Ushauri kwa Serikali kuhusu TARURA na Wizara ya Ujenzi

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
5,427
2,000
Habari ndugu wana jukwaa,

Napenda kutoa ushauri kwa serikali iangalie uwezekano wa kuihamishia Tarura chini ya wizara ya ujenzi na uchukuzi kutoka Tamisemi na kuondoa mambo ya mawasiliano kutoka wizara ya ujenzi kupeleka wizara ya habari

Ili kuleta ufanisi masuala ya barabara yawe chini ya wizara husika ili Tamisemi wadili na mambo ya shule,vituo vya afya na utawala kwa kushirikiana na wizara zingine.

Leo hii ukienda kwenye kila shule ya mjini msongamano wa watoto ni mkubwa,samani ni tatizo,zahanati na vituo vya afya vimejaa watu kwa sababu ni vichache kuliko uhitaji sasa kwa hali kama hii ni busara serikali ikaona namna ya kuchukua ushauri

Sielewi kwa nini masuala ya minara ya simu tcra sijui tehama yako chini ya wizara ya ujenzi badala ya wizara ya habari
 

wankuru nyankuru

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
243
500
Hivi sasa ni takribani miaka 2 sasa tangu ofisi za TARURA zianzishwe kwenye mikoa na halmashauri Kwa lengo la kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara mpya na ukarabati wa barabara hasa kwenye miji na vijijini.

Kwa survey niliyofanya tangu mvua inyeshe nimeshuhudia barabara za mitaani kwa sasa ni mbaya kuliko hata ilivyo kuwa awali kabla ya kuanzishwa kwa hii taasisi.

Yaani hadi nikawa najiuliza si ni bora tu hii kazi ingebaki kuwa chini ya tanroad na halmashauri husika.

Hawa jamaa wamekaa tu maofisini hawana lolote ,hawafanyi ukarabati wa barabara na cha kushangaza siku moja nimetembelea barabara moja hivi nimekuta wamechonga tena msimu wa mvua huu na barabara yenyewe imeshaharibiwa na mvua tiari hadi sasa. Ukiangalia mitaro waliyoijenga unaweza kusema hawa watu walianzisha hii taasisi kwa kufuata mishahara mikubwa tu lakini Kwa sasa ni kinyume chake.

Sasa kama wananchi wazalendo hebu tutoe ushauri kwa TARURA Kwa kurefer hali ya barabara huko uliko.

Unawashauri kitu gani ili kiwasaidie kuboresha utendaji kazi wao???

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom