Ushauri kwa Serikali kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Escrowseal1

JF-Expert Member
Dec 17, 2014
4,429
4,220
Mradi wa Bagamoyo ni moja ya miradi iliyoko mioyoni mwa watanzania nikiwemo Mimi japo wengi hawasemi Kwa sasa. Ni Kati ya vitumbua vya Taifa vyenye mchanga. Huu mradi ni kipimo Kwa Serikali ya Mama Samia maana ni kati ya miradi tukiingia kichwa kichwa mchina atakuwa kapata upenyo wa kutukaba kama anavyowakaba baadhi ya mataifa anakotekeleza miradi yake Kwa janja janja.Tanzania kama nchi hatuna sababu ya kufika hapo kwani hatuko desperate kiasi hicho.

Ushauri wangu Kwa serikali, ili kujenga Imani kwetu Sisi wenye nchi nadhani share yetu ituwezeshe kuwa majority ama Kwa serikali kama serikali au igawe hisa Kwa mwananchi mmoja mmoja ama makampuni yetu kitanzania kuepuka kubinafsisha jikoni ama chumbani kwetu. Mfano ni Kwa bwawa lililojengwa na Ethiopia Kwa kuwatumia diaspora nasi tunao diaspora wetu wapeni hisa ili tusafishe hiyo curse iliyopo mbele yetu japo kuna watanzania mmoja mmoja huwa wanajitokeza kila mara kututia Moyo kuwa mradi ni Safi hauna shida .

Mwisho shukrani zangu Kwa JF Kwa kutupatia uwanja wa ku speak our minds
 
Shida ni kwamba kumekuwa na maoni binafsi na hisia za watu binafsi kuhusu mradi huu kila mtu anasema lake mwisho wananchi wanashindwa kuamini nani yupo sahihi na nani hayupo sahihi ni muda sasa serikali kuweka huo mkataba wazi hii ndo njia sahihi ya kuondoa sitofaham kuhusu mradi huu

Yangu ni hayo tu
 
Shida ni kwamba kumekuwa na maoni binafsi na hisia za watu binafsi kuhusu mradi huu kila mtu anasema lake mwisho wananchi wanashindwa kuamini nani yupo sahihi na nani hayupo sahihi ni muda sasa serikali kuweka huo mkataba wazi hii ndo njia sahihi ya kuondoa sitofaham kuhusu mradi huu

Yangu ni hayo tu
Mwalimu nyerere alisema ukiwa mfalme hifai ukapatwa japo na tuhuma hata kama si za kweli. Bandari mkuu nailinganisha na Tanesco ,huu mradi ni mboni ya jicho la Taifa letu. Tuhuma zake ni kubwa ziwe kweli ama la hazitakiwi kupuuzwa.
 
Back
Top Bottom