Ushauri kwa serikali kuhusu elimu ya awali Tanzania

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,074
1,856
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano

Ninao ushauri mdogo kuhusu elimu yetu ya awali nchini.

Kwanza niwapongeze sana TIE kwa miongozo sahihi nayakisasa ya namna ya kumfundisha mtoto, hasa baada ya kuleta mtaala mpya unaojenga UMAHIRI/COMPETENCE BASED CURRICULUM

Shida iliyosalia nikwamba, walimu wengi wanaofundisha watoto Hawaujui kabisa huu mtaala, pamoja na serikali kutumia pesa nyingi kutoa Seminar kuhusu huu mtaala, lakini bado haufuatwi na walimu. Zipo sababu zinazopendekezwa kufeli kwa mtaala huo kutekelezwa:

1. Hakuna walimu wa awali wenye elimu kubwa ya kuweza kuupambanua huu mtaala
2. Hakuna support ya kutosha kutoka wizara ya elimu kugharamia mahitaji ya elimu ya awali
3. Hakuna walimu wa kutosha wa kuusimamia mtaala wa elimu ya awali
4. Shule binafsi za elimu ya awali hazina huu mtaala na ndiyo waliochukua jukumu hili la kufundisha watoto wetu
5. Bado kuna mtazamo hasi wa kutochukulia maanani elimu ya awali
6. Wakaguzi elimu ya awali hata hawaijui na huenda hawapo

NINI KIFANYIKE
Serikali kupitia wizara, iwatumie wahitimu wa elimu ya juu na diploma kufundisha elimu ya awali na kuusimamia mtaala huuwa CBC, hii nikwasababu wameandaliwa kwa kuusoma mtaala huu mpya.

Vyuo binafsi vya ualimu wa awali vipitiwe kuona Kama vinawalimu wenye uwezo wa kuandaa walimu wa awali, wengi wanaofundisha, ni walimu wa elimu za juu wasiokuwa na uelewa na hii elimu, matokeo yake wanaiahia kumfundisha mwalimu-mwanafunzi saikolojia ya mtoto tu

Serikali iipe kipao mbele elimu ya awali kwa kujenga madarasa mengi ya watoto kwa kila shule na iajiri walimu wa awali wenye sifa stahiki , walimu wapo.

Kuwepo na wakaguzi wabobezi wa elimu ya awali kuliko ilivyo sasa
Daycare Zisimamiwe zaidi maana imekuwa biashara, wanaozisimamia hawana ujuzi wa kutosha na wanakaa na watoto muda mrefu na wakiwekeza katika maarifa madogo kwa watoto, japo wamesaidia sana kupunguza mzigo kwa serikali, hofu yangu ni baada ya muda mfupi ujao, Tanzania itakuwa na watoto wasio wabunifu kabisa.

NB; Taifa Lina watoto wengi sana kwasasa, serikali ikiwaona siyo kitu, itakuwa na sawa na kuotesha msitu ukauacha bila usimamizi, baadae unataka uje uvune mbao, hakika utakutana na kuni tu.

Ahsanteni
 
Kwa mujibu wa Maria Montessori, makuzi ya mtoto yako katika hatua kuu mbili: Miaka 0 - 3; na miaka 3 - 6.

Vitabu vya The Growth of the Mind na cha The Absorbent Mind vingekuwa ni lazima kwa kila mzazi kuvisoma, kama ingewezekana. Maana wazazi wengi husubiri watoto wafikie umri wa kwenda chekechea, wakidhani hapo ndio mwanzo wao wa elimu. Kumbe mtoto anaanza kupata elimu kuanzia day zero.
 
Back
Top Bottom