Ushauri kwa Serikali katika kuongeza mapato na ajira kutoka kwenye sekta ya madini

Oct 12, 2014
76
45
Mnamo mwaka 2017-2018, kampuni ya Acacia inayomiliki Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu ilisimamisha wafanyakazi zaidi ya 1000. Hii ilitokana na usimamishaji au usitishaji wake katika kuzalisha mchanga wa dhahabu au makinikia ambayo Serikali ilizuia usafirishaji wa unbeneficiated ore. Hii inamaanisha only finished or semi-finished products ndizo zitakazoruhusiwa kusafirishwa nje ya nchi (;Acacia yapunguza wafanyakazi tena). Hii inaonesha kua uzalishaji wa mchanga wa dhahabu tu ulikua unaleta ajira zaidi ya watu 1000. Pia according to Hotuba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dr. P. Mpango ni kua mapato ya serikali yamepungua kutokana na kushuka kwa PAYE. Hii imetokana na watu kuachishwa kazi (including watu wa migodini) + kupungua kwa ajira mpya including migodini (maana nao wanazalisha ajira mpya (Dr Mpango akiri uchumi wa nchi kuporomoka - JamiiForums). Nini kifanyike kwa Serikali yetu pendwa?

Ushauri wangu kwa Serikali

Ni vema Serikali ikaingia kwenye biashara ya kuwekeza kwenye smellter ambayo itakua inaprocess huo mchanga wa dhahabu na kuongeza thamani ya madini yetu. Tusitegemee kuunganisha nguvu na wawekezaji ili kujenga smelter maana tutawasubiria sana mpaka tutachoka. Mfano, mwaka 2015 Serikali na mining giant PT Freeport Indonesia, walikubaliana kujenga smelter in Papua (Govt, Freeport agree to build smelter in Papua). Mwaka 2017, mtaalamu wa mambo ya nishati na Executive Director wa Center of Energy and Resources Indonesia (CERI), Ndugu Yusri Usman alishauri ni bora serikali ikajenga smelter wenyewe kuliko kuwategemea hao wawekezaji wa PT Freeport Indonesia ambao ndio wanaochelewesha ujengaji wa hiyo smellter (Government encouraged to go it alone in building new copper smelter). Hii inaonesha kua, kama Serikali inao uwezo wa kujenga ssmelter basi ni bora wakajenga wenyewe ili kuweza kuboresha sekta ya madini na hata sekta nyingine zinazotegemea madini ili ziweze kuendelea mfano Infrastructure inadevelop katika vijiji kwa haraka kama kuna madini, mazao, biashara n.k.

Njia nyingine ni serikali kuruhusu usafirishaji wa unbeneficiated ore au makinikia na inatakiwa sasa kuintroduce au kuincrease exportation levy. Kuongezeka kwa exportation levy kutalazimisha kampuni zinazozalisha au wanunuzi wa makinikia kuwekeza kwenye smelter katika nchi husika. Ripoti ya Ernst and Young (2013) ya Business Risks facing Mining Industries, inaonesha kua China ilikua ina export unbeneficiated iron ore from Indonesia to China. Baada ya kuletwa kwa exportation levy ya 25% mwaka 2012 na kuongezeka mpaka 50% mwaka 2013,ilimlazimu China kujenga smelter nchini Indonesia.

Je ni nini faida itokanayo na uwekezaji wa Serikali kwenye smelter kwa nchi ya Tanzania?

FAIDA

Faida zitokanazo na serikali kuwekeza kwenye smelter ya kuprocess mchanga wa dhahabu ni:
  • Kuongezeka kwa employment rate kutokana na migodi kurudisha wafanyakazi walioachishwa kazi kama nilivoainisha hapo juu na kuleta ajira mpya. Pia Serikali itaweza kutoa ajira mpya kwa wananchi katika hiyo smelter mfano waendesha mitambo, walinzi, wachenjuaji madini na wengineo.
  • Kuongezeka kwa ujuzi kwa watakaoajiriwa katika smelter na hii inatokana na kufanya kazi karibu na watu wenye ujuzi na hii pia itawasaidia katika kupata elimu mpya.
  • Kuongezeka kwa kodi ya Serikali kutokana na migodi kurudisha wafanyakazi wake wa zamani au kuleta wapya na pia Serikali kuajiri watu wapya and hence kuongezeka kwa PAYE. Pia ongezeko la revenue kutokana na kuongezeka kwa thamani ya dhahabu.
Ni muhimu pia Serikali ikalazimisha Vyuo vyetu kama U.D.S.M., U.D.O.M., D.I.T. na M.R.I. kuintroduce Course ya Beneficiation Economics ili watu wajue sababu za nchi kutofanya value addition katika minerals. Pia itasaidia watu kujua ni njia zipi Serikali inastahili kutumia ili iweze kuzilazimisha kampuni kustart mineral beneficiation bila kuathiri ajira na mfumo kodi katika nchi husika

Kuongeza thamani ya madini huleta ongezeko la mapato, elimu, ujuzi na ajira

Mzalendo Mwenzenu
 
Back
Top Bottom