Ushauri kwa Serikali kuhusu mikopo tunayopokea kutoka kwa wahisani

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Kukopa kutoka nje ni jambo jema sana ikiwa utatumia mkopo husika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.

Tangu tupate uhuru 1961 mikopo tuliopata ni mabillioni ya dollar za Kimarekani. Tujiulize kuwa thamani ya mikopo hiyo na hatua ya maendeleo tuliopiga mpaka sasa inaoana?

Wahisani wengi mikopo yao wanaelekeza mara nyingi kwenye masuala ya kujenga uwezo kwa maana ya training kamwe hawataki mikopo yao ijenge vituo vya afya, madarasa, skimu za maji, barabara n.k.

Nitoe mfano wa TASAF.

TASAF imetoa ufadhili kwa Tanzania sasa ni zaidi ya miaka 20 lakini misaada yao wanaitafsiri kuwa ni kumuondolea watu umaskini. Walipoanza walianzia na ujenzi wa miundombinu kama Vituo vya Afya na baadaye wakaja na dhana ya kujenga uwezo baadaye sasa wanagawa fedha kwa kaya masikini.

Binafsi mimi ninatofautiana nao sana. Kwa nini msaada wao usilenge kujenga miundombinu kama dispensari, vituo vya afya, shule , barabara ili hao maskini wafaidi wote kuliko kutoa fedha na fedha yenyewe ni kiduchu au kwanini wasiwajengee hao maskini nyumba za kuishi kuliko kuwapa fedha?.

Nimshukuru sana Mhe. Rais hata fedha za UVICO-19 wahisani kwa maoni yao walitaka kuelekeza kwenye masuala ya kuwajengea wananchi uwezo yaani training lakini Mhe. Rais akaelekeza zijenge miundombinu na sasa wote tumeona mazuri yaliyotendeka na tutayafaidi miaka na miaka.

Kwa hitimisho naishauri Serikali misaada yote tunayopokea ielekezwe kwenye miundombinu na siyo masuala ya kujenga uwezo.

Kama kujenga uwezo basi itengewe asilimia ndogo sana lakini asilimia kubwa ya mikopo ielekezwe kwenye miundombinu.
 
Back
Top Bottom