Ushauri kwa Serikali kwamba sasa ni wakati wa kutumia akiba yetu kumalizia ujenzi wa reli SGR kipande cha Makutopora hadi Mwanza

Yusuf Kashaju

Member
Oct 20, 2019
57
89
Serikali inashauriwa kutumia akiba yetu ya Fedha za kigeni ( draw down) kugharamia ujenzi wa reli ya SGR kipende cha kuanzia Makutopora hadi Mwanza.

Hatua hii itaepusha taifa kuongeza deni la taifa. Vile vile uamuzi huo utapunguza hasara taifa linayoipata kwa kuendelea kulimbikiza fedha nyingi za kigeni.

Benki Kuu wakitoa tathmini ya hasara tunayopata kama taifa kwa kuendelea kulimbikiza mabilioni ya Dola watu wengi watashangaa. Ukweli ni kuwa tunapata hasara kama taifa kulimbikiza fedha za kigeni, tena katika sarafu ya aina moja.

Tunatakiwa hazina hii ambapo kwa maoteo ya muda mfupi haturajii kuwepo kwa janga, tuitumie kukamilisha mradi huu ambao ni muhimu na wa lazima katika kuingia kwenye uchumi wa Kati.

Vile vile Wizara ya Fedha na Mipango inashauriwa kuonyesha flexibility katika kutekeleza sera zake za uchumi, wala haitakiwi kujitetea kama alivyofanya Waziri wa Fedha na Mipango jana.

Duniani kote hakuna nchi yenye sera za uchumi zinazojitosheleza. Kinachofanyika ni kuzifanyia mapitio mara kwa mara ili kuona kama zinafikia malengo tarajiwa katika utekelezaji wake.

Hivyo, Wizara ya Fedha na Mipango inatakiwa kuzifanyia mapitio sera zake ili kupata majibu ya malalamiko ya watu kuhusu hali nguvu ya maisha, inawezekana sera inayotekelezwa bado hajawa na matokeo tarajiwa na kunahitaji sera mbadala.
 
Kuna pesa mchina ametupa kama mkopo, nakumbuka si chini ya Trillion 10 niliona kwenye taarifa ya habari. Ili kumalizia ujenzi wa reli ya kati!
 
Back
Top Bottom