga nyumba kwa staili ifuatayo:
Maeneo ambayo ni informal settlements waanze kuyapunguza kwa kujenga maghorofa Kama ya magomeni,
Serikali kupitia Nhc ichukue maeneo ya wananchi yaliyo holela ijenge kisha iwape nyumba waliopisha maeneo, hivyo automatically serikali itajikuta kuna maeneo inabakiwa na viwanja pamoja na nyumba za kupangisha au kuuza, mfano magomeni najua kuna units zingine zitabaki ambazo ni faida au kupunguzia gharama.

Haya mambo ya kusubiri investors tutakesha, mfano nilikuwa nasoma kuhusu jiji la mwanza kwamba wana mpango wa kuwatoa watu wa milimani kwa kujenga nyumba na kuwapa wananchi na wanasubiri investors wa kushirikiana nao, Mimi nashauri watenge bajeti ya 1bilioni kila mwaka kisha kila mwaka wanajenga ghorofa la bilioni moja mfano liweze kuchukua familia 5, familia 5 zinakuwa zinaondoka milimani kila mwaka hii ni Bora kuliko kusubiri investors ambao hujui watapatikana lini.

Mh Raisi, Jaffo, Lukuvi

Ulipaji fidia kupisha miradi

Napendekeza wananchi wasilipwe fidia ila serikali iweke utaratibu ukivunjiwa nyumba kupisha mradi serikali ikujengee nyumba badala ya fidia.

Watu wakipewa fidia huenda kujenga hovyo na Kesho yake Kama kuna mradi mwingine serikali inajikuta inalipa tena, nashauri fidia ilipwe kama ilikuwa shamba au jengo la biashara. Mfano kuna kaya zinatakiwa kulipwa fidia kupisha BRT phase 3, serikali itafute eneo ijenge maghorofa Kama ya magomeni wanayojenga kutokana na pesa za fidia kisha wananchi wanahamia wanapisha mradi na wanapata makazi Bora hata kama gharama zitazidi kidogo ni Bora kuliko watu wanavyojenga hovyo bila plan.

Haya ni baadhi ya mawazo yangu yawezekana yakawa si sahihi Sana Kama ninavyofikiria ila si vibaya kuyatoa.
Ninayo mengi ila kwa Leo ni hayo tu.

Nitaendelea kuchangia zaidi kadri bajeti zinavyosomwa.

Ni Mimi
Mbunge wa Mitandaoni.
 
Mawazo mujarabu sana,hao viongozi kwa muda huu akili zitakuwa kuhusu kurudi tena Bungeni.Kwakuwa maandishi yanaishi hata hao wengine watapitia humu wayasome hayo madini.
 
Viongozi wanaogopa kutekeleza mipango mizuri kwa sababu zifuatazo;
1.kwa kuogopa wapiga kura na
2.tamaa na ubinafsi
 
Ushauri mzuri sana tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom