gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,305
- 3,327
Wafanyabiashara wakubwa wanaficha sukari kwa sababu kuu mbili.
Moja ni kutengeneza uhaba ili kuuza kwa faida kwa bei kubwa lakini la pili ni kutengeneza uhaba ili kuaminisha serikali kwamba kuna uhaba hivyo wapewe vibali waagize sukari kutoka nje.
Ikumbukwe kwamba sukari inayoagizwa kutoka nje inawapa faida kubwa wafanya biashara kuliko sukari wanayonunua kwenye viwanda vyetu vya ndani.
Nashauri serikali isitishe utoaji wa vibali kwa wafanyabiashara pale panapotokea uhaba badala yake utengenezwe utaratibu viwanda vyetu vya ndani vya sukari ndivyo viwe na mamlaka kuagiza sukari nje pale panapokua na uhaba.
Hili litaendelea kulinda viwanda vyetu vya ndani lakini pia linaweza kuondoa ufichwaji na uhaba wa sukari.