Ushauri Kwa Serikali, kama wanaitaji maendeleo kwenye nchi yetu mfumo wa elimu inabidi ubadilishwe

Sam mirror

JF-Expert Member
Sep 29, 2018
1,462
2,219
Wakuu habari za muda huu, poleni na majukumu ya kujenga taifa.

Jambo ambalo naomba tujadiliane ni kuhusiana na MFUMO WA ELIMU TANZANIA.......ni Kwamba Toka nimekua mpaka kufikisha umri huu sijawahi elewa mantiki ya Elimu ya kukariri vitu wakati nchi nyingine zinafanya ugunduzi wa mambo mbalimbali. Ni Kwamba viongozi wa serikali awalioni hili swala Au wanafanya makusudi huwa najiuliza na moyo unaniuma pale msomi wa Tz anapojiita msomi Kwa kukariri vitu visyomsaidia nchi yangu Tz wapi unaenda...........

Huwa nashangaa sana viongozi wa serikali, wananchi pamoja na mihimili yote ya serikali inasisitiza swala La elimu isiyo na tija Kwa watanzania.

Kwanza nataka tujue nini maana ya Elimu- ni ujuzi anaoupata mwanafunzi ili kukwamua jamii yake kutokana na changamoto inayokutana nayo. Tujiulize wasomi wetu wametatua changamoto zp engineer wamegundua nn afu tunajiita wasomi ukweli unauma ila utabaki kuwa ivo.....

Ushauri Kwa serikali ni kama wanaitaji maendeleo kwenye nchi yetu mfumo wa elimu inabidi ubadilishwe ili kuendana na mfumo wa dunia............

Wakuu ayo ni mawazo yangu kuhusu mfumo wa elimu kama unalolote changia ili tubadili jamii yetu.................

Ni mimi mzalendo (Tz for change) 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
 
Back
Top Bottom