Ushauri kwa serikali: Jengeni njia ya ndani kwa ndani kuunganisha terminal mpya ya airport na ya zamani kutoka international kwenda domestic.

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,257
2,000
Naipongeza serikali kwa kazi nzuri ya kujenga terminal mpya ya airport, ambayo itatumika kwa ajili ya safari za kimataifa.

Jambo moja ambalo nimeona ni kasoro kubwa ni kutokuwapo na njia ya ndani kwa ndani kuunganisha terminal mpya na ya zamani ambayo sasa itatumika kwa domestic flights. Naisihi serikali kufanya mpango wa kujenga njia ya ndani kwa ndani ili abiria wanaounganisha kutoka domestic kwenda international au international kwenda domestic wasiwe wanatoka nje, bali wawe wana-transit kati ya hizi terminal mbili ndani kwa ndani.

Kumbuka pia kujengwa kwa hii corridor la ndani kwa ndani itatoa fursa nzuri kuweka banner za matangazo ambazo Mamlaka ya Viwanja itaingiza pesa nyingi. Na ikiwezekana njia hii iwe na sehemu ya "travelator" ile njia ambayo inatembea ili kufanya utembee kwa kasi zaidi.
 
TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
7,295
2,000
Wataalam wetu waliona hilo ila wakati wa uchambuzi yakinifu mtaalam wetu wa mapato akasema tunaweza kukosa mapato mengi.

Mfano wadanganyifu wanaoweza kupitisha rasilimali zetu moja kwa moja kwa kisingizio cha direct corridor.
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,257
2,000
Wataalam wetu waliona hilo ila wakati wa uchambuzi yakinifu mtaalam wetu wa mapato akasema tunaweza kukosa mapato mengi.

Mfano wadanganyifu wanaoweza kupitisha rasilimali zetu moja kwa moja kwa kisingizio cha direct corridor.
Haiwezekani Mkuu. Hili corridor linakuwa baada ya kupita eneo la customs, sasa tutakosaje mapato? Corridor linaanzia eneo la kucheck in upande wa Tarminal III na kuishia eneo la arrivals upande wa Terminal II. Na kanuni ya transition from international to domestic lazima uchukue mzigo wako kwanza na kisha kuu-check in upande wa domestic.

Tatizo tunakuwa na "wataalamu" ambao hawajawahi hata kusafiri kwenda nje.
 
semper saratoga

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
1,049
2,000
Mkuu nadhani hujamuelewa embu rudia tena kusoma taratibu utampata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,257
2,000
Mkuu nadhani hujamuelewa embu rudia tena kusoma taratibu utampata

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha! Nimekupata. Huyo ndio mtaalamu wetu wa mapato ndiye aliyesema waweke scanner upande wa domestic arrivals kukagua mizigo ya ndani toka domestic flights kabla abiria hawajaenda nyumbani!

Huwa kila nikipita na kifurushi changu cha mchele toka Mbeya nawauliza kama inabidi niulipie import duty!
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
12,835
2,000
Naipongeza serikali kwa kazi nzuri ya kujenga terminal mpya ya airport, ambayo itatumika kwa ajili ya safari za kimataifa.

Jambo moja ambalo nimeona ni kasoro kubwa ni kutokuwapo na njia ya ndani kwa ndani kuunganisha terminal mpya na ya zamani ambayo sasa itatumika kwa domestic flights. Naisihi serikali kufanya mpango wa kujenga njia ya ndani kwa ndani ili abiria wanaounganisha kutoka domestic kwenda international au international kwenda domestic wasiwe wanatoka nje, bali wawe wana-transit kati ya hizi terminal mbili ndani kwa ndani.

Kumbuka pia kujengwa kwa hii corridor la ndani kwa ndani itatoa fursa nzuri kuweka banner za matangazo ambazo Mamlaka ya Viwanja itaingiza pesa nyingi. Na ikiwezekana njia hii iwe na sehemu ya "travelator" ile njia ambayo inatembea ili kufanya utembe kwa kasi zaidi.
Ni wazo zuri. Ila vile vile wanaweza kuweka mabasi ya kutoa watu kutoka terminal moja kwenda nyingine. Ila ikiwepo corridor ni vizuri zaidi.
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,257
2,000
Ni wazo zuri. Ila vile vile wanaweza kuweka mabasi ya kutoa watu kutoka terminal moja kwenda nyingine. Ila ikiwepo corridor ni vizuri zaidi.
Mabasi ni gharama kubwa sana! Na utafanyaje, kwamba yanaenda kati ya terminal III na II saa zote, labda kila baada ya dakika tano?
 
Mikopo Chefuchefu

JF-Expert Member
May 15, 2017
3,399
2,000
Mkuu, ushwahi kufika pale? Kumbu kumbu yangu inanikumbusha kuwa huwa kuna corridor ya wazi imejengwa pale kati ya zile terminal mbili!
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
12,835
2,000
Mabasi ni gharama kubwa sana! Na utafanyaje, kwamba yanaenda kati ya terminal III na II saa zote, labda kila baada ya dakika tano?
Of-course kutakuwa na interval kulingana na utuaji wa ndege. Uwanja kama Hearthrow una utaratibu huu. Nadhani hata Zurich niliona train ya kusafirisha watu. Lakini wazo ulilotowa ni zuri zaidi. Halafu kuongezea... Hiyo terminal 2 nayo ifanyiwe ukarabati iwe kwenye hali nzuri.
 
TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
7,295
2,000
Nashukuru kama umenielewa.
Hahaha! Nimekupata. Huyo ndio mtaalamu wetu wa mapato ndiye aliyesema waweke scanner upande wa domestic arrivals kukagua mizigo ya ndani toka domestic flights kabla abiria hawajaenda nyumbani!

Huwa kila nikipita na kifurushi changu cha mchele toka Mbeya nawauliza kama inabidi niulipie import duty!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom