Ushauri kwa Serikali kuhusu mapato kwenye nyumba za kupanga

babilas25

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
471
333
Heshima kwenu wakuu

Serikali ya Awamu ya 5 imejikita katika kukusanya kodi na Mhe. Rais amekuwa akisisitiza kulipa kodi na umhimu wake.

Lipo eneo moja ambapo Serikali inapoteza mapato makubwa, kwa utafiti wangu usiokuwa rasmi zaidi ya watanzania 80% waishio mjini wanaishi kwenye nyumba za kupanga.

TZ Gov ikiweka mfumo mzuri wa kila mpangaji alipe kodi itasaidia kuongeza mapato.

Nini kifanyike:
1: Madalali wote waondolewe
2: Nyumba zote ziweregistered kwa watendaji na wenyeviti wa mitaa.

Mpagaji atakwenda kwa mtendaji au M/Kiti wa Mtaa anaotaka kupanga atapata tarifa za nyumba zote zilizopo kweye mtaa huo, akishalipa Gov itapata kodi yake kuliko ilivyo sasa madalali wanapga pesa na halipi kodi na wanachangia kupanda kwa bei ya vyumba.

Ni mtazamo wangu kwa Tz_Gov

Babilas Jr
babilasfikiri@gmail.com
 
Namba ya simu ingeweza kurahisisha mawasiliano kwa haraka zaidi.

Cc: wasaka teuzi wote.
 
Ili hao madalali warudi kukaba siyo? au unawapeleka wapi?

Kuwaondoa madalali, wapiga debe makangomba ni sahihi mkuu.

Hawa wanapelekea hata bei kupanda kwa ujanja ujanja usio na tija.

Hawana added value. End result bila madalali hawa hata bei zitashuka.
 
hao watendaji na wenyeviti wa mtaa ndio wapigaji kama madalali, kazi haina mshahara lakini wanahonga waipate
 
Back
Top Bottom