Ushauri kwa Serikali kuhusu mtu akifa hali ya kuwa kwenye simu zake kuna hela

hata mimi

JF-Expert Member
Oct 17, 2017
1,356
1,437
Nilisikia majuzi wabunge wanasema serikali inakosa pesa zinazoachwa kwenye akaunti za mitandao ya simu za mkononi wakisema kampuni husika zinavuna pesa hizo. Katika suluhisho waliloliona wao ni kwamba kuwe na utaratibu utakaowezesha fedha hizo zirudishwe serikalini

Binafsi yangu mimi naona hilo siyo sahihi badala yake wangesaidia mfiwa/mrithi wa marehemu apate fedha hiyo kwanza kabla ya kuwaza kuipeleka serikalini

Nilisoma sehemu fulani kwamba ukitaka kuipata fedha iliyopo kwenye simu ya mtu aliyekufa itakubidi upeleke mlolongo wa viambata (wameviorodhesha huko niliposoma) upeleke kwenye (ofisi za) mtandao husika ndipo wakupe PIN ya marehemu

Jambo la ajabu ni kwamba sikuona popote maelezo ya kuhusu wao mtandao wanachukua fedha hiyo iliyoachwa kwa masharti yapi (kwa viambata gani)

Kwahiyo ushauri wangu aangaliwe kwanza mrithi arahisishiwe namna ya kupata fedha hiyo (iwe ndio namba moja) halafu ikitokea sasa salio likawa dogo au hata kubwa ila akaamua kuliacha kwa hiari yake ndipo tuhamie upande wa serikali wachukue zote (serikali wawe ni namba mbili)

Hatahivyo, nakazia kuwa HAKUNA KUWAACHIA HATA SENTI HAWA MITANDAO, yaani ikitokea labda laini ina sh 50.01 (maana yake haihamishiki hata kwenda airtime labda utupie nyingine kwanza) kisha mrirhi akasema ameridhika (akaipuuza) basi serikali ivute hiyo sh 50.01 yote kama ilivyo IKAFANYE MASWALA YA KIMAENDELEO KWA WANANCHI
 
Hapa wahanga tuchukue somo. Unaishi na mwenzako: mke au mume. Au basi hauko katika hili kundi, una kaka, dada, mdogo au mkubwa wako, achilia mbali wazazi. Unakosa hata mtu mmoja wa kishirikisha siri zako hasa za mapato na akiba ili likitokea lolote wanufaike inakuja kuwa neema kwa wasiokuwa na machungu na uhai wako!!

Nini maana ya viapo makanisani na misikitini?

Au tuseme viapo vilibadilika vinasoma "Tutavumiliana kwa raha, shida ni za kwako!"
 
Miye namba yangu ya siri mwenzangu anaijua, mama na mdogo wangu wa mwisho anaijua km nimedanja hawatapata kitu.
 
Back
Top Bottom